Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kitabu cha Hosea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hosea na mke wake Gomeri katikaBible Historiale,1372.

Kitabu cha Hosea ni kimojawapo kati yavitabu vyaTanakh (yaaniBiblia ya Kiebrania), na hivyo pia vyaAgano la Kale katikaBiblia ya Kikristo.

Kwa kuwa kinasura 14 tu, kimepangwa tangu zamani za kale kati ya vitabu 12 vyaManabii Wadogo.

Hata hivyo umuhimu wake katika maendeleo yaUfunuo wa Mungu kwaIsraeli ni mkubwa, kwa jinsi kilivyoathiri vitabu vilivyofuata hadiKitabu cha Ufunuo.

Kama vitabu vingine vyote vyaBiblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wahistoria ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo hayo.

Muda wa unabii wa Hosea

[hariri |hariri chanzo]

NabiiHosea alitokeaUfalme wa Israeli (Kaskazini) ambapo alifanyakazi yaunabii kuanzia miaka ya mwisho yautawala waYeroboamu II (786 -746 KK) hadi karibu na maangamizi ya mwaka722 KK ambayo aliyatabiri kutokana nauasi wa kidini wa Waisraeli wenzake.

Wakati huohuo walifanya kazi piaAmosi upande wa Kaskazini, halafuIsaya katikaUfalme wa Kusini (Yuda).

Mada kuu

[hariri |hariri chanzo]

Hosea alitangaza hasaupendo waMungu kwataifa lake.Adhabu zenyewe zilizotabiriwa zinaelezwa kuwa zimetokana na upendo huo wenyewivu ambao unalenga kuwarudisha Waisraeli katika upendo mwaminifu wakiuchumba.

Hosea alikuwa wa kwanza kumfananishaMwenyezi Mungu namume mwaminifu wamwanamkemalaya.

Maisha ya nabii mwenyewe yalikuwa natabu ya namna hiyo ili yawe kwa wote kielelezo che uhusiano kati ya Mungu na watu wake.

AlidaiWaisraeli wawe waaminifu kwa Mungu pekee, pamoja na kusisitiza kuwadini haiwezi kuishia katikaibada zisizohuishwa na upendo, la sivyo wataangamia.

Muhtasari

[hariri |hariri chanzo]

Mwanzoni mwa kitabu, Hosea aliagizwa na Munguamuoekahaba atakayemzaliawanaharamu anayewakilisha taifa laIsraeli lililoabudumiungu mingine pia kamaasili yaustawi wake na kutegemeambinu za kisiasa ili kujidumisha salama.

Kwa kuwa hawakumtegemea Mungu wao, Hosea aliwatabiria Waisraeli watapelekwauhamishoni hukoAshuru.

Kama vile mke wa Hosea alivyoweza kujirekebisha, hivyo hata Israeli ikitubu itaokoka na kufaidika nabaraka za Mungu.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Vitabu vyaAgano la Kale

Mwanzo *Kutoka *Walawi *Hesabu *Kumbukumbu *Yoshua *Waamuzi *Ruthu *Samueli I *Samueli II *Wafalme I *Wafalme II *Mambo ya Nyakati I *Mambo ya Nyakati II *Ezra *Nehemia *TobitiDK *YudithiDK *Esta *Wamakabayo IDK *Wamakabayo IIDK *Yobu *Zaburi *Methali *Mhubiri *HekimaDK *SiraDK *Wimbo Bora *Isaya *Yeremia *Maombolezo *BarukuDK *Ezekieli *Danieli *Hosea *Yoeli *Amosi *Obadia *Yona *Mika *Nahumu *Habakuki *Sefania *Hagai *Zekaria *Malaki

Alama yaDK inaonyesha vitabu vyadeuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuKitabu cha Hosea kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kitabu_cha_Hosea&oldid=1331616"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp