Kikalio cha Dhahabu (kwaKiashanti -Kitwi:Sika Dwa Kofi, "Kiti cha Dhahabu kilichozaliwa Ijumaa"; kwaKiingereza:Golden Stool) nikiti cha enzi cha kifalme chawafalme waUfalme wa Ashanti naishara kuu yamamlaka kuu.[1] Kulingana namapokeo,Okomfo Anokye,Kuhani mkuu na mmoja wawaanzilishi wakuu waufalme wa Ashanti, alisababisha kikalio hicho kushuka kutokambinguni na kutua kwenyepaja laOsei Tutu aliyekuwa mfalme wa kwanza wa Ashanti.[2]
Kikalio cha Dhahabu kinaaminika kuwa naroho[3] yataifa la Ashanti ndani yake.
Vita nyingi[4] zimeibuka juu yaumiliki wakiti hicho cha kifalme.[5] Mnamomwaka wa1900,SirFrederick Hodgson,GavanaMwingereza waGold Coast, alitaka[6] kukalia Kikalio cha Dhahabu akaamuru kipelekwe mbele yale. LakiniWaasante walikificha. Ufatwaji wa kiti ulisababishauasi wenyesilaha unaojulikana kamaVita ya Kikalio cha Dhahabu, ambayo ilisababisha maeneo ya Ashanti kutwaliwa naUingereza na kuwakoloni. Lakini Waingereza walishindwa kupata kiti.
Mnamo1921,wafanyakaziWaafrika kadhaa waliojengabarabara waligundua kikalio cha dhahabu wakavuamapambo kadhaa yadhahabu. Walikamatwa na Waingereza, kabla ya kuhukumiwaadhabu ya kifo kulingana namila ya Ashanti. Waingereza waliingilia kati na badala yake wahukumiwa walifukuzwa katika Ghana. Haposerikali ya kikoloni iliahidi kwamba haitaingilia tena mambo ya kikalio kikatolewa mafichoni.[7]
Mnamo mwaka wa1935 kikalio kilitumika katikasherehe ya kumtawaza Osei Tutu Agyeman Prempeh II.[8]
Kikalio cha Dhahabu ni kiti kilichopindikasm 46 juu chenye nafasi yaupana wa sentimita 61 kwa 30.[9]Uso wake wote umepambwa kwa dhahabu, na umetundikwa nakengele kumwonyamfalme juu ya hatari inayokuja.[10] ] Haikuonekana nawatu wengi, ilhali ni mfalme tu,malkia, na washauri wanaoaminika wanajua maficho yake.
Mifano yake yametengenezwa kwa ajili yamachifu na kwenyemazishi yao hupakwadamu yawanyama.[11] ] Kikalio cha dhahabu ni moja yaishara kuu za Asante leo kwa sababu bado inaonyesha mfululizo wa kifalme namamlaka.[12]
Kuhusu kiti kama ishara ya mamlaka:Ukulu mtakatifu
{{cite news}}
: CS1 maint: date auto-translated (link){{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)