Zamani vilihesabiwa kati ya mimea lakini lishe yao ni tofauti. Mimea inategeneza chakula chao au mata ogania inayohitaji kwa njia yauanisinuru yaani kwa njia ina lisheautotropia. Kuvu inatumia mata ogania iliyopo tayari sawa na wanyama hivyo lishe yake niheterotropia. Kuvu hutumia mabaki ya miili ya mimea na wanyama wengine na kuyatumia kama chakula chake.
Tofauti na wanyama wengi kuvu haitembei na muundo waseli zake ni tofauti; seli za wanyama huwa na ngozi ya nje bali seli za mimea na kuvu huwa na ukuta wa seli. Tena tofauti na mimea kuta za seli ni zachitini siselulosi jinsi ilivyo kwa mimea.
Hadi sasa kuna spishi 70,000 zinazojulikana na kuna makadirio ya kwamba jumla inaweza kupita milioni 1.
seli moja-moja kamahamira. Zinazaa hasa wa njia ya kujigawa.
miseli ambayo ni kama nyavu inayojengwa na nyuzi zakungunyanzi; hizi ni seli ndefu umbo la neli zinazoshikana na kuwa uzi ndefu. Inaonekana katika nyuzi nyeupe zianzoonekana katika chakula kinachoanza kuoza maana yake kuoza kwa mkate nis awa na fungu kukua ndani yake. Zinazaa zaidi kwa njia yaspora zinazofanana nambegu za mimea.
Kuvu ni jumla ya kungunyanzi zote na jumla hii huitwa miseli. Miseli ya aina hii inaweza kuenea mbali sana ikikua ndani ya ardhi kwa mfano msituni inayopata lishe kutoka kwa majani, matawi na mashina yaliyoanguka chini. Kama kiumbehai miseli haina umbo maalumu lakini kuna mifano ya miseli moja iliyoenea hektari zaidi ya 30 na kushi miaka 1,000 angalau.
Kwa aina kadhaa miseli inajenga sehemu za pekee zinazotoka kamauyoga. Uyoga si kuvu mwenyewe bali kitu kama tunda lake. Unajengwa na nyuzi nyingi za kungunyanzi na kuwa mahali pa kukuza spora ambavyo ni kama mbegu za kuvu.
Kuvu ni muhimu katika ekolojia ya viumbehai huwa na athira kubwa.
Zikitumia mata ogania ya viumbe vingine kazi yao ni kuvunja miili ya mimea na wanyama. Ni kuvu pekee zinazoweza kuvunja mata ya ubao na kuipasua katika kemikali zake. Pamoja nabakteria na wanyama wadogo hutengeneza ardhi yenye rutba.
Kuvu zinashirikiana na mimea. Takriban asilimia 80-90 za mimea yote zina kuvu kwenye mizizi yao. Hapa inaishi pamoja katika simbiosi aumtoshelezano. Maana yake nyuzi za kungunyanzi za kuvu inaingia ndani ya ardhi kushinda mizizi midogo ya mmea. Hivyo kuvu inasaidia kupata madini na mata ya lishe kutoka ardhi kuchinda mmea mwenyewe. Usaidizi huu unaonekana hsasa kwa mazao kwenye ardhi isiyo na rutba nzuri sana; kuvu huboresha lishe ya mimea. Kwa upande mwingine kuvu inavutahidrati kabonia kutoka mzizi zinazojengwa na mmea kwa njia yausanisinuru.
Uyoga ya champignon hulimwa kibiashara kama chakula ni tunda la miseli
Kuvu hutoa pia madawa na sumu. Chakula kinachooza mara nyingu huwa na miseli ambayo ni sumu kwa wanadamu. Hata sehemu za uyoga ni sumu kali. Kinyume chake aina nyingine za uyoga ni chakula bora kwa sababu ni chanzo chaprotini nzuri.
Kuvu mbalimbali zimetumiwa kwa kutoa madawa ya kutibu magonjwa. Dawa lapenicillin linapatikana kutoka kwa kuvu pamoja madawa mengine yakiuavija (antibiotic). Zinatoa pia madawa ya kuzuia mbu.
Kuvu zinatokea pia kwenye mwili kama magonjwa. Kuvu inaanza kukua kwenye sehemu za ngozi kama mwili unakosakinga (tiba). Inatokea hasa mguuni na kujulikana kwa jina lanyungunyungu aumamunyumunyu; kama mguu hausafishwi mara kwa mara inaonekana kama vidonda kati ya vidole.
Ugonjwa mgumu zaidi ni kukua kwa kuvu kwenye ngozi za utumbo. Wakinamama huathiriwa mara nyingi na kuvu ndani ya uke.
Kuvu pia humea kwenyekuta,dari na mapaa yamajengo hasa yaghorofa. Ukuta unapolowamaji nahewa kuwa naunyevu wa juu kuvu hukua na kuenea si tu kwa kuta bali pia kwafenicha. Kuvu inapoenea huhariburangi ya kuta na huacha kuta zikiwa zimechakaa.
Makala hii kuhusu mambo yabiolojia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuKuvu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.