Makka (rasmi:Makkah al-Mukarramah;Kar.: مكة المكرمة) nimji waUfalme waUarabuni wa Saudia. Ina wakazi 1,294,167(mwaka 2004). Mji uko kwenye bonde la Ibrahimu mnamokm 80 kutoka pwani laBahari ya Shamu na bandari yaJeddah. Mazingira ya mji ni jangwa mahali penyewe kuna visima vilivyowezesha kuwepo kwa mji tangu kale.
Makka ni mji mtakatifu waUislamu. Kila mwaka mamilioni wa Waislamuwanahiji kwenda Makka. Wakati huu wa hajj wanajaribu kufuata nyayo zamtume Muhammad. Makka ni mji uliofungwa kwa wasio Waislamu.
Kwa Waislamu Makka ni mji wa kuzaliwa kwake mtume Muhammad pia mahali alipokaa alipoanza kupokea aya zaKurani. Mjini kuna pia jengo laKaaba linaloaminiwa ni msikiti iliyojengwa naAdamu na kutengenezwa upya naIbrahimu (Abrahamu).
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuMakka kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.