Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Klemens wa Aleksandria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaKlementi wa Aleksandria)
Klemens wa Aleksandria (150-211/216).

Titus Flavius Clemens (anayejulikana zaidi kamaKlemens wa Aleksandria; kwaKigiriki: Κλήμης Αλεξανδρεύς, Klemes Alexandreus;Athens,150 hivi;Aleksandria,215 hivi) alikuwamwanafalsafa namwanateolojia waUkristo katikamji waAleksandria (Misri) mwanzoni mwakarne ya 3[1].

Huhesabiwa kati ya walimu muhimu waKanisa la kwanza.

Anaheshimiwa naWaorthodoksi wa Mashariki,Waanglikana na wengineo kamamtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwatarehe4 Desemba[2].

Maisha

[hariri |hariri chanzo]
Opera omnia, 1715

Klemens alikuwa mwenyeji waUgiriki aliyezaliwa katikafamilia yawapagani matajiri mjiniAthens.

Baada ya kupokeaimani ya Kikristo, alisafiri akitembelea walimu Wakristo katika nchi mbalimbali kama vile Ugiriki,Italia naPalestina hadi Misri.

Huko alipewa nafasi ya kufundisha kwenyeChuo cha Kikristo cha Aleksandria akishirikiana na mwanzilishi wakePanteno.

Jitihada ya Klemens ilikuwa kupatanisha imani ya Kikristo na dhana zafalsafa ya Kigiriki. Alifaulu kufafanua Ukristo kwa wasomi wapagani na kuvuta wengi kwenye imani yake mpya.

Klemens alikuwa ndiye mwalimu waOrigene.

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. https://dacb.org/stories/egypt/clement-of-alex/
  2. https://catholicsaints.info/saint-clement-of-alexandria/

Maandishi

[hariri |hariri chanzo]

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Klemens_wa_Aleksandria&oldid=1313716"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp