Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Mary I wa Uingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malkia Mary I.

Mary I wa Uingereza (pia anajulikana kamaMary Tudor na kama "Bloody Mary"; 18 Februari1516 - 17 Novemba1558) alikuwaMalkia waUingereza naIreland kutoka Julai1553 hadikifo chakemwaka wa1558.

Anajulikana hasa kwa jaribio lake la kubadiliMatengenezo yaKiingereza ambayo yalikuwa yameanza wakati wautawala wababa yake,Henry VIII na kurudisha nchi chini yaKanisa Katoliki. Jaribio lake la kurejesha kwaKanisamali iliyotwaliwa nawafalme wawili waliopita lilizuiwa kwa kiasi kikubwa naBunge la Uingereza. Lakini wakati wa utawala wake wa miaka mitano, Mary aliagizakesi dhidi ya wapinzani wa Ukatoliki zaidi ya 280 waliochomwamotoni wakiwa hai kamawazushi.

Mary alikuwamtoto wa Henry VIII namke wake wa kwanza,Katarina wa Aragon, ambaye peke yake kati ya watoto watumbo moja aliishi hadi kuwamtu mzima. Alirithi ufalme baada ya kifo chandugu yake mdogoEdward VI, aliyezaliwa na Henry VIII na mke wake wa tatu,Jane Seymour.

Baada ya kifo cha Mary kwenye mwaka 1558, hatua zake za kurudisha Ukatoliki katika Uingereza zilibatilshwa na mdogo wake namrithi,Elizabeth I, aliyezaliwa na Henry VIII na mke wake wa pili,Anne Boleyn.

Vyanzo

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMary I wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Mary_I_wa_Uingereza&oldid=1418841"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp