Koho nindege wakubwa kiasi wajenasiPandion, jenasi pekee yafamiliaPandionidae. Zamanispishi moja tu ilifahamiwa, lakini bingwa kadhaa wamekupanususpishi yaAustralasia cheo cha spishi sasa[1] na IOC (Muungano wa Kimataifa wa Wataalamu wa Ndege) unaiafiki. Lakini wataalamu wengine hawakubali.
Mwili wa koho ana sm 50-66 na upana wa mabawa ni sm 127-180. Mgongo wake una rangi ya kahawa na kidari na tumbo ni nyeupe. Mara nyingi kidari kina michirizi kahawia. Kichwa ni cheupe chenye kinyago. Vidole vyote vina urefu sawa na vina kucha za mviringo bila mfuo kinyume navipanga na jamaa. Kidole cha nje kinaweza kugeuzwa kuelekea nyuma, kiasi kwamba koho anaweza kushika mawindo kwa vidole viwile mbele na viwili nyuma. Hii inafaa hasa akikamatasamaki wenye kuteleza. Koho hula samaki takriban pekee, lakini pengine hukamatawagugunaji,amfibia,watambaazi na ndege wengine. Hutengeneza tago lao kwa vijiti juu yamti, mhimili ya huduma za umma aumwamba. Jike huyatagamayai 2-4.
- Pandion cristatus (Eastern Osprey)
- Pandion haliaetus (Western Osprey)
- Pandion h. carolinensis (American Osprey)
- Pandion h. haliaetus (Eurasian Osprey)
- Pandion h. ridgwayi (Caribbean Osprey)
- ↑Wink, M., Sauer-Gürth, H. and Witt, H-H. (2004) Phylogenetic differentiation of the OspreyPandion haliaetus inferred from nucleotide sequences of the mitochondrial cytochrome b gene. Pp. 511-516 in R.D. Chancellor and B-U. Meyburg (eds.)Raptors worldwide. World Working Group on Birds of Prey, Berlin, and MME/BirdLife Hungary, Budapest.