Mnamo mwaka wa 2015, walizaliwa watoto wapatao milioni 135 ulimwenguni.[2] Takriban milioni 15 walizaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito,[3] huku kati ya asilimia 3 na 12 walizaliwa baada ya wiki 42.[4] Katika ulimwengu ulioendelea, kuzaa kwingi hutokea hospitalini,[5][6] wakati katikaulimwengu unaoendelea kuzaa kwingi hufanyika nyumbani kwa usaidizi wamkunga.[7]
Njia ya kawaida ni kuzaa kupitia uke.[8] Inahusisha hatua tatu za kuzaa: kufupisha na kufunguka kwa seviksi, kushuka na kuzaliwa kwa mtoto, na utoaji wa kondo la nyuma.[9] Hatua ya kwanza kwa kawaida huchukua saa 12 hadi 19, hatua ya pili dakika 20 hadi saa mbili, na hatua ya tatu dakika tano hadi 30.[10] Hatua ya kwanza huanza na maumivu makali ya tumbo au mgongo ambayo hudumu karibu nusu dakika na kutokea kila dakika 10 hadi 30. Maumivu haya huwa na nguvu na kutokea karibu karibu kwa pamoja kwa muda.[10] Wakati wa hatua ya pili, kusukuma kwa mikazo kunaweza kutokea.[10] Katika hatua ya tatu, kuchelewesha kushikilia kitovu kwa ujumla kunapendekezwa.[11] Mbinu kadhaa zinaweza kusaidia kwa maumivu, kama vile mbinu za kutuliza, afyuni, na kutiwa ganzi migongoni.[10]
Watoto wengi huzaliwa kuwa kutoa kichwa kwanza; hata hivyo takriban 4% huzaliwa kwa kutoa miguu au matako kwanza, inayojulikana kama chini kwanza badala ya kichwa kwanza.[10][12] Kwa kawaida, kichwa huingia kwenye pelvisi ikitazama upande mmoja, na kisha huzunguka kuelekea chini. Wakati wa leba, mwanamke anaweza kwa ujumla kula na kuzunguka apendavyo.[13] Hata hivyo, kusukuma haipendekezi wakati wa hatua ya kwanza au wakati wa kujifungua kwa kichwa, na kuingiza kioevu kwenye tupu ya nyuma hakupendekezwi.[13] Wakati kukata sehemu iliyo wazi kwenye uke, inayojulikana kama kukata sehemu ya kati ya uke na tupu ya nyuma kwa ujumla hakuhitajiki.[10] Mnamo mwaka wa 2012, karibu milioni 23 walijifungua kupitia upasuaji wa sehemu ya kati ya tumbo na uterasi.[14] Upasuaji wa sehemu ya kati ya tumbo na uterasi unaweza kupendekezwa kwamapacha, dalili za kufadhaika kwa mtoto, au ikiwa mtoto atatoa kwa miguu kabla ya kichwa.[10] Njia hii ya kujifungua inaweza kuchukua muda mrefu kupona.[10] Dozi moja ya antibiotiki, azithromycin, inaweza kutumika kuzuia maambukizi katikanchi za kipato cha chini na cha kati.[15]
↑"The World Factbook".www.cia.gov. Julai 11, 2016. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 16 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo30 Julai 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑10.010.110.210.310.410.510.610.7"Pregnancy Labor and Birth".Women's Health. Septemba 27, 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 28 Julai 2016. Iliwekwa mnamo31 Julai 2016.The first stage begins with the onset of labor and ends when the cervix is fully opened. It is the longest stage of labor, usually lasting about 12 to 19 hours .. The second stage involves pushing and delivery of your baby. It usually lasts 20 minutes to two hours.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑Tita, Alan T.N.; Carlo, Waldemar A.; McClure, Elizabeth M.; Mwenechanya, Musaku; Chomba, Elwyn; Hemingway-Foday, Jennifer J.; Kavi, Avinash; Metgud, Mrityunjay C.; Goudar, Shivaprasad S. (30 Machi 2023). "Azithromycin to Prevent Sepsis or Death in Women Planning a Vaginal Birth".New England Journal of Medicine.388 (13): 1161–1170.doi:10.1056/NEJMoa2212111.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
↑World Health Organization."Newborns: reducing mortality". World Health Organization. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 3 Aprili 2017. Iliwekwa mnamo1 Februari 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)