Lordi nibendi yamuziki wahard rock/heavy metal kutoka mjiniHelsinki,Finland. Wazo la kubuni jina la Lordi lilitolewa mnamo mwaka wa 1992, ingawa bendi ilikuwa haijaanzishwa hadi ilipokuja kuanzishwa rasmi mnamo mwaka wa 1996 naTomi Putaansuu (maarufu kama "Mr. Lordi")[1] waRovaniemi, Finland.
Wanachama wa Lordi wanaeleweka kwa jinsi wanavyojieleza kwa mavazi ya mijitu ya kutisha wakati wanapofanya maonyesho yao au hatavideo zao. Hivyo Lordi hujulikana pia kwa jina la "The Finnish Monsters" na "The Monsters of Finland".
Mwanzoni mwa miaka ya 1990, Putaansuu alikuwa akicheza katika bendi ndogo ya mjini Rovaniemi. Aliondoka bendini kwa kufuatia wanachama wengine wa katika bendi hawakubaliana na uanzishaji wa muziki wakiwa ukumbini hasa kwa kuingiliana na vipengele vya staili ya bendi ya KISS. Putaansuu akaanza kutengeneza muziki wa demo chini ya jina la Lordi kunako mwaka wa 1991 na kuendelea kufanya hivyo kwa miaka kadhaa ya usoni. Mnamo mwaka wa 1995 ametengeneza wimbo wa "Inferno" na muziki wa video kwa ajili mradi fulani wa shule. Video haikutolewa kwa kufuatia Putaansuu hakuvaa kinyago kwenye video hiyo ndiyo sababu iliyopelekea video isitolewe.
Baada ya "Inferno", Putaansuu akaota. Katika ndoto hiyo, ilimwonyesha yeye akiwa akiwa kwenye onyesho na kuna kiunzi cha mifupa kinacheza juu ya jukwaa. Alipoamka, akaelewa kwamba Lordi inapaswa kuwa bendi ya muziki waHeavy metal iliojawa na vizuka. Lile jitu la kutisha alioiona kwenye ndoto hatimaye akaja kuwa mpiga gita wao Kalma.
Makala hii kuhusu muziki wa Ulaya bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuLordi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.