Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Martinique

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uwanja wa ndege wa Martinique
Martinique

Bendera
NchiBendera ya Ufaransa Ufaransa
Mji mkuuFort-de-France
Eneo
 - Jumla1,128km²
Idadi ya wakazi (2016)
 - Wakazi kwa ujumla376,480
Tovuti:  http://www.cr-martinique.fr/
Ramani ya Martinique.

Martinique (kwa Kifaransa; kwa Krioli: "Matinik" au "Matnik") nikisiwa chaAntili Ndogo katikaBahari ya Karibi. Nieneo la ng'ambo la Ufaransa namkoa (departement) waUfaransa. Hivyo ni sehemu yaUmoja wa Ulaya.

Eneo lake nikm² 1,128.

Makao makuu niFort-de-France.Miji mingine ni pamoja naSainte-Anne naSt. Pierre (iliyoharibiwa namlipuko wa volkeno yaMont Peleemwaka1902).

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Idadi ya wakazi ni 376,480. Takriban 83% ni waasili yaAfrika au machotara wa aina mbalimbali. Wazee wao waliletwa huko kamawatumwa kwa ajili yakazi katika mashamba yamiwa. Kikundi kikubwa cha pili niWahindi (10%),Wazungu (6%). Waliobaki niWaarabu,Wachina n.k.

Lugha rasmi niKifaransa, lakini wengi wanaongea piaKrioli yenye asili ya Kifaransa ambayo hata hivyo haieleweki tena naWafaransa waUlaya.

Upande wadini, wengi niWakristo: 86% niWakatoliki, 5.6%Waprotestanti.

Utamaduni

[hariri |hariri chanzo]

Martinique ni maarufu kwamuziki wake wazouk.Mwanamuziki mashuhuri wa aina hii niKassav.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]
  • Guadeloupe, eneo lingine la Ufaransa katika Bahari ya Karibi

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Serikali
Taarifa za jumla
Safari
Nchi huru
Kamili
Sehemu
Maeneo chini ya nchi nyingine
Udani
Ufaransa
Uholanzi
Ufalme wa Muungano
Marekani
Makala hii kuhusu maeneo yaBahari ya Karibi bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuMartinique kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Martinique&oldid=1266377"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp