Kondoo-kaya (Ovis aries) ni mnyama afugwaye na binadamu kwa sababu yanyama,sufu na piamaziwa. Kondoo hula manyasi na kutembea kwa vidole viwili.
Asili yake ni aina za kondoo wa pori waliofugwa kwa sababu ya nyama na maziwa. Katika nchi yenye baridi sufu au nywele zake inatafutwa sana kwa sababu nguo za sufu ni kinga nzuri dhidi ya baridi.
Wataalamu wamegundua kwamba asili ya kondoo-kaya wote ni kondoo wa porini kutokaKaukazi ambako ufugaji wa mnyama huyu ulianzishwa na kuenea.
Kondoo wako katikafamiliaBovidae pamoja naspishi zang'ombe na kama hawa wanacheua chakula chao na huwa na tumbo lenye vyumba vinne. Baada ya kula nyasi mara ya kwanza wanairudisha kutoka chumba cha kwanza cha tumbo na kuitafuna tena. Kwa njia hii wanapata lishe nyingi kutoka nyasi.
Kiuchumi matumizi yake siku hizi ni hasa kwa nyama. Maziwa hutumiwa zaidi kwajibini kama feta. Umuhimu wa sufu umepungua kutokana na uenezaji wa nguo za sintetiki.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuKondoo-kaya kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.