Muundo wa kiunzi cha mifupa
Mfumo wa kiunzi cha mifupa cha wanyamakordata ni mifupa thabiti inayounganishwa kwagegedu. Mifupa hii inasogezwa kwa musuli zinazofungwa kwa mfupa kwakano. Gegedu inapatikana kwamamalia hasa kwenye viungo vya mifupa. Kuna wanyama wengine kamapapa ambako kiunzi chote kimejengwa kwa gegedu.
Pamoja na kupa mwili uthabiti na kuruhusu mwendo mifupa ni pia nafasi ya kuhifadhi minerali hasakalsi nafosfati.
Sehemu kuu ya kiunzi cha mifupa niuti wa mgongo. Unashika mifupa yote kwa pamoja kuanziafuvu hadimabavu hadi mifupa ya chini inayokutana katikafupanyonga. Unakinga ndani yake pianeva kuu zinazoelekea kutokaubongo kwenye fuvu hadi sehemu mbalimbali ya mwili.
Kiunzi cha binadamu huwa na mifupa 206. Mifupa inaunganishwa kwenye viungo kwa nyugwe inayowezesha mwili kuwa nyumbufu. Kano huunganisha mfupa namisuli ikipeleka nguvu ya misuli kwa mfupa.
Kati ya wanyama kuna pia aina zenyekiunzi cha nje au zisizo na kiunzi.Arithropodi kamawadudu huwa na kiunzi cha nje.