Litania
Zana
Kijumla
Chapa/peleka nje
Miradi mingine
Litania ni aina yasala yaUkristo ambayo upekee wake ni kuwa na mfululizo wa maneno ya sifa na maombi ambayo yanaitikiwa na mkusanyiko kwa namna iliyopangwa, kwa kawaida ya kujirudiarudia.
Jina linatokana na neno laKigirikiλιτανεία (litaneía), linalotokana naλιτή (litê), yaani "dua".
Mtindo huo wa kusali ulistawi kuanziaAntiokia ukaenea kwanza Mashariki halafu Mashariki hasa katikakarne IV.
Mfano wa litania fupi katikaliturujia niMwanakondoo wa Mungu inayotumika katikaMisa, na litania ndefu nilitania ya watakatifu inayotumika katika ibada muhimu kadhaa, kama vileupadrisho.