Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Malezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Darasa lawasichana wa Bamozai,Afghanistan.
Mwanafunzi darasani akipinga kuingizwa kwa siasa katika nyenzo za kusoma au walimu wanaotumia vibaya jukumu lao kufundisha wanafunzi, kinyume na malengo ya elimu ambayo hutafuta uhuru wa mawazo na kufikiria kwa kina.
Jan Steen (1672)

Malezi nikazi maalumu yamuda mrefu ambayobinadamu anamsaidia mwingine kukabilimaisha kwa jumla au sehemu yake mojawapo.

Ni kazi inayowapasa kwanzawazazi, ambao wanahitaji msaada waukoo,kabila,taifa,dini n.k.

Ni kazi inayohitajimoyo mkuu naustahimilivu mkubwa.

Nchi zaAfrika zilipojikomboa zilikazaniaelimu ili kupata mapemawataalamu kwa kazi nahuduma zajamii.

Hasa siku hizi wengi wameona umuhimu wa kusoma ili kukabili maisha. Ila mara nyingi juhudi hizo hazilengi kujuaukweli, bali kufanikiwa katika kazi nauchumi, na zinaweka pembenimaadili yaliyokuwa muhimu katikamalezi ya kimila.

Hayo yalikusudiwa kuwaandaawatoto navijana kwa maisha, wawe washiriki waukoo nakabila ambao wamekomaa kiasi cha kuweza kuchukuamajukumu yao.

Hata leo bila ya hayoujuzi naufundi vinaweza kuongezeka, lakiniukomavu haufikiwi.

Hivyo vijana wanachelewa kushika nafasi yao katika ujenzi wajamii, k.mf. kwa njia yandoa.

Badala yake unaeneauhuni (uasherati,bangi,wizi n.k.).

Kwa kuwaujana ni kipindi cha mabadiliko ya haraka pande zote, ni vigumu kuumudu sawasawa na kuwa na msimamo.

Hasamijini kuna mchanganyiko wawatu (makabila,dini n.k.) pamoja na njia hasi za kuishi zinazotokana na ushindani mkubwa, utepetevu katika maadili na upotovu.

Katika hali hiyo dini ya ukoo si kinga tena: kijana mwenyewe anajichagulia aamini nini na aishi vipi badala ya kufuata tu mazoea yanyumbani kama alivyofanya utotoni.

Anahitaji kusaidiwa ajibu maswali makuu ya maisha: “Mimi ni nani? Nimetoka wapi? Ninakwenda wapi? Nafikiriwa kuwa wa namna gani?”

Kumbe watu wazima wengi wanamsema badala ya kujihusisha naye katika matatizo yasiyoepukika yaumri wake.

Anahitaji kueleweka na kuthaminiwa, lakini akitafuta hayo anaitwa jeuri, mwenyekiburi n.k.

Hasa siku hizi kati yawazee na vijanaumbali ni mkubwa kutokana na mabadiliko ya nyakati (upande wa elimu,afya, uchumi,mawasiliano,tunu za maisha n.k.).

Vijana wanaonelea miundo asili ni mambo ya zamani, hata wakadharauutamaduni wamababu kama kwamba mambo yake yote yamepitwa na wakati.

Kinyume chake wanapokea kwa urahisi mkubwa mawazo mengi ya kigeni kupitiavyombo vya upashanaji habari namitindo mipya inayozuka mijini.

Halafu wanatumia muda mwingi kijiweni au katikaburudani, kumbe ule wa kukaa na wazee ni mfupi mno: hilo ni pengo lisilozibika, kwa kuwa linawafanya wasifaidimang’amuzi ya vizazi vilivyotangulia, kutegemezwa na mashauri wanayoyahitaji, kuungana nandugu zao katika kukabili maisha.

Wanakuwa jamii tofauti, wageni kati ya watu wao! Maisha ya vijana kwa mtazamo wa sasa yanazidi kuwa tofauti na vijana wa zamani. Nyakati hizi kuna matatizo mengi yawapatayo vijana pamoja na wakati waubalehe, uzururaji mitaani,wizi, uvutajibangi pamoja na kutumia aina nyingine zamadawa ya kulevya.

Wazee wengi wanaona vijana wakiungana ni nafasi tu ya kujengaurafiki mbaya, sihaja halisi yanafsi na ya maisha.

Hivyo badala ya kuwasaidia kuchambua mambo wanazidisha hali ya kutoelewana nao.

Basi, hatuna budi kulea kwa kuoanishaujuzi na ukomavu ili tupate watu tunaowahitaji: watu ambao ni huru kwa ndani na wanaweza kuwajibika kwauadilifu.

Ili kijana azidi kukomaa kiutu anahitaji kusaidiwa ajifahamu ili kustawishavipawa vyake na kupunguzakasoro zake.

Utu ndio msingi ambao juu yake yanajengwa maisha yote.

Mwenye matatizo nafsini mwake anasumbuka na kusumbua watu anaofungamana nao.

Basi, ni muhimu awahi kujirekebisha kama inavyobidi kuwahi ili kunyoshamti ukiwa bado mbichi.

Ni lazima aifanyie kazinafsi yake kwaustadi nabidii nyingi kulikomkulima anavyoshughulikiashamba lake ili lizae sana.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMalezi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Malezi&oldid=1166352"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp