Majimbo ya Afrika Kusini ni ngazi ya kwanza yaugatuzi nchiniAfrika Kusini. Nchi imegawanywa katika majimbo tisa.[1] Katika mkesha wa uchaguzi mkuu wa 1994 nchi ilikuwa na majimbo manne halafu kulikuwa na maeneo yabantustan. Kabla ya uchaguzi huo wa kwanza ulioendeshwa bila ubaguzi wa rangi maeneo ya bantustan yaliunganishwa tena kisheria na Afrika Kusini na nchi yote iligawiwa kwa majimbo tisa.
Majimbo na maeneo ya bantustan kama ilivyokuwa mwisho wa ubaguzi wa rangi
Wakazi wasio Wazungu walibanwa katika maeneo maalum kuanzia mwaka 1913. Umiliki wa ardhi kwa watu weusi ulizuiliwa kwa maeneo fulani ya jumla ya 13% ya nchi yote. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1950, maeneo haya yalibadilishwa hatua kwa hatua kuwa "homelands" au"bantustan". Nne kati ya nchi hizi zilitangazwa kama nchi za pekee za watu weusi wakati wa enzi yaapartheid . Mnamo 1976, nchi yaTranskei ilikuwa ya kwanza kukubaliuhuru kutoka kwa Afrika Kusini, na ingawa uhuru huu haukuwahi kutambuliwa na nchi nyingine yoyote, nchi zingine tatu. – Bophuthatswana (1977), Venda (1979) na Ciskei (1981) – zilifuata kukubali uhuru bandia.
Tarehe 27 Aprili 1994, tarehe ya uchaguzi wa kwanza usio wa ubaguzi wa rangi ambako pia Katiba ya Muda ilipitishwa, majimbo haya yote na nchi za bantustan zilivunjwa, na majimbo tisa mapya yalianzishwa.[2]