Mark Feehily | |
---|---|
![]() Mark Feehily | |
Maelezo ya awali | |
Amezaliwa | 28 Mei1980 (1980-05-28) (umri 44) Sligo, Ireland |
Aina ya muziki | Pop |
Ala | Vocals, piano. |
Aina ya sauti | Tenor |
Miaka ya kazi | 1998–present |
Ame/Wameshirikiana na | Westlife |
Tovuti | www.westlife.com |
Mark Michael Patrick Feehily (amezaliwa tar.28 Mei1980 mjiniSligo,Ireland) ni msanii wa muziki wa pop kutoka nchiniIreland. Kijana huyu anajulikana zaidi kamaMark Feehily moja kati ya vijana ambao kwa pamoja huunda kundi laWestlife.
Mark ana wadogo zake wawili, Barry aliyezaliwa mwaka 19985 na Colin aliyezaliwa mwaka 1989. Wazazi wake ni Marie and Oliver Feehily.[1]
Katika kundi laWestlife Mark anatambulika kwa sauti yake nzito na hivyo imesikika katika nyimbo mbalimbali hasa katika viitikio na shairi la kwanza, na mara kadhaa akishirikiana naShane Filan
Kabla ya kujiunga na kundi la Westlife,Shane Filan naKian Egan walikuwa katika kundi la IOU ambapo ameshiriki katika utunzi wa nyimbo mbalimbali kama vile,Everlasting Love naTogether Girl Forever.
Feehily pia ameshirika katika kutunga nyimbo kadhaa za kundi la Westlife kama vile :[2]
Feehily anajulikana kwa watu wengi kuwa ni shoga. Hii ikiwa imetangazwa katika gazeti la Udaku la Uingereza laThe Sun, na ametangaza uhusiano wake wa muda mrefu naKevin McDaid, mwimbaji wa kundi la Uingereza la wavulanaV.[3][4] Katika mahojiano alisema "Maisha yangu yamekuwa bora zaidi, maisha yangu ya kimapezi hayawezi kunielezea mimi kama mtu, lakini ni kitu kikubwa kwa mtu yetote kuwa wazi kuhusiana nayo, imebadilisha maisha yangu moja kwa moja, najisikia mwenye furaha na mwepesi zaidi, Hiki ni kitu bora zaidi ambacho nimewahi kufanya" Tofauti na wenzake katika bendi hii, Freehili hapendi kuongelea maswala yake ya mahusiano. Mkurugenzi wakeLouis Walsh anasema, wakati anamchagua hakujua kuhusu maisha yake binafsi.[5]
Wawili hawa wamekuwa katika mahusiano tangu Januari 005, walipokutana katika tamasha laChildline lililofanyika nchiniIreland. Alipohijiwa katika mahojiano mengine, Feehili aliliambia gazeti laSydney Morning Herald Kuwa japokuwa mashabiki wa kundi hili wngi wao ni wasichana, hakujawa na mapokeo mabaya, anasema "Nia furaha sana sasa, na ninadhani hata mashabiki wetu wanaona hili" anasema "Katika miaka kadhaa hadi kufika hapa nilipo sasa, nilikuwa tayari kupitia katika mambo kadhaa kuhusiana na hisia zangu, lakini naweza kusema wazi kuwa, siku niliyoweza kukabiliana na woga huo, sikujali maekeo yake yangekuwa vipi, na hii ndio ilikuwa sehemu ngumu zaidi"
Feehily anasema kuwa, japo hajatarajia kufunga ndoa sasa, lakini ana furaha kujua kuwa, ataweza kufunga ndoa pindi atakapohitaji kufanya hivyo, ikiwa ni ndoa ya kiserikali[6] Wasema muda ukifika,wataweza kuangalia na kuoanga jinsi ya kufunga ndoa ya kiserikali
Mwezi Desemba mwaka 2007, Mark na Kevin walitokea katika ukurasa wa juu wa gazeti laAtitude, ambapo pia walifanya mahojiano. Katika mahojiano hayo Mark alisema kuwa anataka kuzeeka akiwa nae, na ana imani kuwa watakuwa pamoja daima.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link){{cite web}}
:Italic or bold markup not allowed in:|publisher=
(help)