Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kivuli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wakati wa jioni kivuli huwa ndefu

Kivuli ni eneo lenyenuru kidogo katikamazingira yenye nuru zaidi. Kinapatikana nyuma yakitu kinachoangazwa upande mmoja lakini kinazuia nuru kuendelea na hivyo kuunda eneo lenyegiza au nuru kidogo nyuma yake.

Kila kitu kisichopitisha nuru ndani chake kinaweza kuwa na kivuli kikiangazwa upande mmoja. Mfano wagimba ambalo halina kivuli nihewa au piakioo safidirishani.

Kwa maana pana zaidi kuna pia kivuli chamnururisho usio nuru ya kuonwa kwamacho;mata ogania ndani yamwili unapitisha au kuzuiamnururisho waeksirei kwaviwango tofauti na kuonekana baadaye kwenyepicha kwarangi tofauti kutokana na "kivuli" dhidi yamionzi hiyo.

Ukubwa na umbo la kivuli

[hariri |hariri chanzo]

Ukubwa wa kivuli unategemeaumbali wa gimba lenye kivuli na chanzo cha nuru. Kama gimba liko karibu na chanzo cha nuru kivuli huwa kikubwa zaidi, kama liko mbali kivuli huwa kidogo. Ukiwekamkono karibu natochi kivuli chake huwa kikiubwa, kadiri unavyopeleka mkono mbali na tochi kivuli chake kinapungua.

Kivuli kamili (A) na nusu kivuli (B) kutokana na vyanzo viwili vya nuru (N1 + N2)

Vilevileumbo la kivuli unategemeapembe ya kijiometria kati ya chanzo cha nuru na gimba. Hii inaonekana kwa kuzatama kivuli chamtu aunyumba wakati wamchana na wakati wajioni. Jionijua linaonekana chini zaidiangani, hivyo pembe ya nuru yake ni ndogo na kivuli kirefu. Kama jua liko juu kabisa angani kivuli huwa kidogo maana nuru inafika kutoka pande nyingi, hivyo kivuli kina nafasi ndogo tu, ni "fupi". Kama jua liko "chini" wakati waasubuhi au jioni linaangaza upande mmoja tu, hivyo nafasi ya kivuli inakua.

Aina za vivuli

[hariri |hariri chanzo]

Kama chanzo cha nuru kinafanana nanukta, kivuli ni kikali yaani kuna kivuli kamili tu kinachokaribia ranginyeusi. Tofauti kati ya kivuli na eneo lenye nuru ni kali kamamstari uliochorwa. Lakini kama chanzo cha nuru ni kipana zaidi kuna ngazi mbili za kivuli yaani kivuli kamili (en:umbra) na nusu kivuli (penumbra). Kati ya nusu kivuli na maeneo yenye nuru mpaka si mkali tena.

Mchezo wa Kivuli hukoBali,Indonesia.

Hali ya nusu kivuli inatokea pia kama gimba lilelile linaangazwa na vyanzo viwili vya nuru.

Kama chanzo cha nuru ni kipana sana kama anga lililofunikwa namawingu kivuli kinaweza kupotea kabisa. Maana kiasi cha nuru kinatokea kote angani.

Kivuli na sanaa

[hariri |hariri chanzo]

Tangu kale watu walitumia kivuli kwamchezo na kutumia matokeo yake katikauchoraji.

Mchezo unaopendwa ni kupeleka mkono mbele ya chanzo cha nuru kamamshumaa autaa na kuunda kivuli kinachofanana nauso aumnyama fulani.

Katika nchi nyingiwasanii waliendelea kutumia maumbo ya watu, wanyama na vitu vingine vilivyokatwa katikakaratasi na kuleta sura ya umbo kwenyekitambaa cheupe yakiangaziwa na nuru kwa nyuma.

Picha za vivuli

[hariri |hariri chanzo]
  • Kivuli cha maandishi kinageuza mwelekeo wake.
    Kivuli cha maandishi kinageuza mwelekeo wake.
  • Wakati wa mchana: kivuli kifupi
    Wakati wa mchana: kivuli kifupi
  • Kivuli kamili na nusukivuli chumbani kutokana na kipande cha pazia dirishani
    Kivuli kamili na nusukivuli chumbani kutokana na kipande cha pazia dirishani
  • Mchezo wa kivuli unaoonyesha picha ya ndege
    Mchezo wa kivuli unaoonyesha picha ya ndege
  • Mchezo wa kivuli nchini Indonesia

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kivuli&oldid=1359856"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp