Jina limetokana nammonaki namtaalamuMgirikiMt. Sirili (827 -14 Februari869) aliyesemekana aliunda namna hiyo ya mwandiko kwa ajili yalugha za Kislavoni pamoja na mdogo wakeMt. Methodio.
Hali halisi hawakuanzisha aina hii ya alfabeti lakini waliendeleza namna ya kuiandika iliyosaidia kusambaza mwandiko kati ya mataifa wasemaji wa lugha za Kislavoni. Lugha hizo zinasauti kadhaa ambazo hazinaherufi katika alfabeti yaKilatini. (Mwandiko wa Kilatini hutumiwa siku hizi kwa lugha nyingiduniani, zikiwa pamoja naKiswahili naWikipedia hii.)
Kuna lugha za Kislavoni, kama vileKipolandi,Kicheki naKikroatia, zinazoandikwa kwaalfabeti ya Kilatini, lakini kunaalama za nyongeza kwa ajili ya sauti za pekee za lugha za Kislavoni kwa mfano: "Č" kwa sauti ya "tsh" au "Ž" kwa aina ya "sh laini".
Alfabeti za Kisirili zinatofautiana kiasi kati ya lugha na lugha; kuna namna tofauti za kuandika sauti ileile au pia herufi za pekee kwa ajili ya sauti za pekee katika lugha fulani. Alfabeti inayotumiwa na watu wengi ni ya Kirusi inayoonyeshwa hapa.
Lugha za Kislavoni zinazoandikwa kwa alfabeti ya Kisirili ni: