Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Magimbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Majani ya magimbi
Magimbi sokoni

Magimbi,majimbi aunduma (Kiing.taro) ni kimoja yavyakula vyenye asili ya sehemu ya chini yashina lamimea fulani. Hupatikana sehemu mbalimbaliduniani. Yanafanana naviazi au hatamatunguu lakini huitwamashinagimbi. Mmea wao huitwamgimbi,mjembe,mjimbi aumyugwa (Colocasia esculenta) unaoainishwa katikafamiliaAraceae.

Magimbi hupendwa sana na watu, hasa kwenye msimu waRamadhani kamafutari. Mara nyingi hupikwa kwa nazi. Na watu waUnguja huita zege kwa sababu tu, chakula kitamu na ukila sana unavimbirwa haraka mno. Isitoshe hakiishi haraka tumboni. Kuna miundo mingi ya upishi wa magimbi, aidha kwa kuchemsha tu (chukuchuku) au utie na nazi (hasa kwa watu wa Pwani), yaani,Tanga,Mombasa,Kilwa,Zanzibar na kwingineko. Chakula hiki hakina tabia ya kuliwa sana katika miezi ya kawaida. Ndiyo maana upatikanaji wake wakati mwingine inakuwa vigumu kiasi. Kuna baadhi ya maneo hupatikana sana, lakini kwingineko inakuwa shida. Mara nyingi yanauzwa masokoni au katika masoko yasiyo rasmi, yaani, barabarani.

Colocasia esculenta inasemekana ina asili ya huko kusini mwaIndia naAsia ya Kusini, lakini vilevile huko ndiko hasa inakolimwa mno. BaraniAfrika,Oceania na India Kusini ni chakula kikuu na huenda ikawa ni miongoni mwa vyakula vilivyowahi kulimwa tangu hapo awali. Vilevile inaaminika ya kwamba chakula hiki ni maarufu huko India,Nepal naBangladesh, na kutoka huko kinaenea hadi Kusini mwa Asia, Mashariki ya Asia naVisiwa vya Pasifiki; magharibi hadiMisri halafu kusini kisha Mashariki na Magharibi mwa bara la Afrika. Kutoka huko yakaenea hadi huko visiwa vyaKaribi naAmerika.

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala bado nimbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuongezea habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Magimbi&oldid=1321712"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp