Ufafanuzi waumri maalumu wa ujana hutofautiana. Ukomavu wa mtu binafsi huenda unakosa kuwa sawa na umri wao, kwani watu wasiokomaa hupatikana katika umri wowote. Umri ambao mtu anahesabiwa ni "kijana", na anastahili huduma maalumu chini yasheria na katikajamii unatofautianaduniani kote. Mifano:
Mwaka 2015,Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio ambalo linatambua ukuaji wa hisia kali kati ya vijana kama tishio kwa utulivu na maendeleo (vijana katika azimio hili hufafanuliwa kama watu wenye umri wa miaka 18-29). Hati hiyo iliwasilishwa kwa majadiliano na mwakilishi wa Jordan, Dina Kavar, ambaye alisema: "tunajaribu kuvutia umakini wa jamii ya ulimwengu ili vijana wapate umakini wanaostahili, wakati ambapo ulimwengu umekuwa mahali ambapo shida zaidi na zaidi zinaonekana.[4]
Mkataba wa Vijana wa Afrika unafafanua kama vijana watu wenye umri wa miaka 15-35.[5]
"Muda katika maisha ya mtu kati ya utoto na utu uzima. Neno "kijana" kwa ujumla linahusu wale walio kati ya miaka 15 hadi 25. "-Benki ya Dunia.[6]
Kila kijana anawajibu wa kufanyakazi kwabidii ilimaendeleo ya nchi yake yaweze kwenda sawa, kwani kwa kufanya kazi anaepuka zaidimmomonyoko wa maadili uliokithiri kwa vijana, hasa kuiga mambo ya kigeni yasiyo na manufaa kwao na kwataifa kwa ujumla.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuUjana kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.