Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Lithi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Lithi
(Lithium)
Jina la ElementiLithi
(Lithium)
AlamaLi
Namba atomia3
Mfululizo safuMetali alikali
Uzani atomia6.941
Valensi1
Densiti0.534
Ugumu (Mohs)0.6
Kiwango cha kuyeyuka453.69K (180.54°C)
Kiwango cha kuchemka1615 K (1342 °C)
Asilimia zaganda la dunia0.006 %
Hali maadaimara

Lithi nielementi nametali alikali yenyenamba atomia 3 nauzani atomia 6.941 kwenyemfumo radidia.Alama yake niLi.Jina linatokana naKigiriki λίθοςlíthos "mwamba, jiwe" kwa sababu iligunduliwa mara ya kwanza ndani yamiamba.

Lithi ni elementi nyepesi kabisa kati ya elementi zote zilizo imara kwa hali ya kawaida. Inamenyuka haraka namaji, hivyo husababishamajeraha ikiguswa kwamkono kwa sababu mmenyuko wake naunyevu wangozi.

Kwaasili haipatikani kamadutu sahili kwa sababu inamenyuka harakakikemia lakini iko kwakampaundi mbalimbali, hasa katika miamba yaitale. Lithi tupu inapatikana kwa njia ya kikemia na inaonekana kamametali nyepesi yenyeranginyeupe-kifedha lakini haibaki hivyo kwamuda mrefu. Katikahewa yenye unyevu uso wake huwa haraka ganda lahidroksidi ya lithi yenye rangi yakijivu. Kwenye hewa kavu uso huwanitriti ya lithi yenye rangikahawia. Kwa sababu ya mimenyuko hiyo ya haraka lithi ya kimetali hutunzwa ndani yamafuta.

Lithi

Matumizi yake ni ndani yabetri na katikadawa mbalimbali. Betri za kisasa zinazotumiwa katikasimu za mkononi karibu zote zinatumia lithi. Mipango ya kutengenezamagari ya umeme inategemea betri za lithi na hivyo imetabiriwa ya kwambabei yake itapanda.

Isotopi

[hariri |hariri chanzo]

Kunaisotopi 5 za lithi zenyeneutroni 2, 3, 4, 5 na 6 kwenyekiini atomia. Isotopi ya kawaida ni3Li7 ambayo ni 92.58% ya lithi yoteduniani. Nyingine ni3Li6 yenye 7.42 % ya lithi yote. Nyingine zinapatikana kidogokidogo tu.

Picha

[hariri |hariri chanzo]
  • Betri ya lithi
    Betri ya lithi
  • Lithi ya kimetali katika mafuta
    Lithi ya kimetali katika mafuta
  • Moto unabadilishwa rangi na lithi
    Moto unabadilishwa rangi na lithi
Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuLithi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Lithi&oldid=1182436"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp