Makala hii ina vyanzo lakini havijapangiliwa kwa kufuata utaratibu wa uandishi wa Wikipedia
Makala (au sehemu ya makala hii) inatoa habari bila kuonesha vyanzo au uthibitisho wowote mahali husika. Ona namna ya kutaja vyanzo hapa:Wikipedia:Umaarufu naKutaja vyanzo. Ni lazima kuboresha makala hii kwa kuweka vyanzo/marejeo kwenye sehemu zake husika ili kuthibistisha habari zilizoandikwa na pia kuendana na sera za uandishi wa Wikipedia, la sivyo sehemu ya makala au yote kabisa inaweza kufutwa. Unaweza kuondoa kigezo hiki mara baada ya vyanzo sahihi kuwa vimeingizwa katika makala sehemu husika
-Kwa "kuba" (pia: kubba) kama sehemu ya jengo tazamaKuba (jengo)-
Kisiwa cha pili niIsla de la Juventud (Kisiwa cha Vijana) kilichoitwa Isla de Pinos (Kisiwa cha Misunobari) hadi mwaka1978. Kisiwa hiki kina eneo la km² 2,200. Kuba yote ina eneo la kilomita za mraba 110,860 pamoja na sehemu zabahari, nchi kavu peke yake ni km² 109,884.
Baada ya majadiliano marefu Kuba ilipatauhuru wake kuanzia mwaka1902 lakini ilipaswa kukubalimkataba uliotunzahaki ya Marekani kungilia kati mambo ya ndani na kuipa Marekani eneo kwa kituo cha kijeshi.
Hadi mwaka1934 Marekani iliingilia mara mbili nakupinduamarais wawili wa Kuba, ama kwa kutumajeshi lake au kwa kutumia wanajeshi wa Kuba. Eneo laGuantanamo Bay kusini mwa Kuba limebaki hadi leo kama kituo cha kijeshi cha Marekani.
Mkataba mpya kati ya Marekani na Kuba wa mwaka 1934 uliongeza haki za Kuba. Wakati huohuo uasi wa kijeshi ulimwingizasajentiFulgencio Batista kwenye uwanja wasiasa. Batista alijipandishacheo hadikanali akashikamamlaka yote ya kijeshi na kuteua marais waliotekeleza matakwa yake.
Mwaka1940 alichaguliwa mwenyewe kuwa rais, akarudi1952 kwa kugombea tena urais lakini, baada ya kuona angeshindwa, alipinduaserikali kwa njia ya uasi wa kijeshi akasimamishakatiba na kuwadikteta wa Kuba hadi mwaka1959. Chini ya serikali ya Batista ulajirushwa na athira ya kiuchumi ya makampuni ya Kimarekani viliongezwa. Ukali wa utawala na mauaji ya wapinzani wengi vilisababisha kutokea kwa vikundi vilivyokuwa tayari kupinga serikali ya dikteta kwasilaha.
Mwaka1956 Castro pamoja na Guevara na wafuasi 80 walivuka bahari kwajahazi "Granma" wakajificha katika milima ya Sierra Madre. Kutoka huko walianza kushambulia vikosi vya jeshi la Batista. Polepole idadi ya wapiganaji waliojiunga nao iliongezeka na wanajeshi wa serikali mara nyingi walihamia upande wa Castro. Tarehe1 Januari 1959 dikteta Batista alikimbia na kuondoka Kuba, vikosi wa wanamapinduzi waliingia Havana.
Mwanzoni Castro alionekana kama msemaji mkuu wa mapinduzi akimtangaza mwanasheriaManuel Urrutia kama rais mpya. Fidel alichukua cheo chawaziri mkuu katikaFebruari 1959. Hapo mwanzoni serikali mpya ilikuwa muungano wa wapinzani wa udikteta nawanamgambo kutoka milimani.Uchaguzi wavyama vingi ulitangazwa kama shabaha mojawapo ya kurudishademokrasia. Katika miezi iliyofuatawanasiasa wenye mwelekeo wa kati waliondolewa polepole na Castro aliongeza idadi yaWamarxisti katika vyeo vya juu.
Kuanzia1960 na baada ya jaribio la Marekani kumpindua Castro huyu aliongeza mwelekeo wake wakisoshalisti. Baada ya kupingwa na Marekani, Castro alitafutaushirikiano na usaidizi kutokaUrusi wakikomunisti.Castro alitangazasiasa ya kikomunisti akaendelea kutawala bilauchaguzi huru hadi alipojiuzulu mnamo Februari2008 kwa sababu zaafya. Baada yake aliongoza mdogo wake,Raul Castro, hadi mwaka2018Miguel Díaz-Canel alipochaguliwa kuwa rais wa nchi.
Wakazi wengi ni machotara. Vipimo vyaDNA vimeonyesha kwamba Wazungu wameichangia 72%, Waafrika 20% na Waindio 8%.Lugha rasmi na ya kawaida niKihispania. InafuataKrioli yaHaiti.
↑As shown on the obverse of the coins; see"this photo of a 1992 coin". Iliwekwa mnamo2006-09-26. Note that the Spanish word "Patria" is better translated into English as homeland, rather than "fatherland" or "motherland".
Alvarez, José (2001). "Rationed Products and Something Else: Food Availability and Distribution in 2000".Cuba in Transition, Volume11. Silver Spring,MD:ASCE. ku.305–322.ISBN0-9649082-0-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2014-09-07. Iliwekwa mnamo25 Machi 2013.{{cite book}}:External link in|chapterurl= (help);Invalid|ref=harv (help);Unknown parameter|chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Baklanoff, Eric N. (1998). "Cuba on the Eve of the Socialist Transition: A Reassessment of the Backwardness-Stagnation Thesis".Cuba in Transition, Volume8. Silver Spring,MD:ASCE. ku.260–272.ISBN0-9649082-7-1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2014-09-07. Iliwekwa mnamo25 Machi 2013.{{cite book}}:External link in|chapterurl= (help);Invalid|ref=harv (help);Unknown parameter|chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Espino, María Dolores (2000). "Cuban Tourism During the Special Period".Cuba in Transition, Volume10. Silver Spring,MD:ASCE.ISBN0-9649082-8-X. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2014-09-07. Iliwekwa mnamo25 Machi 2013.{{cite book}}:External link in|chapterurl= (help);Invalid|ref=harv (help);Unknown parameter|chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Gleijeses, Piero (1997). "The First Ambassadors: Cuba's Contribution to Guinea-Bissau's War of Independence".Journal of Latin American Studies.29 (1): 45–88.doi:10.1017/s0022216x96004646.JSTOR158071.{{cite journal}}: CS1 maint: ref duplicates default (link)
Pérez-López, Jorge F. (1996). "Cuban Military Expenditures: Concepts, Data and Burden Measures".Cuba in Transition, Volume6. Washington,DC:ASCE. ku.124–144.ISBN0-9649082-5-5. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2014-09-07. Iliwekwa mnamo25 Machi 2013.{{cite book}}:External link in|chapterurl= (help);Invalid|ref=harv (help);Unknown parameter|chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Ramazani, Rouhollah K. (1975).The Persian Gulf and the Strait of Hormuz. Alphen aan den Rijn: Sijthoff & Noordhoff.ISBN90-286-0069-8.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help)
Scheina, Robert L. (2003).Latin America's Wars, Volume I: The Age of the Caudillo, 1791–1899. Dulles,VA: Brassey's.ISBN978-1-57488-449-4.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help)
Smith, Kirby; Llorens, Hugo (1998). "Renaisssance and Decay: A Comparison of Socioeconomic Indicators in Pre-Castro and Current-Day Cuba".Cuba in Transition, Volume8. Silver Spring,MD:ASCE. ku.247–259.ISBN0-9649082-7-1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2014-09-07. Iliwekwa mnamo25 Machi 2013.{{cite book}}:External link in|chapterurl= (help);Invalid|ref=harv (help);Unknown parameter|chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo yaBahari ya Karibi bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuKuba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.