Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Macau

Majiranukta:22°10′N113°33′E /22.167°N 113.550°E /22.167; 113.550
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Macau
Mkoa maalum wa utawala wa China
澳門特別行政區 (Kichina)
Região Administrativa Especial de Macau da República Popular da China(Kireno)
Eneo la MacauEneo la Macau
Lugha rasmiKichina
·Kireno
  Mtendaji mkuu
Ho Iat Seng
  Kuanzishwa kwa mji
Karne ya 5 BK
  Iliundwa na wenyeji Wachina kutwaliwa na Ureno
1557
  koloni ya Ureno
31 Agosti 1862
  Mkoa mwenye utawala wa pekee wa Jamhuri ya Watu wa China
20 Desemba1999
Eneo
  Jumlakm2 30.3
Idadi ya watu
  Kadirio la 2015642,900
  Msongamano18,568/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2025
  Jumla $98.64 billioni(ya 139)
PLT (Kawaida)Kadirio la 2025
  Jumla $59.27 bilioni
HDI (2022)0.925juu sana
SarafuPataca ya Macau
Majira ya saaUTC+8 (MST)
Jina la kikoa.mo
Tanbihi:
1 Mji mkuu ulikuwa "Cidade do Nome de Deus de Macau" au rasi ya Macau yenyewe; makao makuu ya serikali ya koloni yalikaa kwenye tarafa ya Sao Lorenco.
2 Habari kutokaDirecção dos Serviços de Estatística e Censos (ofisi ya takwimu ya Macau )
Makao Makuu ya serikali ya Macau

Macau (Kireno: Macau;Kichina: 澳門; pinyin: Àomén), rasmiMkoa Maalum wa Utawala wa Macao, ni jiji la pwani na Mkoa Maalum wa Utawala (SAR) lilio kusini mwaUchina, likiingilia kati ya Delta ya Mto Pearl kutoka Hong Kong. Kwa eneo la kilomita za mraba 32.9 (maili 12.7), ni mojawapo ya maeneo yenye idadi kubwa ya watu kwa kilomita za mraba duniani, na idadi ya watu inakadiriwa kuwa karibu 700,000. Ikiwa imeorodheshwa kuwa ya 184 kwa ukubwa wa eneo, Macau ina msongamano mkubwa wa watu wa takriban 21,000 kwa kila kilomita ya mraba.

Tarehe23 Oktoba2018rais wa ChinaXi Jinping alizindua rasmidaraja la baharini refu kuliko yoteduniani (kilometa 55) linalounganishaHong Kong, Macau na China bara (mji waZhuhai).

Koloni la Ureno

[hariri |hariri chanzo]

Macau ilikuwa kituo chaUreno tangukarne ya 16 na Wareno wakaikodi tangu mwaka1670.

Macau kamakoloni ilithibitishwa katikaMkataba wa Beijing wa mwaka1887 kati ya China na Ureno.

Macau kama eneo la pekee la China

[hariri |hariri chanzo]

Mwaka1999 ilirudishwa mikononi mwaserikali ya China lakini kwa hali ya pekee inayofanana na ile ya eneo la jirani laHong Kong.

Hivyo Macau inaendendelea kuratibu yenyewe mambo yake kwa ndani, lakinimadaraka kuhusuusalama,jeshi nasiasa ya nje yakoBeijing.

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Wakazi wengi (88.4%) ni Wachina asilia, 1.8% ni Wareno. Kwa kuwauzazi ni mdogo sana, kunawahamiaji wengi, hasaWafilipino (4.6%) naWavietnam (2.4%).

Lugha rasmi niKichina naKireno. Katika matumizi ya kawaida, Kichina cha Canton kinaongoza (87.5%), naKiingereza kina waongeaji wengi (2.8%) kuliko Kireno (0.7%).

Upande wadini, 58.9% wanafuatadini za jadi za Kichina (mchanganyiko waUkonfusio naUtao), 17.3% niWabuddha au Watao, 7.2% niWakristo. 15.4% hawana dini yoyote.

Uchumi

[hariri |hariri chanzo]

Uchumi wa Macau hutegemeautalii na hasamichezo yakamari. Kuna piaviwanda vyanguo.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Serikali
Taarifa za jumla
Utalii
Malezi
Michezo

22°10′N113°33′E /22.167°N 113.550°E /22.167; 113.550

Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iran |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaChina bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuMacau kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Macau&oldid=1472831"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp