Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kuwait

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
دولة الكويت
Dawlat al Kuwayt

Kuwait
Bendera ya KuwaitNembo ya Kuwait
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa:(hakuna)
Wimbo wa taifa:watani alkuwait وطني الكويت سلمت للمجد
(Taifa langu la Kuwait)
Lokeshen ya Kuwait
Mji mkuuJiji la Kuwait
29°22 N 47°58 E
Mji mkubwa nchiniSalmiya
Lugha rasmiKiarabu
SerikaliUfalme wa kikatiba
Mishal Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah
Mohammad Sabah Al-Salem Al-Sabah
Uhuru
kutokaUingereza
19 Juni1961
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
17,820 km² (ya 157)
--
Idadi ya watu
 -2014 kadirio
 -2005 sensa
 - Msongamano wa watu
 
4,044,5002 (140)
2,213,403
200.2/km² (ya 68)
FedhaKuwaiti Dinar (KWD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+3)
(UTC+3)
Intaneti TLD.kw
Kodi ya simu+965

-


Ramani ya Kuwait
Kuwait inavyoonekana kutokaangani (2001)
Jiji la Kuwait

Kuwait (kwaKiarabu: الكويت ‎) ni nchi ndogo yaUarabuni kwenyeGhuba ya Uajemi.

Imepakana naIrak naSaudia.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Karibu nchi yote nijangwa, lakini kunapwani navisiwa vidogo.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Historia ya Kuwait ilianza kamautemi mdogo chini yafamilia ya Al-Sabah iliyokuwa chini yaSultani wa Uturuki aliyetawala nchi jirani ya Irak hadivita kuu ya kwanza ya dunia.

Tangu kuingia kwaWaingereza katika nchi za ghuba, mwaka1899watawala wa Kuwait walijiweka chini yaulinzi waUingereza kwa sababu waliuona afadhali kuliko ukuu wa Uturuki.

Waingereza walitetea hali yake ya pekee dhidi yaWaosmani na baadaye dhidi ya Saudia.

Baada ya kuporomoka wadola la Uturuki Kuwait iliendelea kamanchi lindwa chini ya Uingereza hadi kupatauhuru wake tarehe19 Juni1961.

Katika miaka iliyofuata Kuwait iliona madai yaIrak ya kuwa tangu zamani Kuwait nimkoa wake uliotengwa naukoloni.

Tarehe2 Agosti1990dikteta waIrakSaddam Hussein alivamia Kuwait na kuiteka. Katikavita ya pili ya ghuba Marekani pamoja na nchi nyingine ilishambuliajeshi la Irak katika Kuwait na kurudisha serikali yaEmir al Sabah.

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Kati ya wakazi 4,044,500asilimia 30 pekee ni wananchi au Wakuwait wenyewe. Wengine wote ni watu waliokuja kufanya kazi na kuishi hapo. Pamoja na wahamiaji kutoka nchi jirani, 60% ya wakazi niWaarabu. Zaidi ya 30% tena wana asili yaIndia au nchi nyingine zaAsia.Waafrika ni 76,698.

Lugha rasmi ni Kiarabu; wananchi wanakiongea kwalahaja maalumu. Kiingereza pia kinatumika hasa, hasa katikabiashara.

Upande wadini, wananchi karibu wote niWaislamu, hasaWasuni (70%), lakini piaWashia (30%). Ndiyodini rasmi.Wakristo ni zaidi ya 10%, lakini karibu wote ni wahamiaji.Wahindu kutoka India ni wengi zaidi kidogo (karibu 15%).Wabuddha ni 2%.

Uchumi

[hariri |hariri chanzo]

Nchi nitajiri kutokana na wingi wamafuta ya petroli yaliyopo chini ya ardhi yake. Akiba zake ni kama 10% za akiba zadunia yote. Kabla ya kupatikana kwa mafuta mwaka1938 nchi ilikuwamaskini lakini sasa ni kati yanchi tajiri zaidi duniani.

Kabla ya kugunduliwa kwa mafuta palikuwa nakilimo kidogo sana, halafuufugaji na hasauvuvibaharini.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iran |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuKuwait kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kuwait&oldid=1315925"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp