Kipoland (język polski, polszczyzna) ni lugha rasmi kwa nchi yaPoland. Kinafahamika zaidi kwa kuzungumzwa na watu waishio Maghari mwa Slovoni na ni lugha ya pili kwa ukubwa katika orodha yaLugha za Kislavoni baada yaKirusi. Ni moja kati ya lugha ngumu kujifunza kutokana na ugumu wa sarufi zake.
Katika historia, Kipoland kilikuwa lugha muhimu katika Ulaya ya Kati na Mashariki. Leo hii, kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 38.5 ikiwa kama lugha rasmi katikaPoland. Pia kinazungumzwa kama lugha ya pili katika sehemu za magharibi mwa nchi yaBelarus,Lithuania, naUkraine.
Kutokana na kuhamahama kwa watu wa Poland wa majira tofauti, mamilion ya waongeaji wa Kipoland wanaweza kupatikana katika nchi nyingi tu kama vileAustralia,Kanada,Uingereza,Marekani, na sehemu nyingine nyingi tu. Kuna zaidi ya milioni 50 ya waongeaji wa Kipoland duniani.
Kuna takriban herufi 9 za Kipoland ambazo katika Kiingereza hakuna. Zinaonekana kuwa kama Kiingereza, lakini zenyewe zinaviji alama kwa juu au kwa chini.
Katika herufi ndogo, herufi tisa ni: ą ć ę ł ń ś ó ź ż
Katika herufi kubwa, herufi tisa ni: Ą Ć Ę Ł Ń Ś Ó Ź Ż
Kuna herufi 3 katika Kiingereza ambazo katika Kipoland hazitumiki: q, v, x.
Kuna mchanganyiko wa herufi 7 katika kila herufi 2 ambazo zote zinaonekana kuwa kama sawa katika kusikika (ambazo sawa na "th" au "qu" katika Kiingereza). Ambazo zimejumlisha herufi kama vile "ch", "cz", "dz", "dź", "dż", "rz", "sz".
Lugha ya Kipoland ina lafudhi nyingi sana, lakini ni chache mno kuliko lugha zingine za Ulaya. Kuna utofauti mdogo tu katika Kipolanda cha "kawaida", lakini kila mwongeaji anaweza kumwelewa mwenziwake, na wale ambao wao sio wazawa wa lugha hiii kawaida hawezi kujua tofauti zao katika kutamka.
moja - jeden mbili - dwa tatu - trzy nne - cztery tano - pięć sita - sześć saba - siedem nane - osiem tisa - dziewięć kumi - dziesięć kumi na moja - jedenaście kumi na mbili - dwanaście ishirini - dwadzieścia ishirini na moja - dwadzieścia jeden thelathini - trzydzieści arobaini - czterdzieści hamsini - pięćdziesiąt mia moja - sto elfu moja - tysiąc