Obstructed labour | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Obstetrics and gynaecology ![]() |
DiseasesDB | 4025 |
eMedicine | med/3280 |
MeSH | D004420 |
Kukwama kwa leba, hali ambayo pia hujulikana kamadistosia ya leba, ni wakati ambapo, hata ikiwauterasi ina mikazo ya kawaida, mtoto hatoki kupitia pelvisi wakati wakuzaliwa kwa sababu ya kufungika.[1] Kutatizika kwa mtoto hujumuishaukosefu wa oksijeni ya kutosha hali inayoweza kusababisha kifo. Hali hii huongeza hatari kwa mama ya kupatamaambukizi,kupasuka kwa uterasi, au [[kuvuja damu baada ya kuzaa].[2] Matatizo ya muda mrefu ya mama yanajumuishafistula ya uzazi. Kukwama kwa leba huaminika kusababishaleba ya muda mrefu, wakati awamu tendeti ya leba inapozaidi saa kumi na mbili.[1]
Visababisishi vikuu vya kukwama kwa leba hujumuisha: mtoto mkubwa zaidi au aliyelala kwa namna mbaya tumboni,pelvisi ndogo, na matatizo katika njia ya uzazi. Hali za kulala tumboni zisizo za kawaida hujumuishadistosia ya bega ambapo bega la upande wa juu halipitii chini yafupa la uzazi kwa urahisi.[1] Vipengele vya hatari vya pelvisi ndogo hujumuishautapiamlo na ukosefu wa miale ya jua hivyo kusababishaukosefu wa vitamini D.[3] Hali hii hutokea mara nyingi katikaubaleghe kwa sababu mara nyingi pelvisi huwa haijakamilika kukua.[2] Matatizo kwenye njia ya uzazi hujumuisha uke na msamba mwembamba, hali inayoweza kusababishwa naukekektaji autyuma.[1]Patografu mara nyingi hutumika kufuatilia jinsi leba inavyoendelea na kutambua matatizo.[2] Hii, pamoja na uchunguzi wa kimwili unaweza kutambua leba iliyokwama.[4]
Matibabu ya leba yanaweza kuhitajikuzaa kwa njia ya upasuaji aukuvuta vipande vilivyobakia na hata piaupasuaji wa kufungua simfisisi ya uzazi. Hatua nyingine hujumuisha: kuhakikisha mwili wa mwanamke una maji ya kutosha naantibiotiki ikiwatando zilipasuka zaidi ya saa 18 zilizopita.[5] Barani Afrika na Asia, kukwama kwa leba hutokea kwa wanawake wawili hadi watano wanaozaa.[6] Mwaka wa 2013, hali hii ilisababisha vifo 19,000 tofauti na vifo 29,000 mwaka wa 1990 (takriban 8% ya visa vyote vyavifo vinavyohusiana na ujauzito).[7][1] Vifo vingi vinavyosababishwa na hali hii hutokea katikamataifa yanayoendelea.[2]
{{cite book}}
:|edition=
has extra text (help){{cite book}}
:|edition=
has extra text (help){{cite book}}
:|edition=
has extra text (help){{cite book}}
:|edition=
has extra text (help){{cite journal}}
:|first1=
has generic name (help)CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link)