Ingawaufafanuzi fasaha haujapatikana, kutokana na tofauti kati yawataalamu wa mauaji ya kimbari, ufafanuzi wa kisheria hupatikana katikaMkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari (unaofupishwa "CPPCG" katikalugha yaKiingereza) waUmoja wa Mataifa wamwaka wa1948.Ibara ya 2 yamkataba huo inayafafanua mauaji ya kimbari kama "Tendo lolote kati ya yale yafuatayo linalofanyika kwa nia ya kuharibu, kikamilifu au katika sehemu, kikundi cha kitaifa, kikabila, kirangi au cha kidini, kama vile: mauaji ya watu wa kikundi hicho; kusababishaathari kubwa upande wamwili au waakili kwa watu wa kikundi hicho; kutwika kwa makusudi juu ya kundi hali za maisha, zinazonuiwa kuletauharibifu wa mwili mzima au sehemu ya mwili; kuchukua hatua zinazonuiwa kuzuiawanawake wasijifungue katika kikundi hicho; [na] kuhamishawatoto wa kikundi hicho hadi kikundi kingine kwa lazima.[1]
Utangulizi wa CPPCG unasema kuwa matukio ya mauaji ya kimbari yamefanyika tangujadi,[1] lakini haikuwa hadiRaphael Lemkin alipoyatunga maneno hayo na wahusika waMauaji ya kimbari ya Wayahudi waliposhtakiwa katikakesi za Nuremberg; ndipo Umoja wa Mataifa ulipokubaliana na CPPCG ambayo iliufafanuauhalifu wa mauaji ya kimbari ya watu chini yasheria ya kimataifa.Kulikuwa na zaidi ya miaka 40 kati ya CPPCG kukamilika na mashtaka ya kwanza chini ya masharti ya mkataba kufanywa.
Tangu CPPCG ianze kutumika mnamo Januari1951, takribannchi 80 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepitisha sheria ambayo inayajumuisha masharti ya CPPCG ndani ya sheria za nchi yao, na baadhi ya wahusika wa mauaji ya kimbari wamepatikana nahatia chini ya sheria za namna hizo, kama vileNikola Jorgic, ambaye alipatikana na hatia ya mauaji ya kimbari katikaBosnia na mahakama yaUjerumani (Jorgic dhidi ya Ujerumani).
Wakosoaji wa CPPCG wameangazia uwepo wa ufafanuzi finyu wa makundi yanayolindwa chini ya mkataba, hasa ukosefu waulinzi kwa makundi ya kisiasa, jambo ambalo linajulikana kama Mauaji ya watu wa kundi fulani la kisiasa (Mauaji hayo yamejumuishwa na mauaji ya kimbari katika baadhi ya nchi).[3]
Tatizo moja ni kwamba hadi mkusanyiko wakesi za sheria kutoka mashtaka upatikane, ufafanuzi fasaha wa kile ambacho mkataba ulimaanisha haukuwa umepimwamahakamani, kwa mfano, ni nini hasa maana ya maneno "katika sehemu"? Kadiri wahalifu wanavyozidi kufikishwa mahakamani chini ya mfumo wa mahakama ya kimataifa na kesi za mahakama za nchi, ndivyomkusanyo wahoja za kisheria natafsiri za kisheria unavyosaidia kuyashughulikia masuala haya.
Wasomi wa mauaji ya kimbari, kama vileGregory Stanton, wamedadisi kwamba masharti na vitendo ambavyo mara nyingi hutokea kabla, wakati na baada ya mauaji ya kimbari - kama vile vikundi vya wahasiriwa kunyimwautu,upangaji kabambe katika makundi yanayofanya mauaji ya kimbari, na kukana kwa mauaji ya kimbari na wahusika wake - yanaweza kutambuliwa na hatua kuchukuliwa kukomesha mauaji ya kimbari kabla ya kutokea. Wakosoaji wambinu hii, kama vileDirk Moses, wamedai kwamba haya hayafafani na mambo jinsi yalivyo na kwamba, kwa mfano,"Michafuko ya Darfur itakamilika kwa wakati utakaozifaa nguvu kubwa ambazo zina mambo yatakayozifaidi katika kanda hiyo".
Maneno "mauaji ya kimbari" yalianzishwa na Lemkin Raphael (mwanachuoni wa kisheria mwenye asili yaKiyahudi aliyezaliwaPolandi1900-1959), mnamo mwaka wa1944, kwanza kutokaKilatini "gens, gentis," kumaanisha "kuzaliwa, kabila, ukoo, aina" au mzizi waKigiriki "génos" (γένος) (maana sawa); pili kutoka Kilatini -"cidium" (kukata, na kuua) kupitiaKifaransa -"cide".[4][5]
Wazo la Lemkin la mauaji ya kimbari kamakosa dhidi ya sheria za kimataifa lilikubalika najamii ya kimataifa na lilikuwa mojawapo kati yasheria msingi zaMashitaka ya Nuremberg (mashitaka ya viongozi 24 wa Kinazi) iliyotilia mkazo katika sehemu ya 3 kuwa watuhumiwa "walifanya mauaji ya kimbari kwa makusudi na kwa utaratibu - yaani, kuviaangamiza vikundi vya rangi na vya kitaifa ..."[8])
Lemkin aliiwasilisharasimu yaazimio la Mkataba wa mauaji ya kimbari kwa nchi kadhaa katikajitihada za kuzishawishi zilidhamini azimio hilo. Kupitia msaada wa Marekani, azimio liliwekwa mbele ya Mkuu wa Bunge lizingatiwe. Akiyafafanua mauaji ya kimbari mwaka wa1943, Lemkin aliandika:
Kiujumla, mauaji ya kimbari si lazima yamaanishe uangamizaji wa taifa mara moja, isipokuwa yanapofuatwa na mauaji ya halaiki ya watu wote wa taifa hilo. Inanuiwa kuashiria mpango wa hatua mbalimbali zenye nia ya kuangamiza misingi muhimu ya maisha ya vikundi vya kimataifa, zikiwa na nia ya kuviangamiza vikundi hivi vyenyewe. Lengo la mpango kama huo utakuwa kubomoa miundo-msingi ya kisiasi na kijamii, ya tamaduni, lugha, hisia za kitaifa, dini na kuwepo kwa vikundi vya kitaifa kiuchumi, na uharibifu wa usalama wa kibinafsi, uhuru, afya, heshima na hata maisha ya watu binafsi katika vikundi hivyo.[9]
Kufuatia mauaji ya kimbari ya Wayahudi, Lemkin alifanikiwa katika kampeni za kukubalika ulimwenguni kote kwasheria za kimataifa zilizoyafafanua mauaji ya kimbari na kuyapinga. Mnamo mwaka wa 1946, kikao cha kwanza cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa]] kilipitisha azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Sheria 96 "lililosisitiza" kwamba mauaji ya kimbari yalikuwa hatia chini ya sheria ya kimataifa, lakini ambalo halikutoa ufafanuzi wa kisheria wa uhalifu huo. Mnamo mwaka 1948, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliukubali "Mkataba wa Kuzuia na Kuadhabu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari" ambao ulifafanua kisheria kwa mara ya kwanza mauaji ya kimbari.
"CPPCG" ilipitishwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 9 Desemba 1948 na ikawa rasmi mnamo 12 Januari 1951 (Sheria nambari 260 (III)). Inayo ufafanuzi unaotambulika kimataifa wa mauaji ya kimbari ambao uliingizwa kwenye sheria ya jinai ya kitaifa ya nchi nyingi, na ilikubalika na Katiba yaRoma ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, mkataba ambao ulianzishaMahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC kwa lugha ya Kiingereza). Mkataba (katika ibara ya 2) unafafanua mauaji ya kimbari:
...tendo lolote kutoka ya yale yafuatayo linalofanyika na nia ya kuharibu, kikamilifu au katika sehemu, kikundi cha kitaifa, kikabila, kirangi au kundi la kidini, kama vile
(a) mauaji ya watu wa kikundi hicho;
(b) kusababisha athari kubwa ya kimwili au kiakili kwa watu wa kikundi hicho;
(c) kuzitwika kimakusudi juu ya kundi hali za maisha, zinazonuiwa kuleta uharibifu wa mwili mzima au sehemu ya mwili;
(d) kuchukua hatua zinazonuiwa kuzuia wanawake wasijifungue) katika kikundi hicho;
(e) kuhamisha watoto wa kikundi hicho hadi kundi lingine kwa lazima.
–Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Hualifu wa Mauaji ya Kimbari, Ibara ya II
Rasimu ya kwanza ya Mkataba iliyajumuisha mauaji ya kisiasa, lakiniMuungano wa Jamhuri za Kisosholisti za Kisovyeti[10] pamoja na baadhi ya mataifa mengine yalikataa hatua dhidi ya makundi yaliyotambuliwa kuwa na maoni sawa ya kisiasa au hali ya kijamii yatambulike kama mauaji ya kimbari,[11] kwa hivyo, masharti haya hatimaye yaliondolewa katika maelewano ya kisiasa na kidiplomasia.
Mkataba ulionekana kukubalika kwa minajili ya kuwasaidia watu katika taabani na raia. Malengo yake ni kulinda kuwepo kuwa vikundi fulani vya watu na kutilia mkazo na kusisitiza zile kanuni za kimsingi za utu na maadili. Kulingana na haki zilizopo, majukumu ya kisheria ya kujiepusha na mauaji ya kimbari yanafahamika kamaerga omnes
Wakati mkataba uliporasimiwa kwa mara ya kwanza, tayari ilitarajiwa kuwa haungetumika tu kwa kwa aina ya mauaji ya kimbari ya wakati huo, bali ungetumika "kwa mbinu yoyote ambao huenda ingeundwa siku za usoni kwa madhumuni ya kuangamiza kikundi fulani".[12] Jinsi ilivyosisitizwa katika utangulizi wa Mkataba, mauaji ya kimbari yameadhiri enzi zote za kihistoria, na ni kwa kulifahamu swala hili la kusikitisha ambapo dhana hii inapewa hali yake ya kubadilika ya kihistoria.
Mkataba lazima utafsiriwe kwa nia nzuri, kulingana na maana ya kawaida ya maneno yake, katika muktadha wa maneno hayo, na kwa mujibu wa chombo na lengo lake. Isitoshe, nakala ya Mkataba inafaa itafsiriwe kwa namna itakayowezesha sababu na maana ipewe kwa kila neno. Hakuna neno au sehemu nyeti ambayo inafaa kupuuzwa au kufanywa kana kwamba imetumia maneno mengi bure, labda tu ikiwa kufanya hivi kunahitajika kutupea maana kwa maswala yatakaposomwa kikamilifu.[13]
Mauaji ya kimbari ni hatia chini ya sheria ya kimataifa bila kujali "ikiwa makosa yalitendwa katika kipindi cha amani au vita" (ratiba ya I). Kwa hivyo, muktadha ambapo jambo lilitokea haujalishi (kwa mfano, wakati wa amani, wakati wa migogoro ndani ya kitaifa, migoro ya kimataifa ya silaha au kiujumla yoyote yanayoendela) mauaji ya kimbari ni hatia ya kimataifa inayoadhibika. –
–Kamati ya Wataalamu ya Umoja wa Mataifa iliyochunguza ukiukaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu katika eneo la Yugoslavia ya zamani.[14]
Mnamo mwaka wa 2007 Mahakama ya Ulaya yaHaki za Kibinadamu (ECHR kwa lugha ya Kiingereza), ilibainisha katika uamuzi wake wa kesi yaJorgic dhidi ya Ujerumani kuwa mnamo mwaka wa 1992 wasomi wengi wa kisheria walikuwa na mtazamo finyu kwamba "nia ya kuharibu" katika CPPCG ilimaanisha uharibifu wa kimwili na kibaiolojia wa kundi lenye ulinzi na kwamba haya bado yalikuwa maoni ya wengi. Lakini ECHR pia ilibainisha kuwa wachache walikuwa na mtazamo mpana na hawakufikiri uharibifu wa kimwili na kibaiolojia ulikuwa muhimu kwani dhamira ya kuharibu kundi la kitaifa, kirangi, kidini au kikabila ilitosha kuhitimu kuwa mauaji ya kimbari.[15]
Katika hukumu iyo hiyo ECHR ilipitia uamuzi wa mahakama kadhaa ya kimataifa na ya kimanisipaa na Ilibainisha kuwa Mahakama ya Kimataifa la Jinai ya Yugoslavia ya Zamani na Mahakama ya Kimataifa ya Haki yalikuwa yamekubali kupitia ufafanuzi finyu, kwamba uharibifu wa kibaiolojia na kimwili ulikuwa muhimu kwa tendo kuhitimu kuwa mauaji ya kimbari.
ECHR pia ilibainisha kuwa wakati wa uamuzi wake, mbali na mahakama nchini Ujerumani ambayo yalikuwa na mtazamo mpana, kulikuwa na kesi chache za mauaji ya kimbari chini katika nchi zingine zilizokuwa miongoni mwasheria manisipaa za nchi zilizokuwa zimetia sahini mkataba na kwamba "Hakuna kesi zilizoripotiwa ambapo mahakama ya nchi hizo yamefafanua aina ya uharibifu wa kikundi ambao lazima mhalifu awe amekusudia ili kupatikana na hatia ya mauaji ya kimbari".[16]
Maneno "kikamilifu au katika sehemu" yamejadaliwa kwa kina na wasomi wa sheria ya kibinadamu ya kimataifa.[17]
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Yugoslavia ya Zamani yalibainisha katika kesi la "Mwendesha mashitaka dhidi ya Radislav Krstic - Chumba cha Kesi I - uamuzi- IT-98-33 (2001) ICTY8 (2 Agosti 2001)"[18] kwamba mauaji ya kimbari yalikuwa yametendeka. Katika "Mwendesha dhidi ya Radislav Krstic - Chumba cha Rufaa - Uamuzi- IT-98-33 (2004) ICTY 7 (19 Aprili 2004) "[19] aya za 8, 9, 10, na 11 zilifumbua suala la "katika sehemu" na zilipata kuwa "sehemu lazima iwe sehemu muhimu ya kundi.
Lengo la Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ni kuzuia uangamizaji wa kimakusudi wa makundi zima ya binadamu, na sehemu iliyolengwa lazima iwe muhimu kiasi cha kuadhirisha kundi zima." Mahakama ya Rufaa inapeana maelezo zaidi ya kesi zingine na maoni ya wachambuzi wa kuheshimika kuhusu Mkataba wa Mauaji ya kimbari kuelezea jinsi walivyolifikia hitimisho hili.
Waamuzi wanaendelea katika aya ya 12, “Uamuzi wa ikiwa wakati sehemu inayolengwa inatosha kukidhi mahitaji haya unabidi maswala mengi yazingatiwe. Ukubwa wa kiidadi wa sehemu ya kikundi inayolengwa ndiyo sehemu muhimu na inayofaa kuanzia, ingawa sio mwisho wa uchunguzi katika matukio yote. Idadi ya watu binafsi wanaolengwa lazima inakiliwe si tu kwa ujumla, lakini pia kwa uhusiano na ukubwa wa kijumla wa kundi zima. Bali na ukubwa wa kiidadi wa sehemu inayolengwa, umuhimu wake katika kundi unaweza kuwa wazo muhimu. Ikiwa sehemu maalum ya kikundi inaweza kuliwakilisha kundi lote kiujumla, au ni muhimu kwa uhai wake, hilo linaweza kuunga mkono wazo kuwa sehemu hiyo inahitimu kama muhimu kulingana na maana ya Ibara ya 4 [ya Katiba ya Mahakama].”[20][21]
Katika aya ya 13 ya waamuzi wanaangazia suala la wahalifu kuweza kuwafikia waathirika: “mifano ya kihistoria ya mauaji ya kimbari pia inaonyesha kwamba eneo la wahalifu, wanalojishughulisha nalo na kulidhibiti, na pia kiwango wanachoweza kufikia, yanafaa kutiliwa maanani... Dhamira ya kuharibu inayoundwa na mhalifu wa mauaji ya kimbari daima itakomeshwa na upungufu wa nafasi inayopatikana kwake. Ingawa sababu hii pekee haitaonyesha kama kundi linalolengwa ni la kutosha, inaweza - ikihusishwa pamoja na mambo mengine - kusaidia katika uchambuzi.”[19]
Baada ya nchi chache 20 zilizohitajika kuupitisha Mkataba kutia sahihi, ulifanywa kuwa sheria ya kimataifa mnamo tarehe 12 Januari 1951. Hata hivyo wakati huo, wanachama wawili pekee kati ya wanachama tano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC kwa Kiingereza) walikuwa wametia sahini mkataba:Ufaransa naJamhuri ya Uchina. HatimayeUmoja wa Kisovyeti ulitia sahini mnamo mwaka wa 1954,Uingereza mnamo mwaka wa 1970,Jamhuri ya Watu wa Uchina mnamo mwaka wa 1983 (Ikiwa imeingia badala ya Jamhuri ya Uchina yenye makao Taiwan katika UNSC mnamo mwaka wa 1971), naMarekani mnamo mwaka wa 1988. Kukawia huku kurefu kuunga mkono Mkataba wa mauaji ya Kimbari na mataifa yenye nguvu duniani kulisababisha Mkataba kutotumika kwa zaidi ya miongo minne. Ni tu katika miaka ya 1990 ndipo sheria ya kimataifa ya uhalifu wa mauaji ya kimbari ilipoanza kutekelezwa.
[[Sheria ya Baraza la Usalama laUmoja wa Mataifa nambari 1674, iliyopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mnamo tarehe 28 Aprili 2006, "inatilia mkazo masharti ya aya za 138 na 139 za Nyaraka ya Matokeo ya Mkutano wa Dunia wa mwaka 2005 kuhusu wajibu wa kuwalinda wakazi kutoka mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita, utakaso wa kikabila na uhalifu dhidi ya ubinadamu".[22]azimio linapea Baraza jukumu la kuchukua hatua kuwalinda raia wakati wa vita.
Tangu Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari (CPPCG kwa Kiingereza) ulipofanywa kuwa sheria mnamo Januari mwaka wa 1951 zipatazo nchi 80 ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepitisha sheria ambayo inajumuisha masharti ya CPPCG katikasheria zao za kimanispaa.
Ukosoaji wa CPPCG na fafanuzi mbalimbali za mauaji ya kimbari
William Schabas amependekeza kuwa kuwepo kwa mwili wa kudumu kama ilivyopendekezwa katika Ripoti ya Whitaker kufuatilia utekelezaji wa Mkataba wa mauaji ya kimbari, na kuhitaji nchi kutoa ripoti kuhusu jinsi zinavyoufuata mkataba (kama zile zilizojumuishwa ndani ya Itifaki Isiyo ya Lazima ya Mkataba dhidi ya Mateso ya Umoja wa Mataifa) , kutaufanya mkataba uwe na ufanisi zaidi.[23]
Wakiandika mnamo mwaka wa 1998 Kurt Jonassohn na Karin Bjørnson walisema kuwa CPPCG ilikuwa chombo cha kisheria kilichotokana na maafikiano ya kidiplomasia. Kwa hivyo, maneno ya mkataba hayafai kuwa ufafanuzi ufaao kutumika kama zana ya utafiti, na ingawa inatumika kwa kusudi hili, kwani ina hadhi ya kisheria ya kimataifa ambayo nyingine hazina, ufanunuzi mbalimbali pia umedadisiwa. Jonassohn na Bjørnson wanazidi kusema kwamba hakuna fafanuzi mbadala kati ya hizi ambazo zilizopata msaada mwingi kwa sababu mbalimbali.[24]
Jonassohn na Bjørnson wanadadisi kuwa sababu kuu ya ukosefu wa ufafanuzi wa kiujumla wa mauaji ya kimbari kuibuka ni kuwa wasomi wameurekebisha mtazamo wao ili kuvisisitiza vipindi tofauti na wamepata kuwa ni afadhali kutumia fafanuzi zinazotofautiana kidogo ili kuwasaidia kuyatafsiri matukio. Kwa mfano Frank Chalk na Kurt Jonassohn waliichunguza historia yote ya binadamu, ilhali Leo Kuper na R.J. Rummel katika maandishi yao ya hivi karibuni waliupea uzito karne ya 20, na Helen Fein, Barbara Harff na Ted Gurr wameyaangalia matukio yaliyofuata Vita Vya Pili Vya Duniani. Jonassohn na Bjørnson wameyakosoa baadhi ya matokeo ya utafiti huu wakisema kuwa ni mapana sana na wanahitimisha kwamba nidhamu ya kielimu ya masomo ya mauaji ya kimbari ni changa mno kuwa na msingi ambapo dhana ya kitaaluma itaweza kujengwa.[24]
Kuondolewa kwa makundi ya kijamii na kisiasa kama malengo ya mauaji ya kimbari katika ufafanuzi wa kisheria wa CPPCG umekosolewa na baadhi ya wanahistoria na wataalamu wa kijamii, kwa mfano M. Hassan Kakar katika kitabu chake "Uvamizi wa Kisovyeti na Jibu la Kiafghani, 1979-1982"[25] anadokeza kuwa ufafanuzi wa kimataifa wa mauaji ya kimbari una vikwazo vingi sana,[26] na kwamba ni lazima ujumuishe makundi ya kisiasa au kikundi chochote kinachofafanuliwa hivyo na mhalifu na anawanukuu Chalk na Jonassohn: "Mauaji ya kimbari ni mauaji ya aina ya kihalaiki kwa upande mmoja ambapo nchi au wenye mamlaka wanakusudia kuangamiza kundi, kwani kundi na uanachama katika kundi hilo linafafanuliwa na mhalifu."[27]
Ingawa kuna ufafanuzi mbalimbali wa hayo maneno, Adam Jones anasema kwamba wasomi wengi wa mauaji ya kimbari hufikiria kuwa "nia ya kuharibu" ni sharti iwe kwa kitendo chochote kuitwa mauaji ya kimbari, na kwamba kuna makubaliano yanayozidi kuongezeka kuhusu kujumuisha swala la uharibifu wa kimwili.[28]Barbara Harff na Ted Gurr waliyafafanua mauaji ya kimbari kama "ukuzaji na utekelezaji wa sera na nchi au mawakala wake ambazo husababisha vifo vya sehemu muhimu ya kundi ... [wakati] makundi yanayoteswa yanafafanuliwa kimsingi kupitia sifa za jumuiya zao, yaani, kabila, dini au utaifa."[29] Harff na Gurr pia wanatofautisha mauaji ya kimbari na mauaji ya kundi la kisiasa kupitia sifa ambazo wanachama wa kundi hilo wanajitambulisha kwa serikali. Katika mauaji ya kimbari, makundi yanayodhulumiwa yanafafanuliwa kimsingi kupitia sifa za jumuiya zao, yaani, kabila, dini au utaifa. Katika mauaji ya kisiasa makundi ya wahasiriwa yanafafanuliwa kimsingi kupitia nafasi ya kihierarkia au upinzani wa kisiasa dhidi ya utawala au vikundi muhimu.[30][31]
Daniel D. Polsby na Don B. Kates, Jr. wanasema ya kuwa "... sisi tunafuata mbinu ya Harff inayotofautisha kati ya mauaji ya kimbari na mauaji ya wapinzani wa kisiasa ambayo anaelezea kuwa 'hasira ya halaiki isiyokawia kwa muda mrefu, ambayo, ingawa mara nyingi inaruhusiwa na wenye mamlaka, ni nadra kuendelea. ' Kama ghasia itaendelea kwa muda fulani, basi, anasema Harff, tofauti kati ya kuruhusu na kushiriki itaisha. "[32]
Kulingana na R.J. Rummel, mauaji ya kimbari yana maana tatu tofauti. Maana yake ya kawaida ni mauaji ya watu na serikali kutokana nao kuwa wanachama wa kundi fulani la kitaifa, kikabila, kirangi, au kidini. Maana ya kisheria ya mauaji ya kimbari inahusu mkataba wa kimataifa,Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari. Hii pia ni pamoja na kutoua ambao mwishowe kunaangamiza, kama vile kuzuia kuzaliwa au kuhamisha watoto kwenda kundi lingine kwa lazima. Maana ya kiujumla ya mauaji ya kimbari ni sawa na maana ya kawaida lakini pia inajumuisha mauaji ya kiserikali ya wapinzani wa kisiasa au vinginevyo mauaji ya kimakusudi. Ni kwa minajili ya kuepuka utata kuhusu maana inayolengwa ndio Rummel akayatunga maneno mauaji ya idadi ya wakazi kwa ile maana ya tatu.[33]
Ukosoaji mkuu wa jinsi jumuiya ya kimataifa ilivyokabiliana na Mauaji ya kimbari ya Rwanda ni kuwa ilikuwa tendaji, si makini. Jamii ya kimataifa imeanzisha mfumo kwa ajili ya kuendesha mashtaka dhidi ya wahalifu wa mauaji ya kimbari lakini bado haijaunda nia au mifumo ya kukomesha mauaji ya kimbari wakati yanapotokea. Wakosoaji wanaashiriamgogoro wa Darfur na kupendekeza kwamba ikiwa yeyote atapatikana na hatia ya mauaji ya kimbari baada ya mgogoro huo iwe kupitia mashtaka mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai au Mahakama yakidharura ya Jinai, hili litauthibitisha mtazamo huu.Kigezo:Marejeo yanahitajika
Nchi zote zilizotia saini mkataba wa CPPCG zinafaa kuzuia na kuadhibu vitendo vya mauaji ya kimbari, katika wakati wa amani na vita, ingawa vizuizi kadhaa hufanya hili liwe jambo gumu kutekeleza. Hasa, baadhi ya watia sahini &mdash yaani,Bahrain,Bangladesh,Uhindi,Malaysia,Ufilipino,Singapore,Marekani,Vietnam,Yemen, naYugoslavia &mdash zilitia saini na maafikiano kwamba hakuna madai ya mauaji ya kimbari yangeoweza kuletwa dhidi yao katikaMahakama ya Kimataifa ya Haki bila idhini yao.[34]
Licha ya maandamano rasmi ya watia sahini wengine (hasaKupro naNorway) kuhusu maadili na uaminifu wa kisheria wa kinga wanayojipa, kinga hiyo dhidi ya mashitaka imetumika mara kadhaa, kama wakati Marekani ilipokataa kuruhusu madai ya mauaji ya kimbari kufanywa dhidi yao naYugoslavia kufuatia vita vya 1999 vyaKosovo.[35]
Kawaida imekubalika kwamba, angalau tanguVita Vikuu Vya Pili vya Dunia, mauaji ya kimbari yamekuwa haramu chini yasheria ya kimila ya kimataifa kama kinga na vilevile chini yasheria ya kawaida ya kimataifa. Kwa ujumla, ni vigumu kuyaanzisha mashtaka dhidi ya matendo ya mauaji ya kimbari, kwa sababu mfululizo wa uwajibikaji lazima ufahamike. Mahakama ya Kimataifa ya Jinai hutumika haswa kwa sababu nchi husika haziwezi kuyashitaki au hazina nia ya kuushitaka uhalifu wenye ukubwa wa kiasi hiki zenyewe.
Kwa sababu kukubalika kwasheria za kimataifa ulimwenguni kote, zinazoyafafanua na kuyapinga mauaji ya kimbari kulitimika mnamo mwaka wa 1948, pamoja na kupitishwa kwaMkataba wa Kuzuia na Kuadhibu kwa Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari (CPPCG), wale wahalifu ambao walishitakiwa baada ya vita katika mahakama ya kimataifa, kwa ajili ya kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Wayahudi walipatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na hatia zingine maalum kama vile mauaji. Hata hivyo mauaji ya kimbari ya Wayahudi yanatambuliwa duniani kote kuwa mauaji ya kimbari, na maneno ambayo yalikuwa yameundwa mwaka wa awali na Raphael Lemkin,[36] yalionekana katika mashitaka ya viongozi 24 wa Kinaksi, shitaka la 3, lilisema kuwa watuhumiwa wote walikuwa "wameua kimakusudi na kwa utaratibu - yaani, uangamizaji wa vikundi vya kirangi na vya kitaifa ... "[37]
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR kwa lugha ya Kiingereza) ni mahakama chini ya mwavuli waUmoja wa Mataifa kwa ajili ya kushitaki makosa yaliyotokea nchiniRwanda wakati wa mauaji ya kimbari yaliyotokea pale katika kipindi cha Aprili 1994, kilichoanza tarehe 6 Aprili. ICTR iliundwa tarehe 8 Novemba 1994 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuhukumu wale watu waliofanya vitendo vya mauaji ya kimbari na ukiukaji mwingine mbaya wa sheria za kimataifa nchini Rwanda, au kwa raia wa Rwanda katika majimbo jirani , kati ya tarehe 1 Januari na tarehe 31 Desemba 1994.
Kufikia wakati wa sasa, ICTR imekamilisha kesi kumi na tisa na kuwahukumu washitakiwa ishirini na watano. Kesi za watu wengine ishirini na watano bado zinaendelea. Kumi na watisa wanasubiri kesi zao kizuizini. Kumi bado hawajakamatwa. Kesi ya kwanza, ya Jean-Paul Akayesu, ilianzishwa mnamo mwaka wa 1997. Jean Kambanda, Waziri Mkuu wa mpito, aliyakubali mashtaka.[38]
ManenoMauaji ya kimbari ya Bosnia hutumika kurejelea mauaji ya kimbari yaliyofanywa na vikosi vya Kisabi pale Srebrenica mnamo mwaka wa 1995,[39] au kwa utakaso wa kikabila ambao ulifanyika wakati waVita vya Kibosnia vya mwaka 1992 hadi 1995 (mtazamo unaokataliwa na wasomi wengi).[40]
Mnamo mwaka wa 2001 Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Yugoslavia ya Zamani (ICTY kwa Kiingereza) yaliamua kuwa mauaji ya Srebrenica yaliyotendeka mwaka wa 1995 yalikuwa kitendo cha mauaji ya kimbari.[41]
Mnamo tarehe 26 Februari mwaka wa 2007Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), katika kesi ya Mauaji ya Kimbari ya Kibosnia yaliuunga mkono uamuzi wa awali wa ICTY kwamba mauaji ya Srebrenica yalikuwa mauaji ya kimbari, lakini yalipata kuwa serikali ya Kisabia haikuwa imeshiriki katika mauaji ya kimbari mapana zaidi katika eneo la Bosnia na Herzegovina wakati wa vita, jinsi serikali ya Kibosnia ilivyokuwa ikidai.[42]
Mnamo tarehe 12 Julai 2007,Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR kwa lugha ya Kiingereza) ikiikataa rufaa ya Nikola Jorgic dhidi ya kushitakiwa kwake kwa mauaji ya kimbari na mahakama ya Kijerumani (Kesi ya Jorgic dhidi ya Ujerumani) ilibainisha kuwa tafsiri pana ya mahakama ya Kijerumani kuhusu mauaji ya kimbari imekataliwa na mahakama ya kimataifa yanapozingatia kesi sawa.[43][44][45]
ECHR pia ilibainisha kuwa katikakarne ya 21 "Miongoni mwa wasomi, wengi wana maoni kwamba utakaso wa kikabila, haswa jinsi ulivyotendwa na vikosi vya Kisabi katika Bosnia na Herzegovina ili kuwafukuza Waislamu na Wakroati kutoka makazi yao , haukuwa mauaji ya kimbari. Hata hivyo, kuna idadi kubwa ya wasomi pia ambao wamependekeza kuwa matendo haya yalikuwa mauaji ya kimbari"[46]
Watu wapatao 30 wameshitakiwa kwa mauaji ya kimbari au kushiriki katika mauaji ya kimbari wakati wa miaka ya mapema ya 1990 nchiniBosnia. Hadi wa leo baada ya maombi mengi maalum mbele ya koti na hukumu chache ambazo zilifanikiwa kutupiliwa mbali baada ya rufaa Radislav Krstic tu ndiye aliyekuwa amepatikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya kimbari katika mahakama ya kimataifa.Kigezo:Marejeo yanahitajika Wengine watatu wamepatikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya kimbari nchini Bosnia na mahakama ya Kijerumani, mmoja wao akiwa Nikola Jorgic ambaye alishindwa katika rufaa dhidi ya hukumu yake katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu. Kesi za mashtaka zinaendelea nchini Bosnia na Herzegovina dhidi ya wanachama wengi wa zamani wa vikosi vya usalama vya Kibosnia na Kisabi kwa mashitaka mengi yakiwemo mauaji ya kimbari.
Slobodan Milosevic, alikuwa Rais wa zamani wa Serbia naYugoslavia na alikuwa mtu mwenye ushawishi mkuu zaidi wa kisiasa kuwahi kufikishwa mbele ya ICTY. Alifariki tarehe 11 Machi 2006 wakati kesi yake ambapo alituhumiwa kwa mauaji ya kimbari au kushiriki katika mauaji ya kimbari katika maeneo ndani ya Bosnia na Herzegovina ilipokuwa ikiendelea, kwa hivyo hakuna uamuzi uliorudishwa. Mnamo mwaka wa 1995 ICTY ilitoa kibali kwa ajili ya kukamatwa kwa Wasabia wa Kibosnia Radovan Karadzic na Ratko Mladic kwa mashitaka kadhaa ikiwemo mauaji ya kimbari. Mnamo tarehe 21 Julai 2008 Karadzic alikamatwa Belgrade, na kwa sasa yuko katika gereza la Hague akisubiri kesi yake. Ratko Mladic bado hajakamatwa.
Hadi wa leo mashitaka yote ya kimataifa ya mauaji ya kimbari yamefanywa katika mahakama maalum ya kimataifa. Tangu mwaka 2002, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yamepewa uwezo wa kushitaki kwa mujibu wa mamlaka yake ikiwa mahakama ya kitaifa hayana nia au hayawezi kuchunguza au kushitaka wahalifu wa mauaji ya kimbari, hivyo kufanywa kuwa "mahakama ya mwisho," na kuliachia mchi binafsi jukumu la kimsingi la kushtaki kwa mujibu wa mamlaka yake wanaodaiwa kuwa wahalifu. Kutokana na wasiwasi wa Marekani kuihusu ICC, Marekani inaonelea heri kuendelea kutumia mahakama ya kimataifa maalum kwa uchunguzi wa namna hiyo na mashitaka yatakayoibuka.[47]
Mgogoro unaoendelea katika eneo laDarfur,Sudan, ambao ulianza mwaka wa 2003, ulitangazwa kuwa "mauaji ya kimbari" na Katibu wa Nchi yaMarekaniColin Powell tarehe 9 Septemba, mnamo mwaka wa 2004 katika ushahidi mbele yaKamati ya Seneti ya Uhusiano wa Nje.[48] Hata hivyo tangu wakati huo, hakuna mwanachama mwingine wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambaye ameufuata mfano huo. Kwa kweli, mnamo Januari mwaka wa 2005, Tume ya Kimataifa ya Uchunguzi wa Darfur, iliyoidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Kimataifa Sheria nambari 1564 ya 2004, ilitoa taarifa kwa Katibu Mkuu ikisema kwamba "Serikali ya Sudan haijafuata sera ya mauaji ya kimbari."[49]
Hata hivyo, tume hiyo ilionya kwamba "hitimisho kwamba hakuna sera za uangamizaji zilizofuatwa na kutekelezwa katika eneo la Darfur na wenye mamlaka serikalini, moja kwa moja au kupitia wanamgambo chini ya udhibiti wake, haipaswi kueleweka kwa njia yoyote ile kama kutoashiria ukubwa wa hatia zilizofanywa katika kanda hiyo. Hatia za kimataifa kama vilehatia dhidi ya ubinadamu na hatia za kivita zilizofanywa katika eneo la Darfur zinaweza kuwa na uzito sawa na mauaji ya kimbari."[49]
Mnamo mwezi Machi mwaka wa 2005, Baraza la Usalama lilipeleka kirasmi swala la Darfur kwa mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, huku likiizingatia ripoti ya Tume lakini bila kuutaja uhalifu wowote maalum.[50] Wanachama wawili wa kudumu wa Baraza la Usalama,Umoja wa Marekani naUchina, hawakupiga kura kuhusu azimio la sheria ya kushtaki.[51] Kwa mujibu wa ripoti yake ya nne kwa Baraza la Usalama, Mwendesha mashitaka amepata "uwezekano wa kuweko na misingi ya kuamini kwamba watu waliotambulishwa katika Sheria ya Baraza la Usalama la Umoja wa Kimataifa nambari 1593] wamefanya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita," lakini hakupata ushahidi wa kutosha kuwashitaki kwa mauaji ya kimbari.[52]
Mnamo Aprili mwaka wa 2007, Waamuzi wa ICC walitoa vibali vya kukamatwa kwa ya aliyekuwa Waziri wa Nchi kwa ajili ya Mambo ya Ndani, Ahmad Harun, na kiongozi wa wanamigambowa Janjaweed, Ali Kushayb, kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita.[53]Mnamo tarehe 14 Julai mwaka 2008, waendesha mashitaka katikaMahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC), waliyaandikisha mashtaka kumi ya uhalifu wa kivita dhidi ya Rais wa SudanOmar al-Bashir: matatu ya makosa ya mauaji ya kimbari, matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na mawili ya mauaji. Waendesha mashitaka wa ICC wamedai kwamba al-Bashir "aliongoza upangaji na utekelezaji wa mpango wa kuharibu sehemu kuu" ya makundi tatu ya kikabila katika eneo la Darfur kwa sababu ya makabila yao.
Mnamo tarehe 4 Machi mwaka wa 2009 ICC ilitoa hati ya kukamatwa kwa Omar Al Bashir, Rais wa Sudan kadri Chumba cha utangulizi cha I cha ICC kilipohitimisha kuwa cheo chake kama mkuu wa nchi yake si kinga dhidi ya mashitaka mbele ya ICC. Hati ya kukamatwa ilikuwa kwa sababu ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Haikujumuisha uhalifu wa mauaji ya kimbari kwa sababu idadi kubwa ya waliokuwa katika Chumba cha utangulizi cha ICC hawakuona kama waendesha mashitaka walikuwa wametoa ushahidi wa kutosha kulijumuisha kosa hilo.[54]
Utangulizi wa CPPCG hausemi tu kuwa "mauaji ya kimbari ni kosa chini ya sheria za kimataifa, kinyume na roho na malengo ya Umoja wa Mataifa na linalokashifiwa na dunia iliyostaarabika", bali kwamba "katika vipindi vyote vya kihistoria mauaji ya kimbari yameleta hasara kuu kwa ubinadamu ".
Kuamua matukio ya kihistoria ambayo ni mauaji ya kimbari na ambayo ni tabia za kiuhalifu au unyama tu si jambo rahisi na wazi. Isitoshe, katika kesi zote ambapo shutuma za mauaji ya kimbari zimesambazwa, wanaotoka katika pande mbalimbali wanakana vikali tafsiri na maelezo ya tukio hilo, na hata mara nyingi huwa na maoni mbalimbali kuhusu ukweli. Mashitaka ya mauaji ya kimbari hayachukuliwi kimzaha na mara nyingi huzua utata. Majaribio ya wanaoangaliahistoria upya kuyakana mauaji ya kimbari (hasa mauaji ya kimbari ya Wayahudi) ni, katika nchi chache, kinyume na sheria.
Ili mauaji ya kimbari yatokee, mambo fulani yanafaa kuwepo. Kwanza kabisa ni utamaduni wa kitaifa ambao hauheshimu maisha ya kibinadamu inavyotakiwa. Jamii yenye uongozi wa kiimla, na itikadi zake zinazodaiwa kuwa bora kuliko zingine, ni jambo lingine linalofaa kuwepo kwa matendo ya mauaji ya kimbari kufanyika.[55]
Isitoshe, watu wa kundi linaloonekana kuwa na umuhimu mwingi lazima liwaangalie watu ambao huenda wakawa waathiriwa wa ukatili wao kama wao si binadamu kamili: kama “makafiri,” “watenda-unyama,” “watu ambayo hawajastaarabika,” “wasiomchamungu,” “waliokosa nidhamu,” “waliopingwa na miko,” “walio duni kirangi,” “watu wanaonuia kuharibu mpangilio wa kijamii,” “wanaopinga-mapinduzi,” na kadhalika.[56]
Hali hii pekee haitoshi kwa wahusika kufanya mauaji ya kimbari. Kufanya hivyo — yaani, kufanya mauaji ya kimbari — wahalifu wanahitaji wenye mamlaka wawe na nguvu na muungano na mpango wa ukiritimba na pia kuwe na watu wenye maradhi ya kiakili na wahalifu. Pia kampeni za wahusika za kuwawekea shutuma na kuwakosea utu waathiriwa zinahitajika, ambazo kwa kawaida huwa majimbo au serikali mpya zinazojaribu kulazimisha watu kuzifuata itikadi mpya na mipango yao ya kijamii.[57]
Mnamo mwaka wa 1996 Gregory Stanton rais wa shirika la kulinda dhidi ya mauaji ya kimbari aliwasilisha jarida kwa jina "Hatua 8 za mauaji ya kimbari" katika Idara ya Jimbo nchiniMarekani.[59] Katika jarida hilo alipendekeza kuwa mauaji ya kimbari hufanyika katika hatua nane ambazo ni za "kutabiriwa lakini ambazo haziwezi kuepukika kikamilifu".[59][60]
Jarida la Stanton liliwasilishwa katika Idara ya Jimbo, muda mfupi baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda na uchambuzi mwingi umejikita katika sababu iliyoyafanya mauaji hayo ya kimbari kufanyika. Hatua ya kinga alizozipendekeza, kulingana na shabaha ya awali ya watu ambao utafiti huo ulilenga, zilikuwa zile ambazo Marekani ingeweza kutekeleza moja kwa moja au ingeweza, kwa kutumia ushawishi, wake kufanya serikali nyingine kutekeleza.
Hatua
Sifa
Hatua Zuilifu
1. Uainishaji
Watu hugawanywa katika makundi ya "sisi na wao".
"Hatua kuu zuilifu wakati huu wa mapema ni kuendeleza taasisi zitakazowafikia wote na ambazo zitapunguza ...utengano."
2. Kufanya Mifano
"Ikijumuishwa na chuki, mifano inaweza kusukumwa kwa lazimi kwa wanachama wa vikundi vilivyotengwa ..."
"Ili kukabiliana na kufanywa kwa mifano, mifano ya chuki inaweza kufanywa kuwa haramu kisheria hasa hotuba za chuki."
3. Kunyima watu Utu
"Kundi moja linakana ubinadamu wa kundi lingine. Wanachama wa kundi hilo wanafananishwa na wanyama, viumbe viharibifu, wadudu au magonjwa. "
"Viongozi wa nchi na wa kimataifa wanapaswa kushutumu matumizi ya hotuba za chuki na kufanya hotuba hizo zisikubalike kitamaduni. Viongozi wanaochochea mauaji ya kimbari wanafaa kupigwa marufuku wasisafiri kimataifa na wanafaa kunyimwa fedha walizohifadhi katika nchi geni."
4. Mipangilio
"Mauaji ya kimbari daima hupangwa ...Vikundi maalum vya kijeshi au wanamgambo mara nyingi hupewa mafunzo na silaha ..."
"Umoja wa Mataifa unapaswa kuanzisha vikwazo vya kisilaha dhidi ya serikali na raia wa nchi zinazoshiriki katika michafuko ya mauaji ya kimbari, na kuunda tume ili kuchunguza ukiukaji wa sheria"
5. Ubaguzi
"Vikundi vya kueneza chuki hueneza matangazo yakipropaganda yenye ubaguzi..."
"Kuzuia kunaweza kumaanisha viongozi wa wastani kupewa ulinzi wa kisalama au msaada kwa vikundi vyahaki za binadamu ...Upinduzi wa serikali na makundi haramu lazima yashutumiwe kupitia vikwazo vya kimataifa."
6. Maandalizi
"Wahasiriwa hutambuliwa na kutengwa nje kwa sababu ya kabila au dini wanayojitambulisha nao..."
"Katika hatua hii, ni lazima Hali ya Dharura dhidi ya Mauaji ya Kimbari itangazwe..."
7. Uangamizaji
"Ni "uangamizaji" katika fikira za wauaji kwani hawaamini waathirika kuwa binadamu kamili."
"Katika hatua hii, ni hatua ya dharura pekee yenye kutumia nguvu na silaha inayoweza kuyakomesha mauaji ya kimbari. Maeneo bayana ya salama au maeneo ya kuwawezesha wakimbizi kutorokea lazima yaundwe na yawe na ulinzi imara wa kimataifa wenye silaha."
8. Kukana mauaji ya kimbari
"Wahalifu ... hukana kwamba walifanya uhalifu wowote ..."
"Jibu la kukana ni adhabu kupitia mahakama ya kimataifa"
Katika jarida la Baraza la Utafiti waSayansi ya Jamii Dirk Moses anazikosoa mbinu za Stanton akihitimisha:
Kutokana na mazoea haya yasiyoridhisha katika kuyakomesha mauaji ya kimbari, swali linalofaa kuulizwani mbona dhana ya "masomo ya mauaji ya kimbari" ishindwe kutazamia na kukomesha mauaji ya kimbari kwa ufasaha wa kutegemewa. Dhana ya "masomo ya mauaji ya kimbari," hasa jinsi yanavyoendeshwa katika eneo la Marekani ya Kaskazini, yana nguvu na udhaifu. Ingawa ujasiri wa kimadili na mikakati ya umma inafaa kupongezwa, dhana yenyewe inaonekana pofu kimaana katika miradi ya kiimpiriali ambayo ni sehemu ya shida na pia sehemu ya suluhisho. Serikali ya Marekani iliita Darfur mauaji ya kimbari ili kuyafurahisha mashirika ya kindani yanayotetea haki, na kwa sababu matamshi hao hayana umuhimu wowote. Machafuko ya Darfur yatakamilika kwa wakati utakaozifaa nguvu kubwa ambazo zina mambo yatakayozifaidi katika kanda hiyo.
Mnamo Tarehe 8 Desemba mwaka wa 2008, tume ya utenda kazi ya kuzuia mauaji ya kimbari, iliyosimamiwa naMadeline Albright, Katibu Mkuu wa zamani wa Marekani kama wenyekiti msimamizi, na William Cohen, Katibu Mkuu wa zamani wa Ulinzi waMarekani, ilitoa ripoti yake ya mwisho ambayo ilihitimisha kwamba serikali ya Marekani inaweza kuyazuia mauaji ya kimbari na ukatili mkubwa dhidi ya binadamu katika siku usoni.[62]
Katika mujibu wa maneno ya Bw. Kohen, “Ripoti hii inatoa mwongozo ambao unaweza kuiwezesha Marekani kuichukua hatua ya kuzuia, ikifanya kazi pamoja na washirika wa kimataifa, ili kuchelewesha mazingaombwe ya kesi za mauaji ya kimbari na visa vikubwa vya ukatili katika siku za usoni.”[63]
Kati ya mapendekezo ni:
jukumu la utendaji kwake rais wa Marekani ambalo litaonyesha Marekani na Dunia yote kwamba kuzuia mauaji ya kimbari na visa vikubwa vya ukatili ni kipaumbele cha taifa kitaifa
kuujenga mwili ndani ya Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani kuchambua vitisho na kuwaza juu ya hatua za kinga
kuanzisha mfuko wa dola milioni 250 wa kuizuia migogoro kuzuia na kukabiliana na machafuko
kusaidia kujenga mtandao wa kimataifa kwa ajili ya kubadilishana habari na uratibu wa hatua za kinga[64]
↑Verdirame, Guglielmo "The Genocide Definition in the Jurisprudence of theAd Hoc Tribunals",International & Comparative Law Quarterly (2000), 49: 578-598 Cambridge University Press, doi:10.1017/S002058930006437X.AbstractIlihifadhiwa 4 Juni 2011 kwenyeWayback Machine.
↑Naomi Klein.The Shock Doctrine: The Rise of Disaster Capitalism, Macmillan, 2007ISBN 0-8050-7983-1, 9780805079838.p. 101, see footnote
↑Oxford English Dictionary, second edition draft entry 2004. "genocide".
↑"By 'genocide', we mean the destruction of a nation or of an ethnic group."Axis Rule in Occupied Europe, ix. 79. As quoted in the 3rdOxford English Dictionary.
↑From a statement made by Mr. Morozov, representative of the Union of Soviet Socialist Republics, on 19 Aprili 1948 during the debate in the Ad Hoc Committee on Genocide (E/AC.25/SR.12).
↑See Vienna Convention on the Law of Treaties, opened for signature on 23 Mei 1969, United Nations Treaty Series, vol. 1155, No. I-18232.
↑William SchabasWar crimes and human rights: essays on the death penalty, justice and accountability, Cameron May, 2008ISBN 1-905017-63-4, 9781905017638.p. 791
12Kurt Jonassohn & Karin Solveig Björnson,Genocide and Gross Human Rights Violations in Comparative Perspective: In Comparative Perspective, Transaction Publishers, 1998,ISBN 0-7658-0417-4, 9780765804174.pp. 133-135
↑Origins and Evolution of the Concept in the Science Encyclopedia by Net Industries. states "Politicide, as [Barbara] Harff and [Ted R.] Gurr define it, refers to the killing of groups of people who are targeted not because of shared ethnic or communal traits, but because of 'their hierarchical position or political opposition to the regime and dominant groups' (p. 360)". But does not give the book title to go with the page number.
↑Daniel D. Polsby and Don B. Kates, Jr.of Holocaust and gun controlIlihifadhiwa 15 Januari 2008 kwenyeWayback Machine.,Washington University Law Quarterly 1997, (Cite as 75 Wash. U. L.Q. 1237). Article cites Citing Barbara Harff,Recognizing Genocides and Politicides, in GENOCIDE WATCH 27 (Helen Fein ed., 1992) pp.37,38
↑Oxford English Dictionary: 1944 R. LemkinAxis Rule in Occupied Europe ix. 79 "By 'genocide' we mean the destruction of a nation or of an ethnic group."
↑ECHR Jorgic v. Germany. § 42 citing Prosecutor v. Krstic, IT-98-33-T, judgment of 2 Agosti 2001, §§ 580
↑ECHRJorgic v. Germany Judgment, 12 Julai 2007. § 44 citing Prosecutor v. Kupreskic and Others (IT-95-16-T, judgment of 14 Januari 2000), § 751. In 14 Januari 2000 the ICTY ruled in theProsecutor v. Kupreskic and Others case that the killing of 116 Muslims in order to expel the Muslim population from a village, was persecution, not of genocide.
Andreopoulos, George J., ed. (1994).Genocide: Conceptual and Historical Dimensions. University of Pennsylvania Press.ISBN0812232496.{{cite book}}:|first= has generic name (help);Cite has empty unknown parameter:|coauthors= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
Conversi, Daniele (2005). "Genocide, ethnic cleansing, and nationalism". Katika Gerard Delanty, Krishan Kumar (eds) (mhr.).Handbook of Nations and Nationalism. Juz.lavol. 1. London: Sage Publications. ku.319–333.ISBN1412901014.{{cite book}}:|editor= has generic name (help);|volume= has extra text (help)
Harff, Barbara (Agosti 2003).Early Warning of Communal Conflict and Genocide: Linking Empirical Research to International Responses. Westview Press.ISBN0813398401.{{cite book}}:Cite has empty unknown parameter:|coauthors= (help)
Hochschild, Adam (1998).King Leopold's Ghost: A Story of Greed, Terror, and Heroism in Colonial Africa. Houghton Mifflin Harcourt.ISBN0395759242.{{cite book}}:Cite has empty unknown parameter:|coauthors= (help)
Rotberg, Robert I. (1996).From Massacres to Genocide: The Media, Public Policy, and Humanitarian Crises. Brookings Institution Press.ISBN0815775903.{{cite book}}:Unknown parameter|coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
Sunga, Lyal S. (1992).Individual Responsibility in International Law for Serious Human Rights Violations. Springer.ISBN0792314530.{{cite book}}:Cite has empty unknown parameter:|coauthors= (help)
Totten, Samuel (2008).Century of Genocide: Critical Essays and Eyewitness Accounts (tol.la3rd). Routledge.ISBN0415990858.{{cite book}}:Unknown parameter|coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
"Aegis Trust (genocide prevention trust)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2007-04-04. Iliwekwa mnamo2009-12-26. An independent international organisation dedicated to eliminating genocide
Worst Genocides of the 20th Century - a list of the some of the worst genocides in the 20th century. Listing from the most amount of victims to the least amount.