Kiasili wenyeji wa Amerika Kusini walitafuna majani ya koka jinsi watu waAfrika ya Mashariki naArabia hutafuna majani yamiraa, kwa jina linginemirungi.
Kiasi chadawa kinachopatikana katika majani hakiletiulevi bali hutulizanjaa na kuondoauchovu.
Tangumwaka1860wanakemia wameweza kuondoa dawa tupu kutoka majani kama unga. Kutokana na matumizi yatiba watu walianza kuonja dawa na kutambua uwezo wake wa kusababishandoto na hali ya kujisikiaraha. Ilionekana baadaye ya kwamba kokain inatabia kama madawa mengine ya kulevya ya kuwa watu huzoea haraka kiasi cha kutawaliwa na dawa: hawawezi kuiacha (uraibu).
Siku hizi sehemu kubwa ya kokain hutegenezwa kwa matumizi ya dawa ya kulevya. Nje ya masharti ya tiba matumizi yake ni marufuku, lakini watu hupenda ndoto wanazopata kutokana na matumizi yake.
Marawakitawaliwa na dawa huona haja ya kurudiarudia matumizi yake. Kwa sababu hiyobiashara ya kokain inazalishapesa nyingi hata kama ni marufuku.
Majani ya koka huvunwa hasa katika nchi zaKolombia,Peru naBolivia.Maabara kubwa zasiri za kuondoa dawa ya kokain tupu ziko hasa Kolombia.
Mabwana wa biashara hii nimatajiri wakitumiawanamgambo wanaolinda eneo la maabara dhidi yapolisi. Kiasi cha pesa inayopatikana kimetosha mara kwa mara kuhongawanasiasa namaafisa wa juuserikalini na hivyo kupata nafasi ya kuendesha maabara pamoja na biashara inayotumiandege ndogo zinazopeleka kokain nje, ama moja kwa moja hadiMarekani au hadivisiwa vya Karibi ambako hufikishwa kwenyemeli kwa biashara ya kimataifa.
Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuKokain kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.