Kuna mifumo mbalimbali ya macho kati ya aina mbalimbali zawanyama.
Macho ya kimsingi kwaviumbehai vidogo yanatambua tu kamamazingira yana mwanga au la. Hata kati ya viumbehai wenyeseli moja kuna wenyeprotini zinazotofautishagiza nanuru. Kunakonokono ambao hawawezi "kuona"picha ya mazingira lakini wanatambua mwanga na uwezo huu unawawezesha kuepukana na mwanga wajua ambao ungewakausha.
Macho yaliyoendelea kiasi yanaumbo kamakikombe na hili linawezesha kutambua upande gani nuru inatokea.
Wanyama wengi huwa na macho yaliyoendelea zaidi: yana uwezo wa kuona picha halisi ya mazingira pamoja narangi namwendo.
Wadudu naarthropoda huwa namacho ya kuungwa na vijicho vingi vidogo vinavyoitwaomatidi; kila kijicho huwa na umbo lakijiti na kwenye mwisho wake kuna lenzi yachitini. Mdudu anaweza kuwa na vijichoelfu kadhaa na picha ya mazingira inaunganishwa kutokana na picha nyingi ndogo za kila kijicho.
Macho haya ya kuungwa yanamwezesha mdudu kuangaliaasilimia kubwa ya mazingira yake: kwa aina kadhaa hata nyuma yake. Macho ya kuungwa yanaweza kufunika hadi asilimia 80 ya eneo lakichwa. Mdudu haoni vikali kama mtu lakini anaona mabadiliko na mwendo haraka sana.
Wanyama wanaoishi katikavilindi vyabahari penye giza nene huwa na macho ambamofuwele ziko kamakioo na kupazia nuru hafifu.
Kuna wanyama wanaoweza kuona nuru ambayo ni nje yaupeo wa kibinadamu; kwa mfanonyuki huonamnururisho wainfraredi.
Shida za macho ni nyingi kama vileupofu, kutoonarangi, macho kujiliza, wekundu uliokithiri pamoja na kutoa majimaji. Shida hizo huletwa navumbi, kuzaliwa ukiwakipofu,jua jingi bila kuvaliamiwani vizuia jua.
Makala hii kuhusu mambo yaanatomia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuJicho kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.