Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Mawasiliano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alama ya mawasiliano ya simu

Mawasiliano kwa kawaida hufafanuliwa kama kupashana au kubadilishana mawazo, maoni,hisia auhabari kwa maneno, maandishi auishara kufikialengo lililokubaliwa aumwelekeo uliokubaliwa (habari)[1].

Ingawa kuna mawasiliano yanjia moja, mawasiliano yanaweza kueleweka vyema kamamchakato wa kuhamishataarifa kati ya wahusika wawili.

Katika mawasiliano habari hupakiwa na kutumwa na kupashwa na mtu kwa anayepokea kupitia njia maalum. Kisha anayepokea hupakuaujumbe ule na kumpatia aliyetuma (ma)jibu. Aina zote za mawasiliano huhitaji mtumaji, ujumbe na mpokeaji.

Mawasiliano huhitaji kwamba wanaohusika wawe na jambo linalowaunganisha. Kuna njia zinazohusisha kusikia, kama vileunenaji,wimbo, natoni yasauti, na kuna zile zisizohusisha kusikia, kama vilemiondoko yamwili,lugha ishara, kugusa, kuwasiliana kwamacho nakuandika.

Mabadiliko katika mawasiliano

[hariri |hariri chanzo]

Kadiriwakati unavyopita,teknolojia imeendelea kukua na kuibua aina mpya za mawazo kuhusu mawasiliano.Maendeleo hayo ya teknolojia yalibadilisha jinsi mawasiliano yanavyofanyika. Watafiti wamegawanya jinsi mawasiliano yalivyobadilika katika hatua tatu.

Mabadiliko ya mwanzo: mawasiliano ya kwanza katika maandishi yalianza namichoro. Maandishi hayo yaliandikwa kwenyemawe, ambayo yalikuwa mazito mno kuhamishwa. Wakati huo, mawasiliano ya maandishi hayangeweza kubebwa, ingawa yalikuwepo.

Mabadiliko ya pili: maandishi yalianza kufanyiwa kwenyekaratasi, mavunjo,udongo,nta, n.k.Herufi zaalfabeti zilibuniwa, hivyo basi kuruhusumfanano wa lugha katika maeneo makubwa. Baada ya muda, shirika lauchapishaji laGutenberg lilianzishwa. Gutenberg alitayarishakitabu cha kwanza cha kuchapishwa akitumiamashine yake, na kitabu hicho kilikuwaBiblia. Maandiko hayo yaliweza kusafirishwa kwa watu wengineduniani ili wayaone, pia yaliweza kuhifadhiwa na kubebwa.

Mabadiliko ya tatu:taarifa sasa inaweza kuhamishwa kupitia mawimbi, naishara za kielektroniki.

Kwa hiyo mawasiliano ni njia inayotumiwa katika kutoa na kufikishamaana katikajaribio la kusababishaufahamu wa jumla.Utaratibu huu unahitaji mkusanyiko mkubwa wa ujuzi wa mawasiliano miongoni mwa na baina ya watu, kusikiliza, kutazama, kuongea, kuhoji, kuchambua na kutathmini. Ni kupitia mawasiliano kwambaushirikiano hutokea.[2]

Pia kuna vikwazo vingi vya kawaida katika mawasiliano. Viwili kati yake vikiwakupasha ujumbe kupita kiasi (mtu anapopokea ujumbe mwingi mno kwa wakati mmoja), naujumbe changamano.

Aina za mawasiliano

[hariri |hariri chanzo]

Kuna sehemu tatu kuu katika mawasiliano ya ana kwa ana kati yabinadamu: miondoko ya mwili, toni ya sauti na maneno.

Kulingana nautafiti:[3]

  • 55% yaathari hulingana na miondoko ya mwili. Kwa mfano: jinsi mtu alivyokaa, ishara zauso,mikono na macho
  • 38% hulingana na toni ya sauti, na
  • 7% hulingana na maudhui (ujumbe au maneno) yaliyotumika katika mchakato wa mawasiliano.

Ingawaasilimia yaushawishi inaweza ikabadilika kwasababu tofauti, kama vilemsikilizaji namsemaji, mawasiliano kwa jumla hulenga kutimiza lengo moja, kwa hiyo, katika baadhi ya matukio, huwa yanafanana kote duniani. Mfumo wa ishara, kama vile sauti, kiimbo auuzito wa sauti, ishara za mikono au za uso au ishara zilizoandikwa ambazo huwasilisha mawazo auhisia.

Ikiwalugha inahusu kuwasiliana kwa ishara, sauti,mlio, ishara za uso na za mikono, au ishara zilizoandikwa, je, mawasiliano yawanyama yanaweza kuchukuliwa kama lugha? Wanyama hawana lugha iliyoandikwa, lakini baadhi wanadhani mawasiliano ya wanyama yanaweza kuchukuliwa kama lugha ya namna yake.

Lugha zabinadamu zinazozungumzwa na kuandikwa zinaweza kufafanuliwa kamamfumo waishara (zinazojulikana wakati mwingine kamaleksia nasarufi) ambayo ishara hizo huzingatia. Neno "lugha" pia hutumika kurejeleasifa bainifu za lugha.

Kujifunza lugha ni jambo la kawaida katikautoto wa binadamu. Lugha nyingi hutumia mifumo yasauti auishara ambazo huwezesha mawasiliano baina ya mtu na wenzake. Kuna maelfu ya lugha, nazo huwa na sifa bainifu, ingawa nyingi ya sifa hizi huwa na upekee.

Hakuna mgawanyo dhahiri kati ya lugha nalahaja, lakinimwanaisimuWeinreich Max anatambuliwa kwa kusema kuwa "lugha ni lahaja iliyo najeshi la nchi kavu na lamajini".Lugha za kuundwa kama vileKiesperanto, lugha zatarakilishi, na maumbo mbalimbali yahisabati haziko chini ya sifa bainifu zinazohusisha lugha za binadamu.

Mawasiliano kwa ishara/kutazama

[hariri |hariri chanzo]

Mawasiliano kwa ishara ni mchakato wa kuwasiliana kwa njia ya kutuma na kupokeaujumbe usiohusisha maneno. Ujumbe kama huo unaweza kuwasilishwa kupitia ishara za uso au mikono, miondoko ya mwili au jinsi ya kukaa; ishara ya uso na kutazamana machoni, mawasiliano kwa njia ya vitu, kama vile mavazi uliyovalia, jinsi ulivyotengezanywele, au hata kwa michoro, pia kupitia jumla ya njia zilizoandikwa hapo juu, kama vile mawasiliano kupitiatabia. Mawasiliano kwa ishara huwa najukumu muhimu katikamaisha ya kilasiku ya kila mtu, iwe ni katika uhusiano wa kiajira hadi wa kimapenzi.

Mazungumzo pia huwa na vipengele vya mawasiliano kwa ishara yanayojulikana kama 'viziada-lugha' ('paralanguage'), ambayo huhusishaubora wa sauti, hisia na mitindo ya kuzungumza, ikiwa pamoja na sifa za kiarudhi kama vilemdundo,lafudhi namsisitizo.

Aidha,matini zilizoandikwa zina vipengele vya mawasiliano kwa ishara kama vilemtindo wa kuandika,mpangilio wa maneno, aumatumizi ya hisia. Neno lililounganisha maneno yaKiingereza ya hisia (emote) naikoni (icon),kihisishi (emoticon) ni ishara aumuungano wa ishara zinazotumiwa kupitisha hisia katika maandishi.

Aina nyingine za mawasiliano kama viletelegrafia huwa katikakategoria hii, ambapo ishara hupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa njia tofauti. Ishara hizo zinaweza kuwaviwakilishi vya maneno, vifaa au makadirio tu. Majaribio yameonyesha kwamba binadamu wanaweza kuwasiliana moja kwa moja kupitia njia hii[4] bila miondoko ya kimwili, toni ya sauti au maneno.

Kategoria na sifaGW Porter anagawanya mawasiliano kwa ishara katika kategoria nne:

  1. Kimwili. Hii ni aina ya mawasiliano ya binafsi. Mawasiliano hayo yanahusisha ishara za uso, toni ya sauti, kugusa, kunusa, na miondoko ya mwili.
  2. Ujumi. Hii ni aina ya mawasiliano ambayo hufanyika kupitia njia za ubunifu: kuchezaala ya muziki,dansi,uchoraji nauchongaji.
  3. Ishara. Hii ni aina ya mawasiliano, ambayo inajumuisha matumizi yabendera za ishara, milio 21 yabunduki,pembe, naving'ora.
  4. Kiashiria. Hii ni aina ya mawasiliano ambayo inatumia alama za kidini, hadhi, au za kujenga nafsi.


Sifa zisizobadilika

Umbali. Umbali mtu mmoja anaosimama kutoka kwa mtu mwingine kwa kawaida huwasilisha ujumbe fulani. Katika baadhi ya tamaduni hii ni ishara ya mvuto, na kwa wengine inaweza kuonyesha hadhi au umuhimu wa ujumbe unaopitishwa.

Namna ya kujiwasilisha. Watu wanaweza kujiwasilisha kwa njia mbalimbali: uso kwa uso,ubavu kwa ubavu, au hata wakifuatana. Kwa mfano, watu walio na ushirikiano kuna uwezekano watakaa ubavu kwa ubavu na washindani wakati mwingi hutazamana.

Namna ya kukaa. Kwa kawaida mtu anaweza kuwa amelala chini, ameketi, au amesimama. Hivi si vipengele vya mkao vinavyowasilisha ujumbe. Je, sisi tunatembea kwa kujikokota au tumesimama wima? Tunakunjamiguu au mikono yetu? Njia kama hizi za kukaa huwasilisha kiwango cha urasmi na kiwango cha mapumziko katika mawasiliano.

Mgusano wa kimwili. Kusalimiana kwa mikono, kugusana, kushikana, kukumbatiana, kusukumana, au kupiga kofimgongoni, haya yote huwasilisha ujumbe. Huwa yanaashiriaurafiki au hisia za (au ukosefu wa) mvuto.


Sifa Badilifu

Ishara za uso.Tabasamu, kukunja uso, kuinuanyusi, piga miayo, na kukenua, hivi vyote huwasilisha habari. Ishara za uso hubadilika mara kwa mara wakati wa mawasiliano na hufuatiliwa sana na mpokeaji. Kuna ushahidi kuwa maana ya ishara hizo inaweza kuwa sawa katika tamaduni mbalimbali.

Ishara. Mojawapo ya ishara zinazotumiwa, lakini zisizoeleweka, ni vidokezo katika mwondoko wa mkono. Watu wengi hutumia mara kwa mara miondoko ya mkono wanapoongea. Wakati baadhi ya ishara (mfano, kukunjangumi) zina maana bia, nyingi za ishara huwa kila mtu anajifunza kibinafsi na zina upekee.

Kutazama. Kipengele kikubwa cha mawasiliano ya kijamii ni kutazamana macho. Kipengele hiki kinaweza kuwasilisha hisia, ashiria wakati wa kuzungumza au kuacha kuzungumza, auchuki. Marudio ya kutazamana yanaweza kuonyesha aidha shauku auuchovu.

Mawasiliano ya kutazama

[hariri |hariri chanzo]

Mawasiliano ya kutazama, kama jina linavyodokeza, ni mawasiliano kwa njia ya vielelezo. Ni kupitisha mawazo na habari katika aina ambazo zinaweza kusomwa au kutazamwa. Kimsingi yanahusishwa na vipimo vya ainambili, na yanahusisha:ishara,tipografia,uchoraji, miundo ya grafia, mchoro,rangi na rasilimali za kielektroniki. Mawasiliano hayo hutegemea tu kutazama. Ni aina ya mawasiliano ilijengwa kwenye wazo kwamba ujumbe unaoonekana ukiunganishwa namaandishi huwa na uwezo mkubwa wa kutaarifu, kuelimisha aukumshawishi mtu. Ni mawasiliano kwa kuwasilisha taarifa kupitia vielelezo.

Tathmini ya muundo mzuri wa kutazamwa hujikita kwenye kupima ufahamu na watazamaji, wala si ujumi au upendeleo wa kisanii. Hakuna kanuni bia zauzuri naubaya. Kuna njia mbalimbali za kuwasilisha taarifa kwa kutazama, kama vile kutumia ishara, miondoko ya mwili,video naTV. Hapa, lengo liko kwenye kuwasilishamatini,picha, michoro na kadhalika, zikiunganishwa kwenye maonyesho ya tarakilishi. Dhana wasilisho la kutazama hutumiwa kurejelea uwasilishaji halisi wa taarifa. Utafiti wa hivi karibuni katika sehemu hii umelenga miundo yatovuti na matumizi yagrafiti.Waundaji wa grafiti hutumia mbinu za mawasiliano ya kutazama katika kazi yao.

Aina nyingine za mawasiliano

[hariri |hariri chanzo]

Aina nyingine za mawasiliano maalumu ni kama vile:

Mawasiliano ya mdomo

[hariri |hariri chanzo]

Mawasiliano ya mdomo ni mchakato ambapo habari hupitishwa kutoka kwa msemaji hadi kwa msikilizaji kupitia mdomo, lakini vielelezo vinaweza kutumiwa kusaidia katika mchakato huu. Msikilizaji anaweza kuwa mtu mmoja, kikundi au hata hadhira. Kuna aina chache za mawasiliano ya mdomo: majadiliano, hotuba, mawasilisho, n.k. Hata hivyo, mara nyingi wakati unawasiliana ana kwa anamiondoko yamwili na toni ya sauti yako huwa na athari kubwa kuliko maneno halisi unayoyasema. Kulingana na utafiti wa hapo juu unaweza kuona kwamba maudhui au neno unalolitumia silo litakaloamua sehemu ya mawasiliano mazuri. "Jinsi unavyowasilisha ujumbe" huwa na athari kubwa kwa msikilizaji. Ni lazima unase umakini wa hadhira na uhusiane nao. Kwa mfano, watu wawili wanaosema kichekesho, mmoja wao anaweza kuifanya hadhira kuangua kicheko kutokana na miondoko mizuri ya kimwili na toni ya sauti. Hata hivyo, mtu wa pili anayewasilisha kichekesho kile kwa maneno yale yale anaweza kuifanya hadhira itazamane.

Katika mawasiliano ya mdomo, inawezekana kutumia vielelezo ili kukusaidia kuwasilisha habari kwa usahihi zaidi. Mara nyingi, tunaweza kutumia'PowerPoint' katika mawasilisho yanayohusiana na hotuba zetu ili kuwezesha au kuboresha mchakato wa mawasiliano. Ingawa, hatuwezi kuwasiliana kwa kutumia vielelezo tu kwa sababu sisi hatutakuwa tukizungumza kuhusu mawasiliano ya mdomo tena.

Maumbo ya mawasiliano

[hariri |hariri chanzo]
Mipango mikuu ya Mawasiliano
Mipango ya kodi za mawasiliano

Mawasiliano kwa kawaida hufafanuliwa kwa kuzingatia mitazamo michache mikuu: Ujumbe (mambo ya aina gani yanayosemwa), chanzo / mtumaji / Msemaji /Mfumbaji (ambaye anatuma), aina (ujumbe ni wa aina gani), njia (unatumwa kupitia njia gani), unapokwenda / mpokeaji / lengo /mpokeaji (anayepokea ujumbe), na lengo au kipengele cha kipragramatiki. Kati ya vikundi, mawasiliano yanahusisha vitendo vinavyotunukia maarifa na tajriba, kupatia mawaidha na amri, na kuuliza maswali. Matendo haya yanaweza kuchukua sura nyingi, katika mojawapo ya njia mbalimbali za mawasiliano. Sura hizi hutegemea uwezo wa kikundi kinachowasiliana. Pamoja, maudhui na sura za mawasiliano kukamilishaujumbe unaotumwa mahali. Mpokeaji anayelengwa anaweza kuwa msemaji mwenyewe,mtu mwingine au kiumbe kingine, kikundi kingine (kama vile shirika au kikundi cha viumbe).

Mawasiliano yanaweza kuonekana kama mchakato wakusambaza habari unaoongozwa na viwango vitatu vya sheria zaelimu ishara:

  1. Kiwango cha kisintaksia (sifa rasmi za ishara na viashiria),
  2. Kiwango cha kipragmatiki (kinahusika na mahusiano kati ya ishara / maneno na watumiaji wake) na
  3. Kiwango cha kisemantiki (utafiti wa uhusiano kati ya ishara na viashiria na yale vinayowasilisha).

Kwa hiyo, mawasiliano nimwingiliano wa kijamii ambapo angalau vitu au watu wawili wanaotagusana hutumia seti moja ya ishara na seti moja ya kanuni zakielimu ishara. Sheria hizi zinazozingatiwa wakati mwingine huwa zinapuuzamawasiliano ambayo hutokea bila kupangiwa, yaliwemomawasiliano ya mtu na nafsi yake kupitia kwashajara au mazungumzo-nafsi, yote ambayo ni matukio ya sekondari yaliyofuatia kujifunza lugha katika maingiliano ya kijamii.

Katika mfano rahisi, habari au maudhui (mfano ujumbe katikalugha asilia) hutumwa katika njia fulani (kamalugha ya mazungumzo) kutoka kwa mtumaji / msemaji /mfumbaji kwa mahali maalum / mpokeaji /mfumbuaji. Katika njia changamano zaidi, msemaji na mpokeaji huwa wameunganishwa kwa wakati mmoja. Mfano mmoja wa mawasiliano ni kamatendo usemi. Namna ya kutafsiri ujumbe ya msemaji inaweza kuwa tofauti na ya msikilizaji kulingana na desturi na tamaduni za eneo walilomo, au jinsia; mambo ambayo yanaweza kuathiri ujumbe uliokusudiwa. Uwepo wakelele za mawasiliano katika njia inayotumiwa (ikiwa ni hewa, katika kesi hii), mapokezi na ufumbuaji wa ujumbe unaweza kuathiriwa, hivyo basi tendo usemi linaweza kutofikia matokeo yaliyotarajiwa. Tatizo moja la mfano huu wa kupakia-kutuma-kupokea-kupakua ni kwamba mchakato wa kupakia na kupakua huashiria kwamba mtumaji na mpokeaji, kila mmoja ana kitu kinachofanya kazi kamakitabu cha kodi , na kwamba vitabu hivi viwili vya kodi vinafanana kwa kiasi ikiwa si kabisa. Ingawa kitu kama vitabu vya kodi kimetajwa na mfano huu, havijawakilishwa kwenye sehemu yoyote ya mfano huu, jambo ambalo linaibua matatizo mengi ya kuelewa.

Nadharia zaurekebishaji-pamoja huelezea mawasiliano kama mchakato wa ubunifu na unaobadilika badilika, unaoendelea wala si kubadilishana tu kwa habari. Mwanataaluma wa vyombo vya habari kutoka KanadaInnis Harold alikuwa na nadharia kwamba watu hutumia njia mbalimbali kuwasiliana na njia watakayochagua kutumia itawapa uwezekano tofauti wa kuumba na kudumisha jamii (Wark, McKenzie 1997). Mfano wake maarufu wa kufafanua haya ni kutumiaMisri ya kale na kuangalia vile wao walijijenga wenyewe nje ya vyombo vya habari kwa aina tofauti za mawe na mafunjo. Mafunjo ndiyo aliyoyaita 'Kufunga Nafasi (Space Binding)'. Kufunga huku kuliwezesha kupitishwa kwa maandishi kutoka sehemu moja hadi nyingine na kuwezesha kufanyika kwa kampeni za kijeshi za mbali na utawala wa kikoloni. Mengine ni jiwe na 'Kufunga Wakati (Time Binding)', kupitia ujenzi wa mahekalu na piramidi, wanaweza kuendeleza mamlaka yao kizazi hadi kizazi, kwa kupitia njia hii ya kupitisha habari, wanaweza kubadilika na kuumba ya mawasiliano katika jamii yao (Wark, McKenzie 1997).

Bila mawasiliano ya watu

[hariri |hariri chanzo]

Mawasiliano katika mingi ya mitazamo yake hayajajifungia tu kwabinadamu, au hata kwasokwe. Kilamabadilishano ya habari kati viumbe vilivyo hai - yaani kubalishana kwaishara kunakohusiha mtumaji na mpokeaji walio hai - kunaweza kuchukuliwa kama njia ya mawasiliano. Kwa hivyo, kuna uwanja mpana wamawasiliano ya wanyama, ambayo yanahusisha mengi ya masuala katikaethnolojia. Pia wanyama waasili kama mwamba tumbawe wanaweza kuwasiliana.[5] Katika ngazi ya kimsingi zaidi, kunakupatiana ishara kati ya seli, mawasiliano ya seli, na mawasiliano ya kemikali kati ya viumbe asili kamabakteria,[6] na miongoni mwamimea nahimaya za kuvu. Michakato hii yote ya mawasiliano huhusisha mitagusani inayoshirikisha ishara zilizo na ratibu bainifu mbalimbali.

Mawasiliano ya wanyama nitabia yoyote kwa upande wa mnyama mmoja iliyo na athari ya sasa au baadaye kwenye tabia ya mnyama mwingine. Bila shaka, mawasiliano ya binadamu yanaweza kujumlishwa kama mawasiliano ya wanyama yaliyoendelezwa. Utafiti wa mawasiliano ya wanyama, uitwaozoosemiotiki (zoosemiotics), tofauti naanthroposemiotiki (anthroposemiotics, utafiti wa mawasiliano ya binadamu) umechangia pakubwa katika ukuzaji waetholojia,biolojia-jamii na masomo yauwezo wa mnyama wa kutambua.

Jambo hili ni dhahiri kwani binadamu huwa wanaweza kuwasiliana na wanyama, hasapomboo na wanyama wengine ambao hutumika katikasarakasi. Hata hivyo, hawa wanyama hulazimika kujifunza njia za kipekee za mawasiliano. Mawasiliano ya wanyama, na haswa kuelewa ulimwengu wa mnyama kwa ujumla, nitaaluma inayokua kwa kasi, na hata katikakarne ya 21 kufikia sasa, uelewa mwingi wa hapo awali kuhusiana na nyanja mbalimbali kama vile matumizi ya kiishara yajina,hisia za wanyama,utamaduni,kujifunza kwa wanyama na hatatabia za kingono, zilizofikiriwa kwa muda mrefu kuwa zimeeleweka vizuri, zimebadilika pakubwa.

Mimea na kuvu

[hariri |hariri chanzo]

Miongoni mwamimea, mawasiliano huonekana ndani ya mmea wenyewe, yaani, ndani ya na kati yaseli za mimea, kati ya mimea yaspishi moja au spishi zinazohusiana, na kati ya mimea na viumbe visivyo hai, hasa katika sehemu ya mizizi.Mizizi ya mimea huwasiliana nabakteria za rhizobia, nakuvu pamoja nawadudu walio kwenyeardhi. Mitagusano hii sambamba inayohusisha ishara na inayoongozwa na kanuni za kisintaksia, kipragmatiki na kisemantiki hutokea kwa sababu ya "mfumo wa neva" wa mimea uliogatuka.

Maana asilia ya neno nyuro katikaKigiriki ni "nyuzinyuzi za mboga" na kama utafiti wa hivi karibuni unavyoonyesha, mengi ya mawasiliano ya ndani ya mmea hufanana na ya nyuro.[7] Mimea pia kuwasiliana kupitia kwamivuke katika kisa cha tabia za wakati wa mashambulizi na wanyama wala mimea, ili kuonya mimea jirani. Sambamba na hayo, mimea hiyo hutoa mivuke ya kuvivutiavimelea ambavyo huwashambulia wale wanyama. Katikahali ya dhiki mimea inaweza kubadilishakodi ya kinasaba iliyorithi kutoka kwa wazazi wao na kurudi kwa ile ya mababu zao.[8]

Kuvu huwasiliana ili kuratibu na kupanga ukuaji wao wenyewe na maendeleo yao kama vile malezi yaseli zake nasehemu za kuota. Aidha, kuvu huwasiliana spishi zinazofanana au kuhusiana pamoja na spishi zisizokuvu katika mitagusano ya kimfaano, haswa na bakteria, 'unicellular eukaryotes' , mimea na wadudu. Kemikali za kisemiotiki zinazotumiwa huwa za asili ya kibayotiki na hufanya kuvu kuonyesha athari maalum, ambapo, katika tofauti wakati hata huo kemikali za molekuli huwa si sehemu ya ujumbe wa biotiki unaosababisha msisimko wa viumbe-kuvu. Ina maana kuwa, kuvu zinaweza kutambua tofauti katika molekuli ambazo ni sehemu ya ujumbe wa kibayotiki au kutokuwepo kwa sifa hizi. Hadi sasa kunamolekuli tano tofauti na za msingi zinazojulikana ambazo huratibisha ruwaza tofauti za kitabia kama vile 'nyuzi za hisia', kuzaana, ukuaji, usababishaji wa magonjwa. Uratibu wa tabia na uzalishaji wa vitu kama hivi unaweza tu kufikiwa kupitia michakato fasili: ya kibinafsi au isiyo ya kibinafsi, kiashiria cha kibiotiki, ujumbe wa kibiotiki kutoka kwa spishi zinazofanana, zinazohusiana au zisizohusiana, au hata "kelele", yaani, molekuli zinazofanana lakini hazina ujumbe wa kibiotiki.[9]

Mawasiliano kama taaluma ya kiakademia

[hariri |hariri chanzo]

Mawasiliano kama taaluma ya kiakademia, ambayo wakati mwingine huitwa "komunikolojia,"[10] inahusiana na njia zote tunazozitumia kuwasiliana, hivyo basi inahusisha sehemu kubwa ya utafiti na maarifa. Taaluma ya mawasiliano inahusisha mawasiliano ya kimaongezi na yasiyo ya kimaongezi. Mkusanyiko wa maarifa kuhusu mawasiliano umewakilishwa na kufafanuliwa katika vitabu, machapisho ya kielektroniki, na majarida ya kiakademia. Katika majarida, ripoti za kitafiti ndizo matokeo ya tafiti ambazo ni msingi wa uelewa, unaoendelea kupanuka, wa jinsi sisi wote tunavyowasiliana.

Mawasiliano hufanyika katika ngazi tofauti (hata kwa tendo moja), katika njia mbalimbali, na kwa viumbe wengi, na vilevile kwa mashine fulani. Baadhi ya taaluma za utafiti , ikiwa siyo zote, hutenga sehemu ya mafunzo yake kwa mawasiliano, hivyo basi wakati wa kuzungumza kuhusu mawasiliano, ni muhimu sana kuwa na uhakika kuhusu nyanja ya mawasiliano inayozungumziwa. Ufafanuzi wa mawasiliano hutofautiana sana, baadhi yake ukitambua kwamba wanyama wanaweza kuwasiliana na wenzao na binadamu pia, na baadhi ni finyu zaidi, ukihusisha binadamu katika mitagusano ya kibinadamu iliyo na maana.

Umuhimu wa mawasiliano

[hariri |hariri chanzo]

Hakuna linaloweza kufanikiwa pasipo mawasiliano. Mawasiliano ni kati ya nafsi na nafsi – hivyo nafsi zisipokuwa na mawasiliano ina maana miili inayobeba nafsi hizo haiwezi kushirikiana kwa lolote. Kitu kimoja ambacho ni kikwazo cha mawasiliano ni woga. Ndio unaokufanya usiwasiliane na fulani, usiwe na ushirika naye. Woga huo ndio unaosababisha usipate usaidizi toka popote pale.

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Schwartz, Gary E.; Simon, William L.; Carmona, Richard (2008).The Energy Healing Experiments. Simon & Schuster. uk. 129.ISBN 0743292399.All communication is a process of exchanging energy and exchanging information.{{cite book}}:Check|isbn= value: checksum (help)
  2. "communication".office of superintendent of Public instruction. Washington. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2009-11-19. Iliwekwa mnamo14 Machi 2008.{{cite web}}:Unknown parameter|dateformat= ignored (help)
  3. Mehrabian na Ferris (1967). "Inference of Attitude from Nonverbal Communication in Two Channels". Katika:The Journal of Counselling Psychology Vol.31, 1967, pp.248-52.
  4. Warwick, K, Gasson, M, Hutt, B, Goodhew, I,Kyberd, P, Schulzrinne, H na Wu, X: "Thought Communication and Control: A First Step using Radiotelegraphy",IEE Proceeedings on Communication, 151 (3), pp.185-189, 2004
  5. Witzany G, Madl P. (2009). Biocommunication of corals. International Journal of Integrative Biology 5 (3): 152-163.
  6. Witzany G (2008). Bio-Communication of Bacteria and their Evolutionary Roots in Natural Genome Editing Competences of Viruses. Open Evolution Journal 2: 44-54.
  7. Baluska, F.; Marcuso, Stefano; Volkmann, Dieter (2006).Communication in plants: neuronal aspects of plant life. Taylor & Francis US. uk. 19.ISBN 3540284758....the emergence of plant neurobiology as the most recent area of plant sciences.{{cite book}}:Check|isbn= value: checksum (help)
  8. Witzany, G. (2006 Plant Communication from Biosemiotic Perspective. Plant Signaling na Behavior 1 (4): 169-178.
  9. Witzany, G. (2007 Applied Biosemiotics: Fungal meddelande. Katika: Witzany, G. (Ed). Biosemiotics in Transdisciplinary Contexts. Helsingfors, Umweb, uk. 295-301.
  10. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2009-09-23. Iliwekwa mnamo2009-11-23.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Mawasiliano&oldid=1307781"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp