Ramani ya Kolombia Kolombia (kwaKihispania :República de Colombia ) ni nchi kwenye pembe la kaskazini laAmerika ya Kusini .
Imepakana naVenezuela ,Brazil ,Ekuador ,Peru naPanama . Inapwani mbili, kwenyePasifiki naAtlantiki .
Jina la nchi limeteuliwa kwa heshima yaKristoforo Kolumbus (Kihisp. : Cristóbal Colón; kwaKiitalia : Cristoforo Colombo) aliyegundua njia kati yaHispania naAmerika mwaka1492 .
Upande wamagharibi wa nchi unamilima yaAndes inayopatikana kwasafu tatu za milima zinazoitwa "Kordileri".
Kati ya milima hiyo kunachanzo cha mito miwili mikubwa ya nchi: ndiyoRio Cauca naRio Magdalena inayoishia katikaBahari ya Karibi (Atlantiki).Mto mkubwa upande wa magharibi niAtrato unaoishia Pasifiki.
Milima ya juu niPico Cristobal Colon naPico Simon Bolivar yenyekimo chamita 5,775 juu yaUB kila mmoja.
Sehemu ya mashariki ya Kolombia nitambarare yenyemisitu minene. Mito yake, kama vilePutumayo ,Yapura ,Meta naGuaviare inaishia ama katika mtoOrinoko au kwenyeAmazonas .
Kolombia ina visiwa katika bahari zote mbili.
Upande wa Karibi / Atlantiki kunafunguvisiwa vyaSan Andres na Providencia vilivyoko baharinikm 770 kutokabara . Karibu na pwani ya Karibi nikisiwa chaFuerte na funguvisiwa vyaSan Bernardo nadel Rosario .
Visiwa vyaMalpelo ,Gorgona naGorgonilla viko katika Pasifiki.
Miji mikubwa nimji mkuu Santa Fé de Bogotá ,Medellín ,Cali ,Cartagena de Indias ,Barranquilla ,Ibagué ,Manizales ,Pasto ,Cúcuta naBucaramanga .
Mataifa asilia ya Waindio walikuwaWachibcha ,Waarawak naWakaribi .
Hasa Wachibcha waliokalianyanda za juu walikuwa nautamaduni wa kimaandishi; walitumiakalenda ,hesabu naalfabeti yao. Lakini hawakujenga miji na madola yao yalikuwa madogo.
Wahispania walijenga miji ya kwanza:Santa Marta (1527 ) naCartagena de Indias (1533 ) kwenye pwani. Tangu mwaka1537 waliingia katika nyanda za juu na kuvamia maeneo ya Wachibcha. Hapo walijenga miji yaSanta Fé de Bogotá naTunja (yote miwili1539 ).
Baadaye Kolombia ilikuwakitovu chaufalme mdogo waGranada Mpya .
Tangu mwaka1813 kiongozi Simon Bolivar alipiganiauhuru wa makoloni ya Amerika ya Kusini. Mwaka1819 Jamhuri ya "Gran Colombia" (Kolombia kubwa) iliundwa ikadumu hadi1831 . Baadaye iliachana kuwa nchi za pekee za Kolombia (pamoja naPanama ),Venezuela naEcuador .
Kolumbia ilionavita za wenyewe kwa wenyewe ; wakati wa "vita ya siku 1000 "Marekani ilitumiaudhaifu wa nchi na kusaidiaghasia katikaPanama iliyosababishauasi wa Panama kuwa nchi ya pekee mwaka1903 .
Sehemu ya pili yakarne ya 20 iliona vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoendelea hadi mwaka2016 . Sehemu za nchi zilikuwa chini yawanamgambo wanaodumishautawala wao kwabiashara yamadawa ya kulevya , hasakokain .
Kuna wakazi milioni 41: wengi wakomjini hasa katika mabonde yaRio Cauca naRio Magdalena na kwenyemwambao wa bahari ya Karibi.Mwaka2014 asilimia 76 za wakazi wote wa nchi walikaa mjini.
Kunauhamiaji mkubwa kutoka mashambani kuelekea mjini. Mikoa ya mashariki ina zaidi ya nusu ya eneo la taifa lakini asilimia 3 za wakazi pekee.
Asili ya wakazi ni ya mchanganyiko wa vikundi vitatu:
Sehemu kubwa ni machotara waWaindio naWazungu (takriban 49%), halafuWazungu (37%), machotara wa Kiafrika na Wakolombia wenye asili tupu ya Afrika (10.6%). Wenye asili tupu ya Waindio ni 3.4%.
Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania (99.2%).
Upande wadini , asilimia 90 niWakristo , hasa waKanisa Katoliki (70.9%) na wamadhehebu mbalimbali yaUprotestanti (16.7%).
WikiMedia Commons Makala hii kuhusu maeneo yaAmerika Kusini bado nimbegu . Je unajua kitu kuhusuKolombia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari .