Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Malaysia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shirikisho la Malaysia
Malaysia
مليسيا (Jawi)
Kaulimbiu:Bersekutu Bertambah Mutu
("Umoja Huongeza Ubora")
Wimbo wa taifa:Negaraku ("Nchi Yangu")
Mahali pa MalaysiaMahali pa Malaysia
Mji mkuu
na mkubwa
Kuala Lumpur
Lugha rasmiKimalay (Melayu)
Lugha ya taifaKiingereza
Kabila (2023)
Dini (2020)
 Mfalme
Ibrahim Iskandar
Anwar Ibrahim
  Uhuru wa Malaya
31 Agosti 1957
  Utawala wa Sarawak
22 Julai 1963
  Muungano wa Malaysia
16 Septemba 1963
Eneo
  Jumlakm2 330,803(ya 67)
  Maji (asilimia)0.3%
Idadi ya watu
  Kadirio la 202434,564,810
  Msongamano101/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
  Jumla $1.470 trilioni
  Kwa kila mtu $43,470
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
  Jumla $444.98 bilioni(ya 35)
  Kwa kila mtu $13,140
HDI (2023) 0.819
-juu sana
Gini (2021)40.7
SarafuRinggit ya Malaysia (RM) (MYR)
Majira ya saaUTCUTC+8 (MST)
Msimbo wa simu+60
Jina la kikoa.my
Ramani ya Malaysia.

Malaysia, rasmi kamaShirikisho la Malaysia, ni nchi katikaAsia ya Kusini-Mashariki, inayojumuishaRasi ya Malay na sehemu ya kaskazini ya kisiwa cha Borneo, pamoja na visiwa vichache vidogo.Inapakana naUthai kaskazini,Singapore kusini,Brunei naIndonesia mashariki. Mnamo 2024 Malaysia ina idadi ya watu takriban milioni 34, ikiwa ya 44 duniani. Jiji lake kubwa zaidi niKuala Lumpur, ambalo pia nimji mkuu. Malaysia inajulikana kwa utofauti wake wa kitamaduni, rasilimali asili tajiri, na maendeleo ya haraka ya uchumi, ikifanya kuwa nchi muhimu katika Asia ya Kusini-mashariki. Kisiasa Malaysia nishirikisho la majimbo 13 na maeneo ya shirikisho 3.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Nchi ilianzishwa mwaka1963 wakatiShirikisho la Kimalay(kwaKimalay: Persekutuan Tanah Melayu) liliungana naSingapur,Sabah naSarawak ambazo awali zilikuwa chini yaUingereza.

Hata hivyoSingapur iliondoka mwaka1965 ikawa nchi ya pekee.

Utawala

[hariri |hariri chanzo]

Majimbo ya Shirikisho

[hariri |hariri chanzo]

Malaysia ni Shirikisho la Kifalme. Tisa kati ya majimbo yake 13 nisultani chini ya utaratibu wa kifalme na manne hufuata muundo wajamhuri.

Majimbo ya shirikisho ni kama yafuatavyoː

Sultani tisa zinazoongozwa naSultani pamoja nawaziri mkuu anayechaguliwa nabunge la jimbo:

Majimbo manne chini yagavana anayeteuliwa naserikali kuu na waziri mkuu anayechaguliwa na bunge la jimbo:

Maeneo matatu ya shirikisho:

Demografia

[hariri |hariri chanzo]

Wakazi ni mchanganyiko mkubwa, lakiniWamalay (50.1%) na wakazi asili wengine walioWaislamu wanapewa nakatiba ya nchi nafasi ya pekee.Wachina ni 22.6%.Wahindi ni 7.3%

Lugha rasmi niKimalay, lakini zinatumika pialugha nyingine 136.

Msikiti wa Kitaifa Kuala Lumpur

Dini rasmi niUislamu unaofuatwa na 61.3% za wakazi (wengi wakiwaWasuni), wakati 19.8% niWabuddha, 9.2% niWakristo, 6.3% niWahindu, 1.3% ni wafuasi wa dini za Kichina (Ukonfusio naUtao).

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iran |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuMalaysia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Malaysia&oldid=1454063"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp