Lupus, kitaalamu hujulikana kamasystemic lupus erythematosus (kifupi:SLE), ni ugonjwa wa autoimmune, ambapomfumo wa kingamwili hushambulia kimakosa tishu zenye afya katika sehemu nyingi za mwili.[1] Dalili zake hutofautiana kati ya watu na zinaweza kuwa chini hadi kali sana.[1] Dalili zake za kawaida ni pamoja na maumivu na kuvimba kwa viungo,homa, maumivu ya kifua,kupoteza nywele,vidonda vya mdomo,kuvimba kwa nodi za limfu,kuhisi uchovu naupele mwekundu ambao mara nyingi hupatikana kwenye uso.[1] Mara nyingi kuna vipindi vya ugonjwa huu kuwa mkali (flares), na vipindi vya kupokuwepo dalili zake (remission) ambapo kuna dalili chache tu.[1]
Ugonjwa huu hauna tiba, na matibabu yake yanaweza kujumuisha dawa zisizo za steroidi (NSAIDs), kortikosteroidi (corticosteroids),dawa za kuzuia mfumo wa kinga (immunosuppressants), hidroksiklorokwini (hydroxychloroquine) na methotrexate.[1] Ingawa kortikosteroidi (corticosteroids) hufanya kazi vizuri kwa haraka, matumizi yake ya muda mrefu husababisha madhara.[5] Dawa mbadala haijaonyeshwa kuathiri ugonjwa huu.[1] Umri wa kuishi ni mdogo kati ya watu wenye SLE.[6] SLE huongeza kwa kiasi kikubwa hatari yaugonjwa wa moyo na mishipa, na hii ikiwa sababu ya kawaida ya kifo.[4] Kwa matibabu ya kisasa, karibu 80% ya walioathiriwa wanaishi zaidi ya miaka 15.[3] Wanawake walio na lupus wana mimba ambazo ni hatari zaidi lakini nyingi zake hufanikiwa.[1]
Kiwango cha SLE hutofautiana kati ya nchi kutoka 20 hadi 70 kwa kila 100,000.[2] Wanawake wa umri wa kuzaa huathirika mara tisa mara nyingi zaidi kuliko wanaume.[4] Ingawa kwa kawaida huanza kati ya umri wa miaka 15 na 45, aina mbalimbali za umri zinaweza kuathirika.[1][2] Wale wenye asiliya Kiafrika,Karibea, na Wachina wako katika hatari zaidi kuliko watu weupe.[4][2] Viwango vya magonjwa katika nchi zinazoendelea havijulikani wazi.[7] Lupus ni neno la Kilatini linalomaanisha "mbwa mwitu": ugonjwa huu ulipewa jina hili katika karne ya 13, kwani upele huu ulifikiriwa kwamba una mwonekano kama ule wa kuumwa na mbwa mwitu.[8]