Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kupro

Majiranukta:35°N33°E /35°N 33°E /35; 33
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Κυπριακή Δημοκρατία(Kigiriki)
Kypriakí Dhimokratía
Kıbrıs Cumhuriyeti(Kituruki)

Jamhuri ya Kupro
Bendera ya KuproNembo ya Kupro
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: none
Wimbo wa taifa: Ύμνος εις την Ελευθερίαν
imnos is tin eleftherian
Utenzi wa uhuru1
Lokeshen ya Kupro
Mji mkuuNikosia
35°08 N 33°28 E
Mji mkubwa nchiniNikosia
Lugha rasmiKigiriki,Kituruki
SerikaliJamhuri
Nicos Christodoulides
Uhuru
Tarehe
16 Agosti1960
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
9,251 km² (ya 162)
9
Idadi ya watu
 -2021 kadirio
 -2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
1,244,188 (ya 158)
838,897
123.4/km² (ya 82)
FedhaCyprus Pound (CYP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD.cy3
Kodi ya simu+357

-

1 Sawa na wimbo la taifa laUgiriki


Ramani ya Kupro

Kupro, rasmi kamaJamhuri ya Kupro, nikisiwa kilichoko katikaBahari ya Mediterania, mashariki mwaUgiriki na kusini mwaUturuki. Inapakana kwa karibu na nchi kamaSyria,Lebanon,Israeli, naMisri kupitiabahari. Kupro ina idadi ya watu takriban milioni 1.2, na ni miongoni mwa nchi ndogo kwa ukubwa wa idadi ya watu baraniUlaya. Mji wake mkuu na jiji kubwa zaidi niNicosia. Nchi hii imegawanyika katika sehemu mbili kuu – eneo la Kusini linalotawaliwa na Jamhuri ya Kupro na eneo la Kaskazini linalojitawala na kujulikana kama Jamhuri ya Kupro ya Kaskazini, ambayo inatambuliwa rasmi na Uturuki pekee. Kupro ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu mwaka 2004.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Kisiwa cha shaba

[hariri |hariri chanzo]

Watu waliishi huko walau kuanziamilenia ya 10 KK.

Zamani za Kale kisiwa kilikuwa chanzo chashaba nyingi iliyopatikana katika eneo la Mediteranea ya mashariki.Jina la kikemia la shaba "kupri" linatokana na jina la kisiwa hicho.

Katika Biblia

[hariri |hariri chanzo]

Kisiwa kinazungumziwa naBiblia ya Kikristo, kwa namna ya pekee kuhusiana naumisionari waMtume Barnaba na wenzieMtume Paulo naMarko Mwinjili kisiwani huko.

Kuanziamwaka649 Kupro ilishambuliwa na pengine kutawaliwa naWaarabu walioua wakazi wengi na kubomoamakanisa namiji mizima.

Chini ya Waosmani

[hariri |hariri chanzo]

Baada yaWakristo kujirudishia kisiwa hicho muhimu,WaturukiWaosmani walikiteka mwaka1570 na kuingizaUislamu bila kufaulu kufutadini ya awali.

Chini ya Waingereza

[hariri |hariri chanzo]

Mwaka1878Uingereza ulianza kutawala Kupro bila kuitenga rasmi naDola la Waosmani hadi mwaka1914.

Tarehe16 Agosti1960 Kupro ilijipatiauhuru ingawa kulikuwa na utata kati ya kubaki peke yake, kuungana naUgiriki au kugawiwa kati yakaskazini (Waturuki) nakusini (Wagiriki).

Baada ya uhuru

[hariri |hariri chanzo]

Tanguvita vya Kupro, 1974kisiwa kimegawiwa, huku maeneo yakaskazini yakiwa yanatawaliwa naJamhuri ya Kituruki ya Cyprus ya Kaskazini isiyotambulika kimataifa.

Pamoja na hayo, Kupro imefaulu kujiunga naUmoja wa Ulaya tarehe1 Mei2004.

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Wakazi walio wengi hutumialugha yaKigiriki, wengineKituruki, ambazo zote mbili nilugha rasmi.

Kwa jumla hao wa kwanza niWakristo (72.3% za wakazi wote), wa pili niWaislamu (25%).

Wakristo karibu wote niWaorthodoksi; wengine niWakatoliki (2.9%, hasaWamaroni),Waprotestanti (2%) naWaarmenia.

Dini ina nafasi kubwa katikamaisha ya wananchi.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Government
Tourism
Official publications

35°N33°E /35°N 33°E /35; 33

Nchi zaUmoja wa UlayaBendera ya Umoja wa Ulaya
Austria |Bulgaria |Eire |Estonia |Hispania |Hungaria |Italia |Kroatia |Kupro |Latvia |Lituanya |Luxemburg |Malta |Polandi |Slovakia |Slovenia |Romania |Ubelgiji |Ucheki |Udeni |Ufaransa |Ufini |Ugiriki |Uholanzi |Ujerumani |Ureno |Uswidi
Nchi huru
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
1 nchi yaAsia ya Magharibi kijiografia ambayo huhesabiwa kuwa sehemu yaUlaya kiutamaduni2nchi ya kimabara
Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iran |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Safari ya kwanza
Safari ya pili
Safari ya tatu
Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuKupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuKupro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kupro&oldid=1427662"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp