Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Magnificat

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Magnificat kadiri yaJames Tissot - Brooklyn Museum,Marekani.
Tafsiri mbalimbali zaMagnificat hukoEin KaremKanisa la Ziara.

Magnificat (neno laKilatini lenye maana ya: "Inatukuza") ni jina lautenzi unaotumika sana katikaliturujia yamadhehebu mbalimbali yaUkristo, hasa katikaMasifu ya jioni[1]. Jina hilo linatokana na neno la kwanza la wimbo huo katikatafsiri ya Kilatini.

Wimbo huo ni maarufu pia kamaWimbo wa Maria, kutokana namtunzi wake kadiri yaInjili ya Luka 1:46-55.

Ni mmojawapo kati ya nyimbo nne zinazopatikana katikaInjili hiyo.[2][3]

Humo tunasoma kwambaBikira Maria alitoa moyoni maneno hayo ya sifa kwaMwenyezi Mungu akiwa namimba ndogo yaYesu baada ya kumshangiliwa najamaa yakeElisabeti aliyeangazwa naRoho Mtakatifu kuhusu hali yake yaujauzito na kuhusu ukuu wa mtoto huyo hata akamuita "Mama waBwana wangu". Elisabeti alimpongeza Maria kwabaraka hiyo aliyoipata, kubwa kuliko ile yawanawake wengine wote. Pia alimpaheri kwaimani yake.

Maneno yake ni haya:
Nafsi yangu yatangaza ukuu wa Bwana,
roho yangu inamshangilia Mungu, mwokozi wangu;
kwa sababu ameona unyonge wa mtumwa wake.

Tangu sasa vizazi vyote vitanipongeza,
Kwa sababu Mwenyezi amenitendea makuu;
jina lake takatifu,
ne rehema zake hufikia uaminifu wake
kutoka kizazi hadi kizazi.

Hufanya ushujaa kwa mkono wake:
huwatawanya wenye kiburi moyoni,
huwaangusha wenye nguvu kutoka katika viti vyao vya enzi
na kuwainua wanyonge,
huwashibisha wenye njaa vitu vyema,
na matajiri huwafukuza mikono mitupu,

Umsaidie Israeli, mtumishi wake,
akikumbuka rehema kama alivyowaahidi baba zetu.
Kwa neema ya Ibrahimu
na kizazi chake milele.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. Ufafanuzi waBeda Mheshimiwa unapatikana katika Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk
  2. The History and Use of Hymns and Hymn-Tunes by David R Breed 2009ISBN 1-110-47186-6 page 17
  3. Favourite Hymns by Marjorie Reeves 2006ISBN 0-8264-8097-7 page 3-5

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Familia
Maisha
Maisha ya awali katikaMapokeo
KatikaBiblia
Maisha ya baadaye katikaMapokeo
Apokrifa
Mariolojia
Ukristo
Uislamu
Heshima
Sifa
Sala
Sanaa
Ukristo wa Magharibi
Ukristo wa Mashariki
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMagnificat kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Magnificat&oldid=1454517"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp