Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Lesotho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muso oa Lesotho
Ufalme wa Lesotho
Bendera ya LesothoNembo ya Lesotho
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: Khotso, Pula, Nala
(kwaKisotho: Amani, Mvua, Ustawi)
Wimbo wa taifa:Lesotho Fatse La Bontata Rona: Lesotho, nchi ya babu zangu
Lokeshen ya Lesotho
Mji mkuuMaseru
29°18 S 27°28 E
Mji mkubwa nchiniMaseru
Lugha rasmiKisotho,Kiingereza
Serikali
Letsie III
Moeketsi Majoro
Independence
kutokaWiingereza
4 Oktoba1966
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
30,355 km² (140th)
Negligible
Idadi ya watu
 -Julai 2009 kadirio
 -2004 sensa
 - Msongamano wa watu
 
2,067,0001 (144)
2,031,348
68.1/km² (138)
FedhaMaloti (LSL)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+2)
(UTC)
Intaneti TLD.ls
Kodi ya simu+266

-


Malealea,mandhari ya Lesotho

Ufalme wa Lesotho, auLesotho, ninchi ndogo inayozungukwa naAfrika Kusini pande zote. Hainapwani kwenyebahari yoyote.

Jina Lesotho lamaanisha eneo laBasotho (wakazi 99.7%), watu ambao wanaongealugha yaKisotho, ambayo nilugha rasmi pamoja naKiingereza. Wakati waukoloni ilijulikana kamaBasutoland.

Sasa ni nchi mwanachama waUmoja wa Mataifa.

Ina wakazimilioni 2 hivi.

Mji mkuu niMaseru.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]
Theluji kwenyebarabara ya Lesotho

Ukweli wakijiografia ambao wajulikana zaidi kuhusu Lesotho ni kwamba ni nchi inayozungukwa naAfrika ya Kusini, na ninchi huru pekee duniani ambayo yote iko juu yamita 1,000 juu ya usawa wa bahari (UB) (ft 3,281). Eneo la chini zaidi liko mita 1,400 (futi 4,593), na zaidi yaasilimia 80 za nchi ziko juu ya mita 1,800 (futi 5,906).

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza huaminiwa kuwawawindaji wa jamii yaWasani.

Katikakarne za kwanzaBK walifikawahamiajiWabantu wenyeujuzi wakilimo nauhunzi.

Lesotho ya sasa ilianza kupatikana mwaka1822 chini yachifuMoshoeshoe I aliyeungana na makabila mengine dhidi yaShaka Zulu (1818-1828).

Baadaye nchi iliathiriwa na mahusiano naWaingereza naMakaburu wa .Koloni la Rasi (leoAfrika Kusini), yakiwemo mapigano ya mara kwa mara.

Wamisionari walioalikwa na Mfalme Moshoeshoe I walianza kuandika na kuchapa kwalugha yaKisotho kati ya miaka1837 na1855.

Mwaka1867 nchi ikawa chini yamalkia waUingereza kwa jina laBasutoland lakini mwaka1869, Waingereza waliwaachia Makaburu nusu ya eneo la Basutoland.

Uhuru ulipatikana tena mwaka1966, na nchi ikaitwaufalme wa Lesotho.

Wilaya

[hariri |hariri chanzo]
Wilaya.

Kwa usimamizi wa serikali, Lesotho imegawiwa katikawilaya 10, kila moja ikiongozwa naKarani wa wilaya.

Kila wilaya inamji unaoitwamji wa kambi (camptown).

Watu

[hariri |hariri chanzo]
Nyumba nchini Lesotho

Wakazi kwaasilimia 90 niWakristo, wakigawanyika karibu sawa kati yaWakatoliki naWaprotestanti wamadhehebu mbalimbali.

Utamaduni

[hariri |hariri chanzo]
Mto Makhaleng, mabonde kwa milima ya Lesotho
Malealea, magharibi mwa Lesotho
Bonde nchini Lesotho

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Uchambuzi

[hariri |hariri chanzo]


Nchi zaAfrikaBara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) |Afrika Kusini |Algeria |Angola |Benin |Botswana |Burkina Faso |Burundi |Cabo Verde |Chad |Cote d'Ivoire |Eritrea |Eswatini |Ethiopia |Gabon |Gambia |Ghana |Guinea |Guinea Bisau |Guinea ya Ikweta |Jibuti |Kamerun |Kenya |Komori |Kongo (Jamhuri ya) |Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) |Lesotho |Liberia |Libya |Madagaska |Malawi |Mali |Misri |Morisi (Visiwa vya) |Mauritania |Moroko |Msumbiji |Namibia |Niger |Nigeria |Rwanda |Sahara ya Magharibi |Sao Tome na Principe |Senegal |Shelisheli |Sierra Leone |Somalia |Sudan |Sudan Kusini |Tanzania |Togo |Tunisia |Uganda |Zambia |Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje yaAfrika
Hispania:Kanari·Ceuta·Melilla |Italia:Pantelleria·Pelagie |Ufaransa:Mayotte·Réunion |Uingereza:·St. Helena·Diego Garcia |Ureno:Madeira
Makala hii kuhusu maeneo yaAfrika bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuLesotho kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Lesotho&oldid=1418725"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp