Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Laurent Kabila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Laurent Kabila

Amezaliwa27 Novemba 1939
Baudouinville
Amekufa18 Januari 2001
Nchikongo
Cheorahisi

Laurent-Désiré Kabila (27 Novemba193918 Januari2001) alikuwarais wa tatu waJamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Mei 1997 hadi kuuawa kwake tarehe 18 Januari 2001. Alifuatwa na mwanaweJoseph Kabila.

Kabila alifikaikulu kwakumpinduaMobutu Sese Seko.

Asili ya Kiluba

[hariri |hariri chanzo]

Alizaliwa katikafamilia yaWaluba huko Baudouinville (sasaMoba) karibu na Albertville (Kalemie) kando yaZiwa Tanganyika. Alisoma hukoUjerumani ya Mashariki naParis akarudi Kongo baada yauhuru wa nchi alipojiunga na umoja wa vijana wachama chaPatrice Lumumba.

Mwanaharakati wa Lumumba

[hariri |hariri chanzo]

Baada ya kuuawa kwa Lumumba alijiunga nakundi la wafuasi wamarehemu akaingia katikaupinzani wakijeshi dhidi yaserikali yaJoseph Desiree Mobutu. Majaribio hayo yalikandamizwa na jeshi la serikali. Kabila alikuwa kati yaviongozi wachache walioendelea na upinzani.

Kiongozi wa vita ya msituni

[hariri |hariri chanzo]

Alikuwa na usaidizi wa siri wa raisJulius Nyerere waTanzania na kwa miezi michache katika1965MkubaChe Guevara alijiunga na kundi la Kabila lakini kufuatana nakumbukumbu za Guevara hawakuelewana wala kufanikiwa.

Kuanziamwaka1967 aliungana na kundi dogo la Parti de la Revolution Populaire (PRP) akaongoza jeshi la Forces Armees Populaires (FAP) lililokuwa na makambi Tanzania naZambia lakini aliweza pia kutawala eneo dogo katikamilima ya Fizi yamkoa wa Kivu hadi1977 alipokufuzwa na jeshi la serikali ya Mobutu.

Baadaye aliishiUganda na Tanzania asionekane tena Kongo. Hakushiriki katika uasi wa wananchi dhidi ya serikali ya Mobutu na jitihada ya kuongezademokrasia nchini.

Kurudi kwa msaada wa Rwanda

[hariri |hariri chanzo]

Alirudi nchini mwaka1996 wakati wauvamizi wa Kongo yaMashariki yawanamgamboWahutu kutokaRwanda. Mabaki ya jeshi la Kihutu kutoka Rwanda walikuwa wamekimbilia Kongo mwaka1994 baada yamauaji ya kizazi ya Rwanda na sasa walishambulia Wabanyamulenge waliokuwaWatutsi wa Kongo. Serikali ya Rwanda ilitafuta njia ya kumaliza wanamgambo hao kwa sababu walikuwa tishio kwa utaratibu mpya wa Rwanda. Hapo walikuwa tayari kusaidia kujenga vikosi vya Wakongo wa kupambana na Wahutu katika Kongo.

Kabila aliunda maungano ya "Alliance des Forces Democratiques pour la Liberation du Congo-Zaire (AFDL)" akapokeasilaha na washauri kutoka jeshi la Rwanda.

Katikamuda mfupi Kabila aliweza kujipatia sifa kama kiongozi mwenye uwezo wa kushindana na jeshi la Mobutu aliyejua namna ya kufanya maazimio yake hata bila washauri wake Wanyarwanda aliowategemea bado.

Mshindi dhidi ya Mobutu

[hariri |hariri chanzo]

Vikosi vya Kabila vilisogea mbele haraka dhidi ya jeshi la Mobutu lisilokuwa tayari tena kupigana naadui aliyejuakazi yavita. Kabila alianza vita katika Oktoba 1996 huko Kivu akatekaBukavu mnamoOktoba mwaka uleule,Kisangani katika Machi 1997 naLubumbashi mwezi wa Aprili. Mwezi Mei jeshi lake likaingiaKinshasa na wakubwa wa Mobutu walikimbiaBrazzaville. Tarehe 17 Mei Kabila alijitangaza kuwa rais mpya akabadilisha tena jina la nchi kuwa Kongo.

Kabila alikuwa na tatizo la kutokuwa na uhusiano na watu wa Kinshasa ambao wengi walimwona kama mgeni.Askari zake wengi waliwasiliana kwaKiswahili naKiingereza aulugha za Kongo mashariki, hawakujuaKifaransa wala lugha za Kongo magharibi. Baada ya kushika serikali Kabila alijaribu kupunguza umuhimu wa washauri wake Wanyarwanda.

Rais wa kuona upinzani

[hariri |hariri chanzo]

Hii ilisababisha matatizo na uhusiano ulikuwa mbaya. Wananchi wa Kinshasa wengi hawakuona mabadiliko mengi katikamaisha yao. Kabila hakuongezahaki za kidemokrasia wala kushirikiana nawanasiasa waliokuwa wapinzani wa Mobutu katika miaka ya kutafuta demokrasia nchini.

Upinzani dhidi ya Kabila ikakua katika sehemu za nchi. Hatimaye mwaka 2001 aliuawa na askari waulinzi wake kwa namna isiyoeleweka vizuri hadi leo. Hapo wakuu wa jeshi walimtangazamwana wakeJoseph kuwamwandamizi wake.

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Laurent_Kabila&oldid=1389315"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp