Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kilomita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaKm)
Ufafanuzi wa awali wa kilomita

Kilomita (pia:kilometa) nikipimo chaurefu. Kinamaanisha urefu wamita 1,000.Kifupi chake ni km.

Kilomita ni kipimo cha kawaida katikamaisha ya kila siku cha kupimiaumbali usio karibu. Umbali kati yamiji hupimwa kwa kilomita.

Kilomita ni sehemu ya vipimo vyaSI vyenye msingi wamita.

Katika nchi mbalimbali kilomita imechukua nafasi ya vipimo vingine kamamaili auverst.

Kwa umbali mkubwa mno kama kwa vipimo vyaastronomia kilomita haifai tena. Hapo kuna vipimo vingine. Kwa mfano umbali kati yamwezi nadunia inaweza kutajwa kwa kilomita nilakhitatu au km 300,000. Umbali kati ya Dunia na Jua ni km 150,000,000 na kwa umbali huo kizio chakizio astronomia hutumiwa. Lakini umbali kutokajua letu hadinyota nyingine ni mkubwa mno. Hapa vipimo kamamwakanuru au piaparsek hutumiwa.

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kilomita&oldid=1135470"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp