Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Maandishi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya mwandishi (Misri ya Kale).
Mitindo ya maandishi duniani
buluu:alfabeti ya Kilatini;kibichi:alfabeti ya Kiarabu;nyekundu:Kisirili;njano:mwandiko wa Kichina;kichungwa: miandiko ya Kihindi.

Maandishi (pia:maandiko) nihati ambayo hushikasauti zalugha kwa njia yaalama zinazoandikwa.

Mitindo ya miandiko

[hariri |hariri chanzo]

Sehemu kubwa ya maandishiduniani inatumiaalfabeti mbalimbali. Kati yakealfabeti ya Kilatini imesambaa zaidi, ikifuatwa naalfabeti ya Kiarabu naalfabeti ya Kisirili.

Asia ya Mashariki imeendelea kutumia mwandiko wake wa alama zinazodokezaneno lote badala yaherufi tu. Mtindo wa kutumia alama kwa neno lote ulitumika pia katikautamaduni waMisri ya Kale naMeksiko ya Kale.

Miandiko yaUhindi, inayotokana namwandiko wa Brahmi, hutumia miandiko mbalimbali inayoonyeshasilabi. Hatalugha za Ethiopia hufuata mtindo wa kufanana nayo.

Historia ya maandishi

[hariri |hariri chanzo]

Hakuna hakika maandishi yalianza lini na wapi, ilawataalamu wengi huona ya kwambaSumer katikaMesopotamia ilikuwa ya kwanza duniani.

Wengine huona ya kwambasanaa ya kuandika ilianzishwa na watu mbalimbali kwa nyakati tofauti katika pande mbalimbali za dunia. Si rahisi kuwa na hakika kwa sababu maandishi yenyewe hudumu kwa muda tu kutegemeana namata navifaa vilivyotumiwa.

Maandishi yaliyowekwa penyemawe magumu tena penyehali ya hewayabisi hukaa miakaelfu kadhaa. Kwa njia hiyo tunaushuhuda wa maandishi ya mapema hasa kutoka nchi kamaMesopotamia,Misri,Bara Hindi naChina. Lakini hatuwezi kukanusha uwezekano wa maandishi yaliyotumia mata kamamagome yamiti yanayooza haraka hasa katikamazingira yenyemvua nyingi.

Watu waliandika juu ya miamba,vigae vya mwandiko wa kikabari,bao zanta,kitambaa, ubaoni aumabati yametali mbalimbali.Mainka waPeru walitumia mwandiko wa mafundo kwenyekamba.

Kati ya mata zote za kutunza maandishi ni hasakaratasi inayotumiwa zaidi leo. Ilibuniwa China ilipojulikana mnamo mwaka100BK na kusambaa polepolebaraniAsia halafuUlaya.

Siki hizi maandishi yaelektroniki yamesambaa pamoja na matumizi yatarakilishi namtandao.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo yalugha bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuMaandishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Maandishi&oldid=1399107"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp