Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Maria wa Bethania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kristo nyumbani mwa Martha na Maria kadiri ya mchoro waJohannes Vermeer (1654 hivi) unaotunzwa kwenyeNational Gallery of Scotland,Edinburgh. Maria ameketi miguuni paYesu.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
YesuKristo naUkristo

Umwilisho  •Utoto wa Yesu  •Ubatizo
Arusi ya Kana •Utume wa Yesu •Mifano ya Yesu  •Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura •Karamu ya mwisho •Msalaba wa Yesu  •Maneno saba
Kifo cha Yesu  •Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  •Ujio wa pili
Injili  •Majina ya Yesu katika Agano Jipya  •Yesu kadiri ya historia  •Tarehe za maisha ya Yesu •Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi •Kiaramu •Bikira Maria •Yosefu (mume wa Maria) •Familia takatifu •Ukoo wa Yesu •Ndugu wa Yesu •Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya ·Mitazamo ya Kikristo •Mitazamo ya Kiyahudi •Mitazamo ya Kiislamu •Yesu katika sanaa

Maria wa Bethania (jina lake kwaKiebrania מִרְיָם, Miryām, kwaKiaramu מרים,Maryām, kwaKigiriki Μαρία, Maria) alikuwamwanamke waBethania,kitongoji chaYerusalemu, katikakarne ya 1[1].

Ndugu zake walikuwaMartha naLazaro wa Bethania, ambao woteYesu alifurahiaurafiki wao hasaalipohiji kwenda Yerusalemu.

Wanaheshimiwa naWakristo wengi kamawatakatifu[2].

Sikukuu yao inaadhimishwa pamoja tarehe29 Julai[3] au4 Juni, kadiri yamadhehebu.

Maisha

[hariri |hariri chanzo]

Anajulikana hasa kutokana naInjili, kwa namna ya pekeeInjili ya Luka (10:38-42) naInjili ya Yohane (11; 12:1-8), katikaAgano Jipya ndani yaBiblia ya Kikristo.

Humo anaonekana mwenyesilika yautulivu naimani kwaYesu Kristo, ambaye alipendezwa sana nausikivu wake wakati alimfundisha ameketi chini karibu na miguu yake, kama ilivyokuwa kawaida yawanafunzi wadini ya Kiyahudi, ingawa wakati huowanaume tu walikubalika.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/96761
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/99081
  3. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMaria wa Bethania kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Maria_wa_Bethania&oldid=1324321"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp