Nchi wanachama zilipatana kuhusushabaha zifuatazo:
"(a) Kupatana ongezeko lahalijoto yawastaniduniani kwenye kiwango chini yasentigredi 2 ya wastani ya kipindi kabla yamapinduzi ya viwandani na kulenga mpaka wa ongezeko la halijoto kwa 1.5°C juu ya kiwango kabla ya viwanda, kwa kutambua ya kwamba hii itapunguza hatari ya mabadiliko ya tabianchi.
(b) Kuimarisha uwezo wa kupatana na athari hatari za mabadiliko ya tabianchi na kujenga unyumbukaji dhidi ya mabadiliko hayo na kupunguza ongezeko lagesijoto kwa njia zisizohatarishauzalishaji wavyakula.
(c) Kupatanisha sera yafedha na mwelekeo wa kupunguza gesijoto namaendeleo yenye unyumbufu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Kila nchi inatakiwa kupangasiasa yake ipasavyo na kuchukua hatua halisi na kutoa taarifa kuhusu hatua hizi kwaofisi ya UNFCCC na nchi nyingine.
Lakini mapatano hayana masharti ya kisheria, hivyo kila nchi inachangia kwahiari yake.
Nchi nyingi zilileta taarifa ya kwamba zilibadilisha sheria na maagizo kwa ajili yauchumi wao. Unyumbufu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi unadai mabadiliko kama vile