Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kucha wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kucha wa Afrika
Kikucha uso-mwekundu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Animalia (Wanyama)
Faila:Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila:Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli:Aves (Ndege)
Oda:Passeriformes (Ndege kamashomoro)
Familia ya juu:Sylvioidea (Ndege kamakucha)
Familia:Macrosphenidae (Ndege walio na mnasaba nakolojojo)
Wolters, 1983
Ngazi za chini

Jenasi 6, spishi 18:

Kucha wa Afrika nindege wadogo ambao zamani waliainishwa katikaSylviidae,familia yakucha wengine. Sasa wataalamu wanakubaliana kwamba ndege hawa ni kundi lao lenyewe pamoja navikucha nakolojojo. Kwa hivyo wamepata familia yaoMacrosphenidae. Kucha waAfrika bila vikucha na kolojojo wanafanana nashoro,kuchanyika nakuchamsitu ambao zamani waliainishwa pia katika familiaSylviidae. Wana mkia mrefu kiasi na rangi yao ni kahawia au kahawianyekundu. Wana michirizi mizito kujumuisha “masharubu”, isipokuwakucha wa Victorin. Vikucha na kolojojo wana mkia mfupi.

Hulawadudu ambao huwatafuta ardhini, chini ya uoto au katika gome lamiti. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika miti au ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyatagamayai 2-5.

Spishi za Afrika

[hariri |hariri chanzo]

Picha

[hariri |hariri chanzo]
  • Kuchamwamba wa Damara
    Kuchamwamba wa Damara
  • Kuchakulu
    Kuchakulu
  • Kucha-nyasi
    Kucha-nyasi
  • Kikucha kaskazi
    Kikucha kaskazi
  • Kikucha utosi-mwekundu
    Kikucha utosi-mwekundu
  • Kikucha domo-refu
    Kikucha domo-refu
  • Kikucha kijani
    Kikucha kijani
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kucha_wa_Afrika&oldid=1084514"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp