Nahau ya Kilatini ("Kukosa ni jambo la kibinadamu").
Kilatini(Lingua Latinala) ni lugha ya kale yaKihindi-Kiulaya ambayo ilizungumzwa katikaDola la Roma. Ilianza kama lugha ya eneo la Lazio nchiniItalia na baadaye ikawa lugha kuu ya utawala waKirumi, ikienea koteUlaya kupitia upanuzi waDola la Roma. Ingawa haizungumzwi tena kama lugha ya asili, Kilatini bado hutumika katika taasisi za kidini, sayansi, sheria, na elimu ya juu, hasa katika Mji wa Vatikani na taasisi za kitaaluma. Lugha za Kirumi kamaKihispania,Kifaransa,Kiitaliano,Kireno, naKiromania zilichipuka kutoka Kilatini cha Kawaida (Vulgar Latin), ambacho kilitumiwa na watu wa kawaida katika Milki ya Roma
Kiswahili kimerithimaneno yenyeasili ya Kilatini hasa kupitiaKiingereza kilichopokea karibuasilimiahamsini ya maneno yake yote kutoka Kilatini kupitia hasa Kifaransa. Maneno mengine ya Kilatini yameingia Kiswahili kupitia Kireno, Kifaransa n.k.
Kilatini kilikuwa na upanuzi mkubwa kuanziakarne ya 16; misingi ya sayansi ya kisasa ilijadiliwa katikaUlaya kwa Kilatini kilichokuwa lugha ya vyuo vikuu kote Ulaya. Katikakarne ya 18 na19mataifa mengi yaliimarisha lugha zao na kuzitumia kwa ngazi zote za elimu. Lakiniwataalamu wa Ulaya naMarekani waliendelea kutumia majina ya Kilatini kwa kutaja habari za kisayansi na kubuni majina mapya kufuatana na kanuni za Kilatini kwa kutaja vitu na viumbe vilivyotambuliwa na kuelezwa kisayansi. Kazi hii iliendelea hata wakati matumizi ya Kilatini kama lugha ya kujadiliana yalishafikia mwisho wake.
Katikakarne ya 20 kulikuwa na harakati ya wapenzi wa lugha kuundamisamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa,mtandao n.k.Wikipedia ya Kilatini ilifikia makala zaidi ya 130,000 kwenye mwaka2019.
Makala hii kuhusu mambo yalugha bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuKilatini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.