Mahdi (piamehdi; kwaKiarabu مهدي -anayeongozwa) nicheo chamwokozi wadunia katikaimani yaUislamu.
Kufuatana na imani hiyo mwokozi huyu atatumwa naAllah kabla ya siku za mwisho wa dunia yaani kabla yasiku ya hukumu (yawm al-qiyamah) na atasafisha dunia na kila aina yadhambi, ukandamizaji nautawala mbaya.
KatikaKurani hakuna maelezo ya wazi juu ya kuja kwa Mahdi lakini anatajwa katikahadithi mbalimbali; isipokuwaSahih al-Bukhari haina habari zake. Katika imani ya Waislamu wengi (hasaWashia lakini pia katika mielekeo kadhaa yaWasunni) mahdi ina nafasi muhimu.
Mahdi anategemewa kuwa atawaongozabinadamu kumwaminiMungu na kumshindaDajal anayetazamiwa kuwa mwovu kati ya wanadamu. Mahdi ataongozwa moja kwa moja na Allah. Waislamu wengi wanaona ya kwamba ataongoza jitihada kwa kutumia nguvu ya silaha lakini kundi laAhmadiyya wanasisitiza kuwajihad yake itakuwa ya kiroho tu.
Katika imani ya Washia mahdi anajulikana tayari jina lake: niMuhammad ibn Hasan al-Mahdi aliyezaliwatarehe29 Julai869 akawaimamu wa 12 wa Washia, lakini tangu mwaka874 alifichwa na Allah mbele ya maadui zake na tangu wakati ule anaishi mafichoni (ghaiyba).
Kati ya Wasunni kuna mafundisho tofautitofauti kuhusu mahdi. Wanaokubali hadithi juu yake huamini atazaliwa katikaukoo wamtumeMuhammad na atatawala dunia pamoja naYesu atakayerudi duniani kwa muda wa miaka 40.
Lakini Wasunni wengine hawakubali hadithi juu ya Mahdi.
Hata hivyo, imani katika ujio wa Mahdi ilikuwa na umuhimu mara kadhaa hata kati ya Wasunni. Mashuhuri alikuwaMuhammad Ahmad aliyejitangaza kuwa Mahdi mnamo mwaka1881 akafaulu kuundaDola la Mahdi katikaSudan.