Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Kiingereza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaKiingereza lugha)
"en" inaelekezwa hapa. Kwa matumizi mengine, tazamaen (maana).
Kiingereza
English (en)
Lugha
AsiliUingereza
Marekani,Australia,
Nyuzilandi,Kanada,Eire
Wasemaji

L1 : 380 Milioni
L2: 1.077 Bilioni

Jumla: 1.457 Bilioni[1]
Familia za lughaKihindi-Kiulaya
Kijerumaniki
Kijerumaniki cha Magharibi
Aina za AwaliKihindi-Kiulaya cha Kale
Kiingereza cha Kale
Kiingereza cha kati
Mfumo wa kuandikaKilatini
Lugha Rasmi
Lugha rasmi kwaNchi 57
Nambari za Msimbo
ISO 639-1en
ISO 639-2eng
Glottologstan1293

      Kiingereza ni lugha ya kwanza ya wananchi wengi;
      Kiingereza ni lugha rasmi au lugha ya pili lakini si lugha ya kwanza ya watu wengi

Kiingereza,(Englishen) ni lugha yaKijerumaniki cha Magharibi kutoka katika familia ya lugha zaKihindi-Kiulaya, yenye asili yake niUingereza. Lugha hii ilianza kuibuka baada ya uvamizi waWaanglia-Saksoni katikavisiwa vya Britania mnamo karne ya 5 BK. Kupitia historia yake, Kiingereza kimeathiriwa na lugha nyingine, haswaaKilatini,Kifaransa, naKigiriki, ambazo zimechangia sana msamiati wake. Leo, Kiingereza ni lugha inayozungumzwa sana ulimwenguni, ikiwa na wasemaji wa asili takriban milioni 380, na zaidi ya bilioni moja wanaokitumia kama lugha ya pili au ya kigeni. Ni lugha ya kwanza katika mataifa kadhaa, yakiwemoMarekani,Uingereza,Kanada,Australia, naNyuzilandi na hutumika sana kama lugha ya kidiplomasia, biashara, sayansi, na teknolojia.

Kutokana na athari za ukoloni wa Uingereza na baadaye ukuaji waMarekani kama nguvu kuu ya kiuchumi na kiutamaduni, Kiingereza kimekuwa lugha ya mawasiliano ya kimataifa na mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa.Kwa mabadiliko yakihistoria na kiutawala, Kiingereza kimeendelea kuenea na kubadilika, kikichukua nafasi muhimu katika nyanja mbalimbali za mawasiliano na utawala.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Lugha ya Kiingereza ilianzia hukoUingereza kutokana na kuingiliana kwa lugha mbalimbali, hasa lugha za kale zaUjerumani,Denmark naUfaransa.Sehemu yakusini yakisiwa chaBritania ilikuwa ndani yaDola la Roma hadi mwanzo wakarne ya 5.Wenyeji walitumia lugha yaKikelti pamoja naKilatini chaWaroma, hasamjini.[2]

Uvamizi wa Waanglia-Saksoni: (kuja kwa Kijerumaniki

[hariri |hariri chanzo]

Baada ya Waroma makabila kutokaUjerumani yakaskazini naDenmark walianza kuvamia kisiwa hicho. Katika mwendo wakarnembili waliteka sehemu kubwa ya Uingereza ya leo isipokuwa sehemu zamagharibi kama vileCornwall naWales na sehemu za kaskazini walipoishiWaskoti.

Wavamizi walileta lugha zao zaKisaksoni naKianglia (Ujerumani ya Kaskazini) zilizounganika kuwa lugha yaKiingereza cha Kale ambacho kilikuwa karibu sana na Kijerumani cha Kale. Inaonekana ya kwamba wenyejiWakelti walio wengi walianza polepole kutumia lugha yawatawala wapya[3], wengine waliuawa au walihamia sehemu zisizo chini ya Waanglia-Saksoni.

Lugha hii iliathiriwa mara mbili. Kwanza Wadenmark ndio waliojaribu kujengaufalme wao kisiwani. Waliteka sehemu za Uingereza ya Magharibi. Kiasi cha maneno kutoka lugha yao kimeingia Kiingereza cha kale kama Wales.

Uvamizi wa Wanormandy: kuja kwaKifaransa, lugha mbili kando

[hariri |hariri chanzo]

Mwaka1066jeshi laWanormani kutokaUfaransa ya Kaskazini walivamia na kuteka Uingereza. Wanormani walikuwa wa asili yaSkandinavia lakini walikuwa wameshaanza kutumia lugha yaKifaransa cha kale. Wanajeshi hao walikuwa mabwana wapya wa Uingereza wakitumia Kifaransa chao.

Kwa karne kadhaa lugha mbili zilitumika kandokando: Kiingereza cha Kianglia-Saksoni cha watu wa kawaida na kile Kifaransa cha Kinormandy chatabaka lawatawala. Kwa jumla watawala walianza kutumia lugha yaraia lakini lugha hii ilibadilika pia kwa kupokea maneno mengi kutoka Kifaransa. Kuna makadirio ya kwamba zaidi yatheluthi moja ya maneno yote ya Kiingereza yana asili ya Kifaransa.

Kuingiliana kwa lugha zote mbili: Kiingereza cha Kati

[hariri |hariri chanzo]

Kipindi hiki cha kuingiliana kati ya Kifaransa cha mabwana na lugha ya kawaida kililetaKiingereza cha Kati. Hadi leo asili ya maneno kutoka Kijerumani na Kifaransa ni wazi kabisa.

Mfano mzuri ni maneno tofauti kwawanyama kadhaa nanyama yao:ng'ombe huitwa "cow" (sawa na Kijerumani wa Kaskazini "Kau") lakini nyama yake ni "beef" (kutokana na neno la Kifaransa kwa ng'ombe "boeuf"); vilevile "sheep" kwa mnyamakondoo na "mutton" kwa nyama yake (Kijerumani ya Kaskazini: "Schaap" - Kifaransa: "mutton"), vilevile swine=mnyama – pork=nyama (nguruwe) na calf=mnyama – veal=nyama (ndama).

Wakulimawafugaji walitumia lugha yao kwa mnyama - mabwana wasiogusa mnyama lakini hula nyama yake waliendelea kutumia neno la Kifaransa kwa ajili ya mnyama yuleyule. Maneno yote mawili yaliingia katikaKiingereza cha Kisasa lakini kwa mambo mawili tofauti.

Kiingereza cha Kisasa

[hariri |hariri chanzo]

Kiingereza cha Kisasa kimeanza natafsiri yaBiblia yaWilliam Tyndale; baadaye nawashairi muhimu kamaWilliam Shakespeare.

Teknolojia yauchapaji vitabu ilisambaza lugha hii nchini kote na kupunguza athira yalahaja mbalimbali.

Wakati ule Kiingereza kilipokea pia maneno mengi kutoka lugha zaKilatini naKigiriki zilizokuwa lugha zataaluma na sayansi hadikarne ya 18 koteUlaya.

Kiingereza cha Kisasa kimeendelea kurahisisha lugha. Lakiniurekebisho watahajia umeshindikana hadi leo hata kama kulikuwa na majaribio mbalimbali. Kutokana nahistoria yake Kiingereza kimebaki na tahajia isiyolingana namatamshi ya maneno.

MwandishiGeorge Bernhard Shaw alionyesha tatizo hilo kwapendekezo ladhihaka kwamba neno "fish" (samaki) liandikwe "ghoti": gh kama sauti ya "f" katika "cough", o kama sauti ya "i" katika "women", na ti kama sauti ya "sh" katika "nation".

Pamoja na hayo, lahaja za Kiingereza zinazidi kutofautiana, zile muhimu zaidi zikiwa zile za Britania na Marekani.

Uenezi

[hariri |hariri chanzo]

Pamoja naDola la Uingereza namakoloni yake, lugha ilieneaduniani kati yakarne ya 17 na19.

Tangukarne ya 19 idadi kubwa ya wasemaji wa Kiingereza hawaishi tena Uingerezea baliMarekani. Katika karne ileile Kiingereza kilikuwa lugha yautawala katika maeneo makubwa ya makoloni yaDola la Uingereza.

Baada ya makoloni kuwanchi huru mara nyingi Kiingereza kimeendelea kuwa lugha rasmi za nchi hizo.

Kutokana na matukio hayo yote, naMarekani kujitokeza katikati yakarne ya 20 kama nchi tawala kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia, Kiingereza kimekuwa leo lugha ya kwanza yamawasiliano duniani hata kama si lugha yenye wasemaji wengi wa lugha ya kwanza.

Pia aina nyingi zaKrioli naPijini zimetokana na Kiingereza na kudumu hadi leo.

Kiingereza nilugha rasmi pekee katika nchi za Uingereza,Marekani,Australia,Nyuzilandi,Jamaica, na nchi nyingine.

Kiingereza ni lugha rasmi pamoja na lugha nyingine katika nchi nyingi, kwa mfanoKanada (pamoja naKifaransa),India (pamoja naKihindi na lugha za majimbo),Ireland (pamoja naKigaelik),Philippines (pamoja naKitagalog).

Kwa jumla ni lugha rasmi katika nchi karibu 60, mbali yaUmoja wa Mataifa naUmoja wa Ulaya.

Kiingereza barani Afrika

[hariri |hariri chanzo]

Nchi nyingi zaAfrika zinatumia Kiingereza kama lugha rasmi, lakini niWaafrika wachache (isipokuwa Waafrika Kusini) wanaoitaja kuwa lugha ya kwanza kwao. Nchi hizo niAfrika Kusini,Eswatini,Ghana,Kamerun,Kenya,Lesotho,Liberia,Namibia,Nigeria,Sierra Leone,Zambia naZimbabwe.

Kiingereza kinazumgumzwa pia katika nchi nyingine za Afrika ambapo si lugha rasmi. Lugha nyingi za Afrika zimekopamaneno ya Kiingereza. Maneno hayo yamerekebishwa kulingana nasauti ya lugha nyingine, kwa mfano:Kiingereza:train -->Kiswahili:treni.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Ciarra Gillan."Population of English speakers" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2025-03-27.
  2. David Crystal.History of English language (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2025-03-27.
  3. Celtic and the History of the English Language, blogu ya Jonathan Owen kuhusu athira za Kikelti katika Kiingereza cha Kale

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Makala hii ni nzuri sana.
Rasmi
Kimataifa
Kitaifa
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kiingereza&oldid=1412655"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp