Ugunduzi wainjini ya mvuke uliunda msingi wa matumizi ya mashine katika shughuli nyingi za uzalishaji. Pamoja na hayo, mashine hizi zilikuwa nagharama kubwa, hivyo ulimbikizaji warasilmali uliundatabaka mpya yamabepari.
Kuenea kwa viwanda kulisababisha mabadiliko makubwa katikajamii zadunia. Mafundi wa weledi nyingi walipoteza nafasi zao kwa sababu bidhaa zilitengenezwa sasa kwabei nafuu na katikamuda mfupi, mara nyingi pia kwaubora mkubwa kuliko jinsi mafundi walivyoweza kuzitoa kwakazi ya mikono. Lakini viwanda vimeleta pia kazi mpya naufundi tofauti na awali.
Uzalishaji wa bidhaa katika viwanda umekuwa msingi muhimu wa mchakato wautandawazi ambako bidhaa nyingi zinazalishwa katika nchi fulani na kuuzwa koteduniani ilhali vipuli vya kutengenezea bidhaa hizi tena zinatoka katika nchi tofauti.
Zipo nchi zenye viwanda vingi zaidi; nchi yenye viwanda vingi ni nchi tajiri, kwa mfanoJapani. Viwanda vyake ni vya kutengeneza bidhaa kubwa na nzito zaidi, kama vilemeli,ndege,treni, magari n.k.
Faida na hasara
Kila nchi ina viwanda mbalimbali. Viwanda hivyo huisaidia nchi hiyo pindi iuzapo bidhaa hizo, pia huisaidia nchi husika kunufaika kiuchumi kwa uwepo wa viwanda hivyo.
Viwanda vinafaida kubwa sana katika nchi yenye viwanda hivyo; faida hizo ni:
Tunapokuwa na viwanda tunanufaika kwa vitu vingi. Lakini viwanda vina madhara pia, tena mengi sana. Madhara hayo ni:
1)moshi unaotoka viwandani huharibuanga hewa (ozon layer) ambapoanga linapotoboka husababisha kuwa najoto kali sana,
2)majitaka yanayotiririshwa kwenyemito husababisha madhara kwaviumbehai wamajini na watu wanaotumia maji ya mto huo,
3)uchafu unaobaki husababishamagonjwa mbalimbali ya milipuko,
4) viwanda hutoahewa chafu ambayo husababisha matatizo yaupumuaji kwa ujumla.
Kwa hiyo tuvitunze viwanda vyetu ili vilete faida, si kuangamiza watu na viumbe wengine.
Makala hii kuhusu mambo yauchumi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuKiwanda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.