Kisiwa kipo takriban 1500 km upande wa mashariki ya Australia. Pamoja na visiwa vidogo jirani vya Nepean na Phillip ni ya asili ya kivolkeno hivyo kuna ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo.
Kisiwa kiliwahi kukaliwa na Wapolynesia jinsi inavyoonekana kwa mabaki ya kijiji kilichogunduliwa na waakiolojia na kuwepo kwapanja nandizi ambazo zilisambazwa na Wapolynesia kwenye visiwa vya Pasifiki.
Lakini wakati wa kufika kwa nahodha MwingerezaJames Cook mwaka 1774 kisiwa kilikuwa bila watu. Cook alikipa jina laNorfolk kwa heshima ya kabaila Mwingereza fulani aliyeitwa hivyo.
Kuanzia 1788 kisiwa kikakaliwa na wafungwa kutoka magereza ya Uingereza na Australia. Lakini majaribio haya yameachwa tena na makambi ya wafungwa kuhamishwa penginepo.
Mwaka 1856 mababu wa kwanza wa wakazi wa leo walifika kutokaPitcairn. Idadi ya wajukuu wa waasi wa Bounty ilikuwa imeongezeka mno kwa kisiwa kidogo na serikali ya Uingereza iliwahamisha watu 194 kwenda Norfolk.
Leo hii theluthi moja ya wakazi wa Norfolk ni wa asili ya Pitcairn. Wengine wamekuja kutoka Australia au kutoka Polynesia.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuiongezea habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.