Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Majira ya baridi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tallinn,mji mkuu waEstonia, ulivyofunikwa natheluji tarehe1 Januari2010.
Theluji kaskazini mwa dunia:Kuusamo,Ufini.
Theluji kusini mwa dunia:Tierra del Fuego,Argentina.

Majira ya baridi (pia:kipupwe; kwaKiingerezaWinter) ni mojawapo kati yamajira manne ya kanda za wastani, nahalijoto yake ni yabaridi kuliko majira mengine. Ni kinyume chamajira ya joto auchaka.

Pengine baridi inakuwa kali sana na kuendana nabarafuto: ndiyo maana maeneo mengine yadunia hayana wakazi wa kudumu, hasabara laAntaktiki.

Yanafuatamajira ya kupuputika majani (kwa KiingerezaFall auAutumn) na kutanguliamajira ya kuchipua (kwa KiingerezaSpring).

Majira hayo yanatokeaduniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyokaskazini aukusini kwaikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfanoKenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.

Majira hayo tofauti hupatikana zaidi katikaukanda watropiki.

Wanyama, mimea, binadamu na majira ya baridi

[hariri |hariri chanzo]

Ili kuhimili ukali wa majira ya baridi,wanyama wengi wana njia mbalimbali zakimaumbile nakitabia.

  • Uhamaji ni mbinu mojawapo inayotumiwa hasa nandege wakati wa baridi. Hata hivyo, ndege wengi hawahami. Baadhi yavipepeo pia huhamamsimu huu.
  • Wanyama wengine hulala ili kupunguza shughulimetabolimwilini wakati wa majira ya baridi. Wanyama hao, kama vilevyura,nyoka, napopo huamka msimu huu unapomalizika.
  • Wanyama wengine huhifadhichakula watakachokula wakati wa majira ya baridi.
  • Wanyama wengine wenye manyoya hukuza manyoya yao kama wakati wa baridi; hii inaboresha uwezo wa manyoya kuhifadhijoto.
  • Msimu huu huathiri pia tabia za wanyama. Kwa mfanopanya kawaida huishi chini ya theluji.
  • Baadhi yamimea ya kila mwaka haiwezi kuishi wakati wa baridi. Hata hivyo, mimea mingine ya kila mwaka inahitaji baridi kukamilisha mzunguko wamaisha yao. Baadhi ya mimea ya msimu hufaidika kwa kufunikwa na theluji wakati mimea mikubwa huacha sehemu ya juu kulala hukumizizi yake ikihifadhiwa na theluji.

Binadamu nao hufanya mambo mbalimbali ili kuweza kukabiliana na majira ya baridi.

  • Baadhi ya nyumba za majira ya joto, ambazo zilijengwa kwa ajili ya matumizi ya majira ya joto tu zinahitaji kutunzwa wakati wa majira ya baridi. Wakati wa msimu huu nyumba hizo hutunzwa kwa kufungwa, kuzimamaji,umeme, na mistari yasimu, na kulinda vipengele mbalimbali kutokana na theluji kubwa.

Kwa mfano katika eneo laNew England, nchiniMarekani,familia nyingitajiri zilizoishi humo wakati wakarne ya 19 zilikuwa na nyumba za majira ya joto milimani ili kuondoka mwanzoni mwamagonjwa kwahoma ya njano na magonjwa mengine ambayo mara nyingi yalijitokeza katika miezi ya majira ya joto.

  • Mabwawa yasamaki yanahitaji hatua kadhaa za ziada ili kuhakikisha kuwa samaki wanaishi vyema wakati wa baridi.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Viungovyanje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMajira ya baridi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Majira_ya_baridi&oldid=1205160"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp