Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Magnesi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Magnesi (Magnesium)
Jina la ElementiMagnesi (Magnesium)
Namba atomia12
Mfululizo safuMetali za udongo alkalini
Uzani atomia24,305 u
Valensi2, 8, 2
Ugumu (Mohs)1–2.5
Kiwango cha kuyeyuka923 K (650 °C)
Kiwango cha kuchemka1380 K (1107 °C)

Magnesi (piamagnesiamu) nielementi nametali ya udongo alkalini yenyenamba atomia 12 kwenyemfumo radidia inauzani atomia 24.3050.Alama yake niMg.Jina linahusiana naneno laKigiriki μαγνησιη (magnesia -sumaku) hata kama Mg hainatabia zakisumaku.

Elementi tupu inavalensi mbili narangi yake ninyeupe-fedha. Mg ni kati ya elementi zinazopatikana kwa wingiduniani ikiwa na nafasi yanane naasilimia 1.4 zaganda la dunia ni magnesi.

Inamenyuka kwa urahisikikemia, hivyo haitokei kama elementi tupu lakini kwakampaundi mbalimbali, hasa katikamagnesiti,dolomiti namadini mengine. Katikamaji yabahari iko kwa kiwango chakg 1 kwa kila.

Unga wa magnesi au vipande vidogo vya metali huunguamoto mkali mweupe, unga hata bila kuwashwahewani tu.

Magnesi ni muhimu kwamiili yawanadamu nawanyama, pia kwamimea.Wanamichezo hutumia mara nyingidawa ya magnesi wakitaka kuboreshambio au kuongezewanguvu.

Picha

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMagnesi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Magnesi&oldid=1300064"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp