Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kiongozi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Julius Caesar, mmojawapo kati ya viongozi maarufu zaidi katikahistoria.

Kiongozi ni mtu ambaye huongoza wa wenzake, ama mmojammoja ama katika kikundi.

Mara nyingi kiongozi hupewaheshima ya juu katikajamii au kikundi cha watu kuanzia katikafamilia ambapo huheshimiwa na wote katika eneo husika analolisimamia.

Kiongozi katika familia

[hariri |hariri chanzo]

Kiongozi katikafamilia huwa ni mtu aliye naumri mkubwa katika familia husika, ambapo viongozi huwa nibaba namama. Katika familia nyingi baba ndio huwa kiongozi mkubwa akifuatiwa na mama.

Pia familia huweza kuwa na kiongozi waukoo ambapobibi nababu huwa viongozi wa juu katika ukoo.

Kiongozi katika jamii

[hariri |hariri chanzo]

Katika nchi nyingi duniani kiongozi hupatikana kwa wananchi kupigakura ambapo watu mbalimbali wanaogombeauongozi hupigwa kura kwa ajili ya kuwa kiongozi katikajamii au kikundi cha watu hupatikana.

Mara nyingine kiongozi huchaguliwa kwa kuteuliwa na mtu mmoja pasipo kupigwa kura.

Pia katika jamii nyingine kiongozi hupatikana kwa kurithi, ambapomrithi huwa kiongozi kwa kurithi uongozi kutoka kwa kiongozi aliyefariki na kuachiamadaraka.

Kiongozi kadiri ya Biblia

[hariri |hariri chanzo]

KatikaBiblia kiongozi ni mtu ambaye humwakilishaMungu katika kuongoza watu wake hapaduniani[1]. Hivyo anapaswa kukumbuka kwamba ameshirikishwamamlaka ya juu na kwamba atapaswa kuhukumiwa kwa namna alivyoitumia.

Yesu alisema kwa kawaida watawala hutumia mabavu na hata hivyo hupenda kuitwa wafadhili.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. https://www.vaticannews.va/sw/church/news/2018-07/uongozi-wa-kanisa-ni-huduma-ya-neno-upendo-na-sakramenti.html
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuKiongozi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kiongozi&oldid=1392120"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp